Neno La Leo: Nani Atauzima Mshumaa Wa Serikali?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,858
36672326_10214750163720465_7168430618957578240_n.jpg

Neno La Leo: Nani Atauzima Mshumaa Wa Serikali?
Ndugu zangu,
Miongoni mwa viongozi waliopata kuongoza dola ya Kiislam, hususan baada ya Mtume Muhammad (SAW) na baada ya masahaba, ni Amir muumini na Khalifa Umar bin Abdulaziz.
Wanazuoni wa Kiislamu wanatwambia, kwa utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ulijaa uadilifu. Si kwa viongozi tu, hata kwa raia wake.
Inasemwa kwamba moja ya mafanikio makubwa ya utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz, ni kukusanya zakka. Katika Uislamu, zakka ni ibada ya lazima kwa mwenye nacho kuwapa masikini, yatima, wajane, wasafiri, raia na wengineo wenye kuhitaji.
Watu walijengewa imani kubwa, kiasi hakuna aliyethubutu kukwepa kutoa zakka. Hata wale waliopokea zakka walikuwa waadilifu, hawakupokea zakka mara mbili kama walishapokea kabla. Wote waliostahili kupata zakka , walipata zakka. Hakika, zakka zilitolewa zikajaa mabohari.
Siku moja raia mmoja alikwenda kwenye ofisi ya Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wakati wa maongezi yao, Khalifa Umar alikuwa akihangaika kuupuliza na kuuzima mshumaa mmoja na kuwasha mwingine.
Alikuwa na mishumaa miwili mezani. Kadri mazungumzo yalivyoendelea, Umar aliendelea kufanya hivyo. Alipuliza mshumaa mmoja ukazimika, kisha akawasha mwingine.
Jambo hilo lilimstaajabisha sana mgeni wa Khalifa Umar bin Abdulaziz. Akauliza:
"Je; ni kwanini unazima mshumaa huu na kuwasha mwingine, kisha huo nao unauzima na kuwasha ule wa kwanza?
Khalifa Umar bin Abdulaziz akamjibu:
"Mshumaa huu ni wa Serikali, wewe unaponiuliza habari za Serikali, nauwasha. Lakini naona mara unauliza habari za familia yangu, ndiyo maana nauzima wa Serikali na kuuwasha mshumaa wangu mwingine nilioununua kwa pesa za mfukoni mwangu. Nachelea nisije fanya dhuluma kwa mali ya nchi."
Ndugu zangu,
Bila shaka, hicho ni kisa chenye kutupa mafundisho muhimu
juu ya dhana nzima ya maadili katika utumishi wa umma.

maggid
 
Dunia ya leo ni tofauti, kwa mtumishi wa umma kufanya hivyo utashindwa hata kusomesha watoto
 
Dunia ya leo ni tofauti, kwa mtumishi wa umma kufanya hivyo utashindwa hata kusomesha watoto
kumbe ndio maana 1.5 trillion haijulikani ilipo.
Mithali : Mlango 28

16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.
 
Back
Top Bottom