Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania....!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania....!"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 18, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  ... Hatuwezi, Hatuwezi!... Mchakamchaka, Chinja, Mchaka mchaka, chinja!  Ndugu zangu,


  Utotoni niliwasikia kaka na dada zangu wakiimba wimbo huu wa mchakamchaka uliojaa hisia za utaifa. Ni kwenye mchakamchaka wa shuleni kila asubuhi.


  Naam, hata wakati huo kulikuwa na utata wa masuala ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi . Zilikuwa ni enzi za Rais Kamuzu Banda.


  Na Watanzania hatukuwa na ukame wa nyimbo za kebehi dhidi ya Banda. Mwingine uliimbwa hivi; " Kipara cha Banda kina ukoko!" Hakyamungu. Hata wakati huo kulikuwa na harufu ya vita baina ya ndugu wawili; WaMalawi na WaTanzania. Maana, ukweli sisi ni ndugu wa damu.


  Kuna hata simulizi za kweli za Watanzania upande wa pili wa Ziwa Nyasa waliokesha kusheherekea Uhuru wa Malawi. Hivyo basi, tunaweza kabisa kidiplomasia kutamka, kuwa "Jambo la Malawi ni letu!" Ndio, shida yao ni yetu, furaha yao ni yetu.


  Na tushukuru kuwa JK wetu ni mwanadiplomasia. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa JK anaweza kutuingiza katika ' Vita vya kiwendawazimu' dhidi ya jirani na ndugu zetu wa Malawi.


  Na picha hiyo hapo juu inaongea; JK na JB ( Joyce Banda), wanazungumza kwa furaha kama ndugu. Wawili hao hawatoi nafasi kwa wachonganishi wale wa enzi za ugomvi wa utotoni. Maana, utotoni ilikuwa hivi, kaka zetu walipotaka kufurahia wadogo zao tukipigana makonde, walisubiri pale mmoja anapomkasirikia mwenzake. Haraka atatokea kaka na mchanga mkononi. Atatamka kwa mmoja kati ya wawili walio mbele yake;


  " Haya, puta mchanga wangu kama kweli wewe ni mwanamme!" Nani asiyetaka kuwa mwananme? Atauputa mchanga. Kisha kaka anamgeukia mwingine; " Haya sasa, nilipie ng'ombe wangu!".


  Kulipa ng'ombe ilikuwa na maana ya kuanza kurusha konde. Na hapo ugomvi ulianza rasmi!


  Na kuna miongoni mwetu wenye kutamani vita. Anayetamani vita ni mtu mjinga. Mwalimu alipata kutamka; " Vita si lelemama". Na katika dunia hii inasemwa; Chagua vita vyako. Vita vingine havina lazima ya kupiganwa.


  Na tofauti zetu na Malawi zinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kama anavyoonekana JK pichani akiongea na dada yake; JB- Joyce Banda.


  Na wala hatuwahitaji tena akina Moses Nnauye kututungia nyimbo za Mchakamchaka. Eti twende tukiimba; " Banda ( Joyce) Wa Malawi, Katuvalia Kitenge Cha Ngozi Ya Mamba, Kututishia Watanzania, Hatuwezi, Hatuwezi!".


  Naama. Wakati umebadilika.


  Maggid Mjengwa,
  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha nyimbo za zamani Majjid!
  Hii ni pamoja na:
  Kaburu matata ia ...
  Ooh sasi jabelwa mitwe, sasi aah, ooh sasi...

  Nduli Idd Amin Dadaa n.k.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mama ana mume kweli?mbona kaa kibabe sana
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nakumbuka Uganda walishakuwa na makamu wa rais mwanamke ilibidi arolewe maana mumewe alikuwa anampiga vifuti daily!!! ikaonekana jamaa anaidhalilisha taasisi ya umakamu wa rais..hahaaa
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  ila vita ikipiganwa vyema huwa ni epusho kubwa sana la vita za kizembe ambazo pia huwa na muaji mabaya zaidi.Vita ikipigwa kwa ufanisi na nguvu zote hisha haraka sana.

  Nakumbuka nami shule enzi hizo pia nilikuwa nikimaliza ngumi bila kupigana sana,na pengine ningepigana ningeweza uwawa na heshima kubaki.Som eof those guys hata tkiwa nao huwa hamaniamini sana kuwa nimezeeka.Kwani siku zote walikuwa wakipata result za kuwachanganya.Huwa mimi by nature sipendi kupigana, wala distructions,but huwezi amini kuna watu huwa hawapati amani na furaha bila tishia watu wanaowazunguka, na hawa watu huwa wakipata mafunzo kidogo ya kupigana au hata wakiingia gymn siku ya kwanza basi tayari hutembea vifua mbele.Huwa hawa mimi nilikuwamajiepusha nao sana ila baadaye nikaja gundua kuwa kujiepusha wao hutafsiri kuwa nimekuwa mwoga na hivyo wajisikiavyo huwa wanafanya wapendacho, na ukiuliza au hata kujitoa huwa wanaona kuwa hiyo ni revolt na hivyo kutaka toa adhabu ya mfano ili watumwa wengine wasiige.Hii ni Human nature.Ndugu yangu nisikuambie, nilikuwa nafanya mazoezi ya kupeleka mikono mizito kuliko miwli wangu , na hata kama natumia mawe nilikuwa nayapeleka kama mvua mpaka adui atokomee,kama akibaki mimi nikuwa natandik tandika bila break. Mjengwa huwezi amini sikubahatika mpiga mtu ngumi zaidi ya tatu, bila kunikimbia, piga magoti au hata kupoteza fahamu.Wote kati yao sikuwahi pata nao shida, na mara zote jukumu likawa kwangu kutoingia katika taabu nao,kwani wao hawakuwa tena na imani nami kwa uhai wao.Wadogo zangu wote wenye miili mikubwa na walioamini kuwa kipindi kimefika cha kuonyesha ubavu katik familia hadi kwa wazee, huwa wanalijua hilo.Huwa dogo huwa hata kama naumwa huwa wananiangalia kwa jicho kuwa huyu jamaa hakuna mwamini akiwa hai.Same goes kwa level ya nchi,kabila, na tamaduni nyingi.Na kichapo huwa hakipotei mbele ya uzao wao,kwa hiyo ni sisi tuu baadaye tusiwe na sifa za kuchokoza wenzetu.Tuna washezi wengi wametuzunguka wantamani sana wapate njia ya kwenda baharini.

  Malawi hapa bado hawataishia hapo, sana sana usalama utategemea busara ya kiongozi aliyepo na uweo wao kiuchumi na kivita, pengine na ustawi wetu.Tukiingia katika vita vya ndani kama Rwanda kuna uwezekano wakajikatia kipande.Sadam alsihajenga mzinga Kuwait na Ghaddafi kwa kuwa na ushawishi kwa maitaifa ya africa na kufadhili vikundi vya kigaidi na huku akijifich achini ya wapalestina huku akiona hakuna alichofanyiwa kimabavu.Walifika mahali wakadhani na hata kuaminisha watu katika dunia kuwa jamaa wana ubavu sana hata mbee ya jumuia za kimataifa.Jamaa walisahahu kuwa kama mataifa ya magharibu yangekuwa na uhuru na nia ya kwenda kuua kama kufanya uvuvi na dunia ikaona poa.Kuna watu wangekuwa wamefutwa kwa silaha kali na mataifa korofi kama jamii ya kimataifa haikuwa na mitizamo ya kuchukia maangamizi.

  Malawi anahitaji kuchapwa,kuchapwa sana na mwishowe tuweke mamluki wetu kuongoza nchi , nchi yao itatulia sana na kila wakumbukapo hiyo halia huamua kwenda lima au kufanya kazi.Hakuna amani kama adui ana doubt na uwezo wako, halafu akawa ameamua amani na furaha yake ni kukunyanyasa.Hawa jamaa na uamsikini wao wa roho na mwili wanapewa moyo na watenda matukio mabaya ndnai ya nchi yao,kiasi cha kudhani kuwa wanaweza vuka mipaka.Sasa wameanza na TZ kwa vile nadhani hawajaona askari wetu wakiruka mipaka yao na kufanya uahalifu.Ila hawa watu ni waoga kweli kweli, kuwatisha hakutoshi kwani watapata tena ujasiri,ila kuwatega na kuwachapa kutamaliza kabisa mashaka na kubeep kutaisha.
   
Loading...