Neno la faraja kwa wanajamiiforums.

.... Cha msingi tambua kuwa upendo na heshima kwa wakubwa na wadogo ndio tunu ya utu. Usimdharau mtu maana Mungu hana dharau juu yako. Sali sana kama vile utaondoka duniani dakika sifuri ijayo.

Mwenyezi Mungu atujalie tuwe watu wema tusio chukiana kwa rangi zetu au tofauti za imani zetu na itikadi zetu.

Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke na mbarikiwe hadi mpigwe na butwaa.
Mohamedi Mtoi, Hii ni faraja ! ... Umegusa NENO KUBWA!!!

Utu ni ufahamu ndani ya mwanadamu unaomjengea uadilifu na maadili ya kibinadamu kupitia Fikra, Kauli na Matendo yake. Utu ni ufahamu wa kiuungu ndani ya Mtu, unao mtofautisha na viumbe wengine wote ulimwenguni.

Utu hauna dini, hauna itikadi, hauna ukabila, hauna ukanda, hauna jinsia, hauna hisia hasi za chuki, hasira, kinyongo, woga au kulipiza kisasi, Utu hauasisiwi na Rangi za ngozi zetu ... Utu ni Heshima, Tumaini, Upendo ... UTU ni Uungu ndani ya MTU!

Utu ni umoja uanaowaunganisha Watanzania wote. Utu ni Utanzania!!

Namuamini Mungu kwa Moyo wangu wote na DINI yangu ni UTU!!

Mungu ibariki Tanzania na Watu Wake Wote!!

Aaaamen!!
 
Japo Neno la faraja ni la juzi lakini Mungu hushusha baraka zake bila ya kuchelewa na si kwa wakati tuutakao wanadamu.
Neno lako mkuu Mohamedi Mtoi ni kweli iliyo kwa Mungu daima. Asante kwa kunitia faraja, ubarikiwe. Amina
 
Ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo na hatua unayofikia. Pia kukumbuka kwamba kila mwanadamu kajaliwa karama yake.
Ukifanya na kufahamu hilo, hakika mawazo yatapungua.

Siyo vibaya kuwa na wivu wa kimaendeleo, lakini wivu huo husikufanye ujione mnyonge na husiye bahati. La hasha. Bali ukufanye ufikie malengo yako kwa karama uliyojaliwa na Mungu.

Nimependa hapo nilipo-bold mdau maana tukijirekebisha hapo tutafika kwani fursa zipo (tusibaki tunajilaumu tu kwani tutaishia kuwaona waliotupita ni wezi kumbe wengi wamepitia katika njia halali)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom