Neno hili kikongo lina maana gani?

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Ndugu Wanajamvi,
Naomba nieleweshwe maana ya neno Kitoko kwa lugha ya kikongo. Kuna mtangaji wa redio Uhuru fm pia anajiita Mwasikitoko.
Kwa kilugha chetu huku Umakondeni ni tusi kubwa sana huwezi kutamka hilo neno mbele ya ndugu na jamaa. Nakosa uhuru kabisa pale Mtangazaji wa uhuru fm anapolitaja jina lake hasa nikiwa na watu niniaowaheshimu kwakuwa neno hilo ni tusi kubwa.
Naomba kuelimishwa maana ya neno kitoko kwa kikongo.
 
mpaka unasikiziza matanangazo hayo inamaana kuna baadhi ya maneno unayaelewa, unganisha dot bro ukiweza vinginevyo subiri wataalam waje
 
Ndugu Wanajamvi,
Naomba nieleweshwe maana ya neno Kitoko kwa lugha ya kikongo. Kuna mtangaji wa redio Uhuru fm pia anajiita Mwasikitoko.
Kwa kilugha chetu huku Umakondeni ni tusi kubwa sana huwezi kutamka hilo neno mbele ya ndugu na jamaa. Nakosa uhuru kabisa pale Mtangazaji wa uhuru fm anapolitaja jina lake hasa nikiwa na watu niniaowaheshimu kwakuwa neno hilo ni tusi kubwa.
Naomba kuelimishwa maana ya neno kitoko kwa kikongo.

Kitoko kwa tafsiri ya moja kwa moja ina maana "uzuri/nzuri" japo laweza kubadilika kidogo kulingana na muktadha
Mwasi maana yake "mwanamke/mke/msichana"

Mwasi kitoko = Msichana mzuri/msichana mrembo/mwanamke mzuri/mwanamke mrembo

Mifano:
Kitoko ya mwasi ya/na ngai eleki wana ya mwasi ya/na ye -Uzuri wa mke/msichana wangu unazidi wa mke/msichana wake
Likolo ezali kitoko - anga/hali ya hewa ni nzuri
 
Back
Top Bottom