Nenda, nakutakia kila kheri

Nenda, nakutakia kila kheri

Noel Ngiama Makanda

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2018
Posts
1,782
Reaction score
3,111
Kuna wimbo mmoja wa Diamond Sound unaitwa nadhani Valentine. Nimeutafuta sana sijaupata wadau, mwenye link please anaweza kushare hapa. Nakumbuka baadhi ya lyrics kama:” Jumamosii eeeeeeh, Jumamosii ya leo, marafiki wawili wawili, mimi mkono kwenye shavu, naumiaaaa, naumiiaaaaa” then kuna kipande wanaimba nendaaa nendaaa, roho yangu ipatwe na amani, huko unakokwendaa nakutakia kila la kheri, utakayekutana nayeee, umpe mapenzi ya kweli na sio ya faidaa, ili usije muumiza kama vile umeniumizaaa”
Ninaweza kusema huu ni mmoja kati ya nyimbo bora kabisa kwenye list yangu. Kipindi hicho nina redio yangu ya betri mbili, kila nikipata muda nasikiliza zangu sebene huku nakamua shule taratibu, those good old days.
Kipindi hicho muziki ulipokuwa muziki, ikifika mwezi huu huwa naukumbuka sana huo wimbo.
Noel Ngiama Makanda, kwa sasa niko Alexandria Misri.
 
Bila shaka ushalizwa na mafarao wa Misri.
Pole aisee.
 
Back
Top Bottom