Nenda Makwetta Nenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nenda Makwetta Nenda

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Malila, Aug 15, 2010.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Ni kweli umekaa/umetutumikia muda mrefu,sasa ni wakati wako wa kupumzika,wala usijisikie vibaya kushindwa. Hata kama hakuna tafrija ya kukuaga,mimi nitakuaga kwa kukushukuru kwa machache mazuri uliyofanya.

  Ulijitahidi sana kuhakikisha Njombe inakuwa na shule nyingi ( NDDT),hata kama ulishirikiana na wenzako,vijana wengi tulisoma ktk shule zile. Sijui kama ilikuwa ni juhudi yako au la,nakumbuka ulikuja kufungua RTC kijijini kwetu,porini kwelikweli. Na vituo vya afya vikawa vingi,kilimo kikawa juu,nk.

  Nilikuona 1979 ukienda Makete kuweka jiwe la msingi ili eneo hilo liwe Wilaya pamoja na Ludewa ukiongozana na Sokoine (RIP),ukiwa mbunge wa wilaya yetu. Baadaye Njombe ikawa na wabunge watatu,wewe upo. Na baadae Njombe imekuwa Mkoa, wewe upo ktk usukani,hapana sasa mzee nenda kapumzike.

  Wewe ndiye Mbunge pekee uliyewahi kuongoza wilaya iliyozaa wilaya mbili,bado eneo lako likazaa majimbo mawili mapya,na bado eneo lako ulilowakilisha kwa kipindi chote ukiwa Mbunge likawa mkoa. Wewe ni mzee wetu wa mkoa,nenda kapumzike kwa amani.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jackson Makwetta should have seen the writting on the wall since the 2005 elections; he should have retired honourably instead of waiting to be shoved out of the political stage disgraceffully by an illiterate pretender!! He had an illustrious career which has ended miserably. Pole sana Mtwa wa wabena!!
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Jah people kamwaibisha vibaya mzee wangu huyu,ndio siasa.
   
Loading...