Nenda kabeti

20PROFF

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
8,217
Reaction score
7,263
Dogo, katoka shule kachoooka viatu vimeisha kinoma. Kaenda barazani , kumwambia mzee wake amnunulie viatu vipya.

Dogo; Baba shikamoo,

Mshua; marhaba umerudi eeeh, haya toka nenda ndani.

Dogo; Baba viatu vimeisha ,nimeambiwa nikanunue vingine.

Mshua; ( kaingiza mkono mfukoni katoa jero) chukua hii nenda kabet upate hela ya viatu.
 
Nasikia betting ni shughuli kuu kwa baadhi ya wakazi wa Dar! Kwa hiyo simshangai huyo dingi na mtoto wake.
 
Nasikia betting ni shughuli kuu kwa baadhi ya wakazi wa Dar! Kwa hiyo simshangai huyo dingi na mtoto wake.

Ukiwakuta watu.wanabet unaweza hisi wanajisomea kwa ajili ya pepa au presentation
 
Toka niibiwe sent 5 iliyokuwa na samaki mwenye mdomo mrefu, kwenye kamali ya korokoro...! Niliacha kabisa habari hizo, imefikia kipindi kama vinywaji vinaendesha shindano la bahati nasibu sinywi vinywaji hivyo...!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…