Nelson Mandela, South African Icon of Peaceful Resistance dies at 95

Kuna dogo hapa home ananiuliza"Kwahiyo Uncle Mandela sasa ndo kafa kikwelikweli" nikamjibu ndio kipindi kile walikuwa wanamzushia

R.I.P Madiba

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mpigania uhuru na baba wa taifa mzee Nelson Madiba Mandela amefariki usiku wa kuamkia leo mida ya saa 3 kasoro za usiku.
Mandela na wapigania uhuru wengine wa Afrika Kusini watakumbukwa kwa harakati zao za kupigania uhuru wa Afrika Kusini. Zaidi atakumbukwa kwa tactic yake ya non violence movement aliyojifunza kwa Gadhi wakati huo akiwa gerezani.
 
kifo kingalikuwa kinaruhusu rufaa, nyingi zingeshawekwa mezani. Upumzike kwa amani mzee wetu Madiba.
 
Wanakufa watu wema tu, wabaya wanabaki. Mungu anamakusudi!. R.I.P Madiba, mwambie Nyerere chama chake alichokiacha mtu kama Mwigulu ndio kiongozi mwenye maono!.
 
"Our AFRICA has lost her greatest son" says MpigaKelele.


"Afrika tumempoteza Mwanaafrika mahiri akiwa ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Waafrika kwa dhati. Uwepo wake hapa duniani nina imani umejenga kujiamini kwa waafrika wengine mahiri kuisaidia Afrika wakati wowote, ni jukumu letu waafrika kuhakikisha waafrika wenzetu wenye umahiri kuisaidia Afrika kuwapa nafasi na kuwaunga mkono wakati wote.

Mungu twaomba umlaze mahali pema peponi, Mwanaafrika Nelson Mandela.

Mungu ibariki Afrika.Amen." imesemwa na MpigaKelele
 
Ndiyo njia yetu sote.


RIP Shujaa wa Afrika kwa jinsi ya kibinadamu.

Ila kama hukulikiri Jina lile lipitalo majina yote, sijui uko kwenye hali gani muda huu; maana kuna njia mbili tu baada ya maisha haya ama uwe pamoja na watakatifu katika Mji ule Mtakatifu au Lusifa na malaika zake wakukaribishe kwenye himaya yao yaani kule Jehanam. Naamini ulijiandaa vizuri kiroho.
 
Ulale kwa amani Mzee Nelson Madiba Mandela, familia ilikupenda, South Afrika ikakupenda, Afrika ikakupenda, Dunia ikakupenda. Utakumbukwa daima milele. Amen
 
Back
Top Bottom