Nelson Mandela, South African Icon of Peaceful Resistance dies at 95

Nasikia JK ametangaza siku 3 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti kote nchini Tanzania. Je, wafanyakazi za kuajiliwa hawatoenda kazini?
 
_71575555_71568884.jpg
_71575554_71568476.jpg
 
Mandela's death should be treated not as a loss, but as a hope with his passing someone of his sort is being born somewhere in Africa, someone who will touch this and the coming generation like Mandela had in his and past generation. It is a period of cherishing and thanking the Almighty to have given his nation, Africa and the world a person of his unmeasurable Caliber.

Mandela has lived life to the fullest.

May he Rest in Peace.

*The following is a speech he gave announcing his retirement from the public in June 2004. In a way I feel as if it is still applicable in his death.

'Don't call me, I'll call You'

I am turning 86 in a few weeks time and that is a longer life than most people are granted. I have the added blessing of being in very good health, at least according to my doctors. I am confident that nobody present here today will accuse me of selfishness if I ask to spend time, while I am still in good health, with my family, my friends and also with myself.

One of the things that made me long to be back in prison was that I had so little opportunity for reading, thinking and quiet reflection after my release. I intend, amongst other things, to give myself much more opportunity for such reading and reflection. And of course, there are those memoirs about the presidential years that now really need my urgent attention. When I told one of my advisors a few months ago that I wanted to retire he growled at me: "you are retired." If that is really the case then I should say I now announce that I am retiring from retirement.

I do not intend to hide away totally from the public, but hence forth I want to be in the position of calling you to ask whether I would be welcome, rather than being called upon to do things and participate in events. The appeal therefore is: don’t call me, I’ll call you.
 
Kati ya watu ambao hata kama kimwili hawapo pamoja na sisi lakini wanaendelea kuishi ni Mwalimu na Madiba. Wapo wengine pia lakini hawa ni mifano ya haraka sana!

Hawa waliamini kwenye falsafa ya "Living Today for Tomorrow"! Walipojifikiria wao walifikiria na ustawi wa wakazi wengine wa dunia hii.

Nasikitika kuona kuwa watu wa kariba hili siku hizi hawapo popote na waliopo hawapewi fursa zozote zile!

Tumeendekeza umimi, ubaguzi, kujilimbikizia mali, utajiri wa haraka haraka kwa gharama/mbinu zozote na matendo mengine maovu huku tukiendelea kuzaliana! Laiti tungejua kuwa siku zetu za baadaye zitakuwa za kulia na kusaga meno kutokana na misingi ya kinyang'au tunayoijenga leo!

Mimi ni mwanafunzi wa maisha ya Nyerere na Madiba. Ninapotafakari maisha ya hawa ndugu zetu naona kwamba walikuwa binadamu zaidi ya watu wengi tulionao duniani.
Walikuwa na madhaifu yao lakini hayawezi kamwe kulinganishwa na mazuri waliyoifanyia dunia.

Ingependeza kama kila mtu akutane na moyo wake;kutoka humo aone ni jinsi gani anashiriki kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri/salama ya kuishi leo na kesho! Living Today for Tomorrow!

Ee MUNGU naomba utuinulie akina Nyerere na Madiba wengine...!
 
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema patakatifu.Amin

Dunia sasa yapasa kujifunza mambo mengi mazuri aliyoyaacha
Hayati Mzee Mandela kwa kuyaenzi kwa vitendo,hasa suala la ubaguzi
wa rangi miongoni mwa wanadamu.

Hayati Mzee Neslon Mandela alikuwa ni taswira muhimu ambayo
binadamu wengine waliiona kama ni kikwazo kwao kuendelea
kukandamiza misingi na haki za mtu mweusi.

Hivyo kuondoka kwake mbele za haki isiwe ni mwanzo wa manyanyaso
na ukandamizaji wa haki za wanaSA na waafrika wengine kusini mwa
jangwa la sahara na Afrika mzima.

Ifike mahala wenzetu hawa waache ubaguzi moja kwa moja na sote
tuishi kama ndugu moja katika taswira tofauti,lakini msingi wetu mbele
za Mungu kuwa ni mmoja kwani duniani hapa tunapita tu.
 
Leo nasherehekea maisha ya muungwana mmoja mwaminifu,aliyejitambua yeye ni nani,ameletwa na Mungu kufanya kipi,kwa faida na wokovu wa nani.Ameifanya kazi yake vema mzee Madiba,na ameimaliza kwa mafanikio,ndio maana leo hii sisi tukiwa maili nyingi toka Afrika kusini,tunaomboleza kuondoka kwa mzee huyu shujaa wa kizulu.Namtazama mzee Mandela ndani ya coffin,namuona amelala na ile tabasamu yake,nakumbuka zile purukushani zake zilizomkomboa mtu mweusi wa South Afrika,nakumbuka nyimbo tulizokuwa tukiziimba shuleni kumsifu mzee huyu na mwalimu Nyerere,najiuliza sana,WHAT ABOUT ME?siku nikiondoka jamii yangu na wanadamu walionijua watazungumza nini juu yangu?jiulizeni sana ndugu zangu katika maisha mliyopata hapa duniani ni wanadamu wangapi wana-celebrate uwepo wenu?binafsi nasherehekea maisha ya Mandela.Leo hii namshukuru Mungu kwa kutupatia wazee hawa walioikomboa Afrika.Nakutazama Mandela ukiwa ndani ya coffin,unatabasamu,unaingia kanisani kwa mara ya mwisho hapa duniani,choir nzuri zikiimba na kumshukuru Mungu kwa uwepo wako,sauti kama za malaika mbinguni wakiimba hymns,nami naungana nao kukuimbia hymn hii..."Sun of my soul,thou saviour dear,it is not night,if thou be near,oh may no earth-born cloud arise,to hide thee from thy servant eyes.Come near and bless us when we wake,ere,through the world our way we take,till in the ocean of thy love,we lose ourselves in heaven above."Siyabonga khakulu baba Madiba.
 
Back
Top Bottom