Negative, positive and advanced corruption | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Negative, positive and advanced corruption

Discussion in 'International Forum' started by chash, Jul 5, 2012.

 1. chash

  chash JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nikichunguza haina tofauti za corruption napata kuna corruption inayo leta au kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi, kuna corruption inayo zuia kabisa maendeleo au kurudisha nchi nyuma na kuna corruption ambayo haieleweki kama ni corruption hadi inavyo chunguzwa kwa kina.

  Nchi masikini zina kuwa kwa wingi na corruption inayo zuia maendeleo. Nchi zinazoendelea na za kati zina corruption kwa wingi inayo leta au kuongeza maendeleo ya nchi. Na nchi zilizo endelea ndio zenye state of the art corruption. Kwa hiyo nchi zote duniani zina corruption au rushwa. Hakuna ambayo haina corruption kwa sababu kila mahali watu wanataka wapate pesa na wajiendeleze pamoja na familia zao. Mfanya biashara anapo tafuta tender, contract au deal yeyote ile lazima awe na mbinu fulani atakazozitumia kuweza kufanikisha na hizi mbinu ndizo zinaweza kuleta haina moja au nyingine ya corruption.

  Nianze na positive corruption. Mfano, kuna shule yenye wanafunzi wengi, lakini haina mafunzo ya computer. Sasa huyu corrupter ananunua computer 100 anaenda kwa mwalimu mkuu wa ile shule anampa kitu kidogo na ahadi ya kitu kidogo kila mwezi. Anaruhusiwa kuweka zile computer pale shule na kuleta mwalimu wake. Mwalimu mkuu anatangazia wazazi kwamba sasa kuna somo la computer ila kwa sababu ni ya mtu binafsi kuna kulipia shilingi elfu mbili kwa mwezi. Kwa sababu kila mzazi anataka mtoto wake apate elimu hii, analipa na corrupter anapate hela, corrupted anapata hela, shule inaweza pia ipate kitu kidogo wanafunzi wanapata elimu nzuri zaidi na nchi inapiga hatua. Mfano mwingine. Tajiri ananunua lap top elfu moja lakini hana soko. Anazungumza vizuri na meneja wa benki, ile benki inaanza kutoa mikopo kwa watu wenye ajira kuwawezesha kununua laptop. Tajiri anauza laptop zake haraka, benki inapata faida kubwa na watu weeeengi wanapata laptop.Positive corruption.

  Negative corruption: Kuna mabasi yanayotoka Mwanza kuja dar kila siku. Pia, kuna meli inayo toka Mwanza kuja dar mara mbili kwa wiki. (ni mfano jameni) Sasa hii meli moja inabeba abiria wengi sana kama elfu tano na mizigo tani elfu kumi yote kwa bei nafuu sana. Wafanya biashara wanafurahia hii meli sana na wanapata faida kubwa kwa hiyo uchumi wa nchi unaendelea ku kuwa. Mabasi hayapati abiria kwa hiyo wanatafuta mbinu ili ile meli ipigwe chini Wanafaulu meli inatimuliwa. Mabasi yanapata abiria, wafanya biashara wanafilisika, uchumi wa nchi unarudi nyuma. Mifano mingine pia inaweza kuwa kuzuia daraja muhimu kujengwa ili kivuko au ferry iendelee kufanya kazi, kuzuia mji mpya wa kisasa au tecno city kujengwa, kuzuia road by pass au road expansion kufanyika kwa ajili ya manufaa ya mtu binafsi anaye faidi bila hayo maendeleo kuwepo. Hii ni negative corruption na inarudisha nchi nyuma.

  Advanced corruption:Mtu mmoja anafurahia mtoto wake kapata scholarship ya kwenda majuu kusoma, mtoto analipiwa kila kitu na kupewa allowance ya nguvu, yeye mzazi anaona ni bahati kwa ajili hakuhusishwa kutafuta ile scholarship. Mwaka unao fuata kampuni anayo fanya kazi inam-promote na sasa anasimamia kitengo cha tender. Kampuni fulani ina wasilisha tender application na bahati mbaya ile kampuni ni tawi ya kampuni iliyo patia mtoto scholarship. Ina sifa nyingi za kushinda tender lakini kuna sifa moja haija timiza ila hiyo sifa inaweza kuwa overlooked. Sasa yule mzazi anakuja kujua kuwa hiyo kampuni ina uhusiano na kampuni iliyo patia mwanae scholarship. Heshima inaleta yule bwana kuwapa tender ya mabilioni. Hakuna rushwa inayo onekana kutolewa. Haijulikani kampuni ilivyo cheza hiyo karata lakini ilicheza kweli.

  Sasa unaweza ku grade corruption mbali mbali unazo zijua utujuze kama ni negative, positive au advanced.
   
Loading...