Habari wadau,
Kuna hii habari imekuwepo kwenye gazeti la mwananchi leo ikidai;
HESLB imeanza mazungumzo na taasisi za fedha na mifuko ya pensheni ili kuongeza vyanzo vya mapato na kuweza kufadhili wanafunzi zaidi.
Kwa ninavyoona hii ni neema kwa wanaotarajia kujiunga na vyuo mwaka huu na kwa miaka ijayo.
Tusubiri tuone
=======
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB), Abdul-Razak Badru akizungumza na wafanyakazi wa Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea ofisi za MCL zilizopo Tabata Relini, Dar es Salaam juzi
Dar es Salaam. Katika kuhakikisha inaongeza vyanzo vya mapato, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imeanza mazungumzo na taasisi za fedha na baadhi ya mifuko ya pensheni ili kuongeza idadi ya wanufaika vyuoni.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alipotembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Badru alisema hatua hiyo itasaidia bodi ya mikopo kupunguza utegemezi kutoka kwa Serikali Kuu.
Alisema kwa sasa bodi inategemea fedha kutoka vyanzo viwili tu ikiwamo makato ya mwezi kutoka kwa wanaufaika walioajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi pamoja na Serikali Kuu.
Alisema wastani wa bajeti ya bodi ya mikopo kwa mwezi ni karibu Sh40 bilioni ambapo makusanyo kutoka kwa wadaiwa kwa mwezi ni Sh12.5 bilioni.
“Makusanyo haya pekee hayatoshi hivyo tunalazimika kuendelea kutegemeaa kiwango kikubwa kutoka kwa Serikali Kuu…tunaendelea kubuni vyanzo mbadala vya mapato ili kupunguza utegemezi kutoka serikalini,” alisema.
Akizungumzia ongezeko la makato ya asilimia 15 kutoka asilimia nane za mishahara ya wanufaika, Badru alisema maamuzi ya kuongeza viwango vya makato yalifikiwa ili kupunguza muda wa urejeshwaji na hivyo kuiwezesha bodi kuhudumia watu wengi zaidi.
“Fedha hizi zinapaswa kuzunguka zenyewe pasipo kutegemea bajeti ya Serikali, maamuzi haya ni kwa mujibu wa sheria. Pia, imesaida kuongeza makusanyo ya mwezi kutoka Sh3.5 bilioni hadi Sh12.5 bilioni, mafanikio haya yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa waajiri wanaofika takribani 6,500.”
Mkurugenzi huyo alisema bodi pia, inashughulikia changamoto za kiteknolojia zinazojitokezeza hasa katika urejeshwaji wa makato ya wanufaika.
Alisistiza kuwa mikopo inatolewa kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye fomu ya maelekezo ambayo hutolewa mwezi mmoja kabla ya dirisha la maombi kufunguliwa.
“Huwa tunapima viwango vya waombaji kulingana na vipaumbele vilivyopo,” alisema.
Kuhusu wanufaika wenye vyeti feki, Mkurugenzi huyo alisema hakuna mwanafunzi yoyote aliyepata mkopo kwa kutumia vyeti feki kwa kuwa muombaji hutakiwa kuwasilisha namba ya cheti. Lakini, vyeti feki walivyobaini ni vile vya vifo vya wazazi kuonyesha wao ni yatima na waliobainika waliondolewa.
Badru alisema katika kuhakiki nyaraka za waombaji, bodi inashirikiana na taasisi nyingine za Serikali kama Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Baraza la Mitihani ya Ufundi Stadi (Nacte) kwa vyeti ya taaluma na Wakala wa Udhamini na Ufilisi (Rita) unaaohusika na vyeti vya uzazi na vifo.
“Tukigundua nyaraka yoyote iliyoghushiwa kutoka kwenye fomu za maombi hua tunamuondoa muombaji kwani moja kwa moja anakua amekosa vigezo stahiki,” alisema.
Kwa upande wake, mkuu wa idara ya habari na mawasiliao kwa umma wa bodi ya mikopo, Dk Cosmas Mwaisobwa alisema kuanzia mwaka 1994/95 hadi 2004/5 bodi hiyo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 48,378 huku ikitumia jumla ya Sh51.1 bilioni.
“Baada ya marekebisho ya sheria mwaka 2005/6 hadi 2015/16 bodi imetumia Sh2.5 trilioni ambapo wanufaika wa mikopo ni 345,029” alisema.
Chanzo: Mwananchi