NECTA yatangaza Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka mwaka 2017

“Katika Shule ya Msingi Mwekako iliyopo Chato, wasahishaji walibaini karatasi zilizotumika kujibia maswali ni tofauti na zilizotolewa na NECTA, watahiniwa walivyohojiwa walisema majibu walipewa na mwalimu Mkuu” Dk. Charles Msonde - Mkurugenzi Mtendaji NECTA. #KwanzaHabari
Hizo ni habari za kizandiki wewe watu wa mikoa mingine mna gubu sana
 
Hapo lazima watusue yani mtihani full machagulio ebu fikilia mtoto anapewa swali hili

Raisi wa kwanza wa tanganyika alikua ni nyere_______
A: ra
B: re
C: ri
D: ro
Oya hii serious au?kama ni kweli ,ole wetu kama Taifa maana hao wasomi ni kujilisha upepo
 
Kisichowezekana ni kipi? Mwanafunzi kuotea au?
huwezi kuotea 100percent kama mtunzi ni profession hata principles za probability haziswii.practically nimekuwa nikisaidia family members especially kwenye english na maths nimeona mitihani yao mingi .
 
Madhumuni ya mtihani si kupima kumbukumbu tu na hatutakiwi kusheherekea namba tu kama taifa, nadhani muhimu zaidi ni kupima na kusheherekea kuongezeka kwa ufahamu na uwezo wa kufikiri na kuamua wa wanafunzi. Kuna wakati (nadhani mwaka juzi baadhi ya watoto waliochaguliwa form one walikuwa hawajui kusoma wala kuandika! Mfumo wa majibu ya kuchagua unaweza kumfaulisha hata asiyejua kusoma na kufelisha wenye uwezo zaidi. Hapa sina maana waliofaulu wote wamebahatisha. Ninachosema ni kuwa ubora wa elimu na namna nzuri ya kupima ni muhimu zaidi. Tuachane na multiple choice.
 
Back
Top Bottom