NECTA waige mfano wa NBAA katika suala la Mitihani !!!!!!!!!!!

CPA TUTOR

Member
Joined
May 11, 2013
Posts
8
Reaction score
1
NBAA ni Chombo Cha Serikali na NECTA ni Chombo cha serikali pia!!!
Jambo la Kushangaza ni kwamba wakati NBAA na NECTA vikiwa vyombo vya serikali utaona kuwa NBAA wapo makini sana katika utungaji, usahishaji na upangaji wa maksi na grading.Tangia NBAA ianze miaka ya 1970 Bodi hiyo imesimamia viwango vya juu ambavyo vinaheshimika kimataifa.

Wasimamizi wa mitihani ya NBAA ni walimu wa Shule za Misingi na Sekondari . Na pia wasimamizi wa NECTA ni walimu wa Sekondari sasa kwa nini kuna ubabaishaji NECTA??

Kwa Mfano mzuri mitihani ya NBAA imemalizika tarehe 10/5/2013 na mitihani mingine inafanyika November 2013.
Pia NBAA kuna mabadiliko ya Syllabus na wametoa taarifa kuwa ita anza kutumika mwaka 2014 na hivyo kutoa taarifa kwa wadau kujiandaa vyema.Angalia mpangalio wa watahiniwa wa NBAA nchi nzima walivyo pangwa katika attachment na hakuna kinacho haribika

Kwa upande wa NECTA ambayo mwenyekiti wake ni Prof Mkandala na Kiongozi wake ni Dkt Ndalichako wamefanya : 1.mabadiliko ya Grading bila kujulishwa wadau
2.Wanafanya mabadilko ya Syllabus bila kuhusishwa wadau
3.Vitabu vinabadilishwa bila kuhusishwa wadau
4.Wakati wa Mungai walifuta somo la Kilimo wakani sera ya CCM ni Kilimo kwanza!!!
5.Wamefuta matokeo ya mwaka 2012 bila kueleza sababu halisi za kufeli wanafanzi!!

Suali :
1.Je ,sababu iliyotolewa na Lukuvi ndio chanzo cha kufeli wanafunzi???
2.Je,Prof Mkandala wa UDSM hakuhua tatizo hilo??
[h=2]Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4 [/h]
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya
Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha
Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka
iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka
aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba
hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji
wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973
wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika
mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba

KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA UFUNDI
10/05/2013

Attachments

Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4

[h=2]Serikali ilidanganya kuhusu matokeo ya kidato cha nne?[/h]
Binafsi nimemsikia Tundu Lissu akiongelea jambo hilo kupitia taarifa ya habari ITV ya saa 2 usiku huu.

Kwa ufafanuzi zaidi,alichosema Tundu Lissu katika mkutano huo wa hadhara, ni kuwa, NECTA walipewa barua kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwaagiza watumie utaratibu wa 30% ya alama za mwanafunzi kutoka kwenye continuos assesment na asilimia iliyobaki yaani 70% ya alama itokane na mtihani wa mwisho wa Taifa.

Pia,Mh.Tundu Lissu, amedai kuwa wanao ushahidi wa hiyo barua kutoka Wizara ya Elimu kwenda NECTA.​
 
hao NBAA unaowasifia ndio wanatuletea wahasibu wa hovyo kwenye halmashauri zetu.maziga nyanza!!
 
kumbe ilikuwa ni kutoa tangazo la MSASIRA...? Ila ujue necta inawatahiniwa wengi zaidi kuliko nbaa...
 
Hata NBAA wababaishaji tu...hawana lolote!!! inabidi mfumo mzima wa elimu kwa Tanzania uangaliwe upya........
 
hao NBAA unaowasifia ndio wanatuletea wahasibu wa hovyo kwenye halmashauri zetu.maziga nyanza!!
Ufisadi ni tabia wapo Wahasibu wengine wamesoma UK ACCA ni wezi!!!
UDSM ni chuo lakini Maprofesa wengi hapo wamejifungamanisha na Wizi wa CCM.
Redent iliasisiwa UDSM na kupigia debe CCM lakini imekufa kwa unafiki huohuo!!!

Prof Safari Kitila Mukombo ,Prof Mwesiga Baregu wametoka UDSM hivyo huwezi kuwaunganisha na ufisadi wa Redent
 
Back
Top Bottom