NECTA/TAMISEMI/Wizara ya Elimu na hili nalo mlitazame

NECTA/TAMISEMI/Wizara ya Elimu na hili nalo mlitazame

Mara baada ya Matokeo ya Jana ya Darasa la Saba, niliamua kufanya utafiti wangu Mdogo.

Kwanza, nilichagua Mikoa ya Tanzania 20 randomly.

Pili, Kila Mkoa nikachagua wilaya 2 .
Tatu, Kila Wilaya nikachagua Shule 5 za Serikali ( Kidumu mfagio ,wanyonge ) ... Na shule 1 ya Magari ya njano( Wakishuaaa/Walamba Asali ).

Nikagundua ya kwamba .

Kwenye hizo Shule 5 za Serikali, HAMNA USHINDI WA DARAJA ""A"". Wachache wameanzia Daraja B, wengi wameangukia Daraja C.

Kwa upande wa "Magari ya Njano, Wakishuaaa .. UNAKUTA SHULE INA WATOTO 50, WOTE WANA DARAJA "A"

yaan mpaka hiyo HESABU /HISABATI ambayo wengine wakati tunasoma , ukipata "A" , Kuanzia Shule, Diwani ,Wazazi, ni wanakufanyia Sherehe ... Ila watoto wa MAGARI YA NJANO, kwao Hesabu ni Maji ya kunywa, Usishangae Darasa Zima Kupata A.

Ni kweli Hawa wote ni watoto wetu, na lengo ni Moja tu, kuwapa ELIMU !!.

Ila Sasa Ndugu zangu, Ni kweli hizi shule binafsi, Zina fundisha vizuri Kwa kiwango hicho kwamba Darasa Zima lipate A, ?? A mpaka ya Hisabati ?.

Hivi ni kweli, watoto wa Magari ya njano, wako na intelligence hiyo hata Darasa Zima wapate A ?.

Hivi kweli, Watoto wetu wa Kidumu Mfagio , ni wajinga sana mpaka waishie kupata B, C, D ?.

Au ndo kwamba, shule za Kidumu mfagio, Walimu hawajali na hawafundishi au malupulupu au nini??.

OMBI LANGU KWENU WAHUSIKA.

1-TAMISEMI, Wakati wa upangaji wa majina ya kwenda Sekondari, niwaombe sana, WALE WANAFUNZI WA KIDUMU NA UFAGIO, WALOBATIKA KUPATA UFAULU WA "B" , Tena akiwa amefaulu SOMO LA HESABU Kwa UFAULU WA " B ", wafikirieni Mara tatutatu kwenye Shule za Vipaji .

2-Wizara ya Elimu, hizi shule binafsi zinafanya Biashara, Hawa watoto sanasana wanachojua ni lugha tu ya kingereza, ila uwezo wao ni Mdogo , wanapata ufaulu mkubwa sababu ya WIZI WA MITIHANI ....NA KWA MAWAZO YANGU , WIZI WA MITIHANI UNAFANYIKA NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI , YAAN MSIMAMIZI/WASIMAMIZI WANAPIGWA MLUNGULA, KISHA MWALIMU AU MSAMIZI HUYOHUYO ATAANZA KUSOVU MTIHANI, KISHA MAJIBU WATAPEWA WANAFUNZI HAWA .

Sio haki, na haiwezekan Mwanafunzi alofaulu Kwa wizi WA MITIHANI wa SHULE BINAFSI, Apelekwe shule za Kipaji maalaumu ili hali amechukua Nafasi ya Mwanafunzi wa serikali alofaulu Kwa Daraja B lakini Kwa nguvu zake na Akili yake yaaan 'Kuvuna sawa na ulichopanda'.
Non-sense.
 
Ukiona shule wanafunzi wote wamepata 'A' maarifa ya jamii....lazima kuna wizi. Fuatilieni shule moja iko TARIME wanafunzi wote(50) wana A masomo yote na wastani wa 296/300.
Hapo lazima kuna kitu....so mleta mada yuko sahihi....hatuwezi kurisk future ya watoto wetu kisa hela za rushwa na ufisadi.
Katika dunia ya Leo elimu serious ni muhimu kuliko kuhodhi mapesa mengi.
 
Mkuu necta imezifungia shule 24 kwa udanganyifu wa mitihani

Moja ya shule hyo n st anne Marie ya ubungo ambayo mwaka juz ilishika nafas za juu kat ya shule kum bora kitaifa na ikatoa wanafunz 4 katka kum bora kitaifa

Shule nyingne iliyofungiwa n kidama ya chato geita mwaka Jana iliingia kumi bora kitaifa

Huon Kama kuna ukweli hapo mkuu?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hebu mkuu tusiaidie tupate list ya shule zilizofungiwa iwe Kama alert kwa sisi wazazi
 
Kama wamefikia Hadi kuifutia Hii,
This is very serious, kongole necta[emoji120]
Mwaka huu vilio tu kila kona ya nchi.
Wazazi na watoto ndio wahanga sababu hawakuhusishwa lakini wanahadhibiwa wao.
Ilitakiwa wapewe mtihani mwingine haraka maisha yaendelee, wenye kupata nafasi za shule za sekondari za umma wapate hiyo fursa.
 
Sio kweli kuna cousin wangu kapiga A za kutosha kasoro ana B moja tu ya Hesabu na anasoma Shule za Serikali za kawaida tu hizo unazosema mfagio na kidumu ila usisahau siku hizi hawabebi kidumu na mfagio wanaenda mikono mitupu na mabeg tu mgongoni, hizo zama za kidumu na mfagio zilishapitaga, angalia Shule inaitwa Mlimani Primary School
Kanuni tuiangalie mlimani.. nenda kaangalie mbagala primary SCHOOL halafu urudi.. utaedit comment yako
 
Kanuni tuiangalie mlimani.. nenda kaangalie mbagala primary SCHOOL halafu urudi.. utaedit comment yako
Nmesema kwa kupinga kwamba shule za Serikali hakuna waliopata  A elewa comment yangu na kile nilichomweleza mleta mada, cousin wanga kachapa A kote kasoro hesabu ana B kwa hio si kweli kwamba shule za Serikali hakuna waliopata alama A
 
Mkuu hizo kidumu na mfagio ndo mabingwa wa kuiba na wanaiba kweli kweli hasa shule za vijijini watoto hawajui kusoma ila wanafaulu.Na wanaohonga ni walimu wakuu ili wabaki kwenye nafasi zao
 
Kwa mtazamo wangu tofauti ya ufaulu wa private na serikali ni hii.
Shule za Serikali ni kapu la pamoja. Wenye akili na wasio na akili wote wanafanya mitihani.
Mbaya zaidi watoto wanaoonekana wako vizuri kichwa wanakwenda private. Hivyo shule za Serikali zinabaki na vilaza tupu. Hapo Mwl. hata afundishe vipi utamlaumu bure tu.
Wakati huo huo shule za private zinachukua vipanga tupu. Ukimchukua mtoto wa mwisho private ukampeleka shule za Serikali atakamata namba 1 na kuwaacha wenzake mbali sana.
2. Siasa, shule za Serikali zinatawaliwa sana na siasa. Kiasi kwamba mpaka asiyejua kusoma na yeye anafika DRS la 7. Wakati private hakuna longolongo
 
Nmesema kwa kupinga kwamba shule za Serikali hakuna waliopata  A elewa comment yangu na kile nilichomweleza mleta mada, cousin wanga kachapa A kote kasoro hesabu ana B kwa hio si kweli kwamba shule za Serikali hakuna waliopata alama A
Umeelewa lkn utafiti wangu niloufanya??.
 
Nimepitia shule Tano Tano upande wa serikali, Na Shule 1 ya private katika Kila Wilaya mbili za Kila Mkoa Kwa Mikoa 20.
Vizuri sana mkuu umepitia kwa kuchagua kwa mtazamo wako sio vibaya, maoni yako na yaheshimiwe
 
Jamani Kama hujawahi kufundisha shule ya private ukiambiwa kuna wizi au kuwasaidia watoto mitihani unaweza bisha, ila tuliofundisha shule hizo tunajua mifumo yote ya wizi na ndio maana wiki moja kabla ya mtihani kuanza vikao haviishi vya kupanga itakuaje, hatukatai kuwa private hawana watoto wazuri darasani ila Kuna mifumo huwa inapangwa ya kusaidia watoto.
 
Shule za jumuiya ufundishaji ni mbovu ,hii nikutokana na wingi wa wanafunzi kwa darasa husika ,unakuta darasa moja lina watoto 300 /400+ mwalimu wa somo ni mmoja unazani nini kitatokea?
 
Mara baada ya Matokeo ya Jana ya Darasa la Saba, niliamua kufanya utafiti wangu Mdogo.

Kwanza, nilichagua Mikoa ya Tanzania 20 randomly.

Pili, Kila Mkoa nikachagua wilaya 2 .
Tatu, Kila Wilaya nikachagua Shule 5 za Serikali ( Kidumu mfagio ,wanyonge ) ... Na shule 1 ya Magari ya njano( Wakishuaaa/Walamba Asali ).

Nikagundua ya kwamba .

Kwenye hizo Shule 5 za Serikali, HAMNA USHINDI WA DARAJA ""A"". Wachache wameanzia Daraja B, wengi wameangukia Daraja C.

Kwa upande wa "Magari ya Njano, Wakishuaaa .. UNAKUTA SHULE INA WATOTO 50, WOTE WANA DARAJA "A"

yaan mpaka hiyo HESABU /HISABATI ambayo wengine wakati tunasoma , ukipata "A" , Kuanzia Shule, Diwani ,Wazazi, ni wanakufanyia Sherehe ... Ila watoto wa MAGARI YA NJANO, kwao Hesabu ni Maji ya kunywa, Usishangae Darasa Zima Kupata A.

Ni kweli Hawa wote ni watoto wetu, na lengo ni Moja tu, kuwapa ELIMU !!.

Ila Sasa Ndugu zangu, Ni kweli hizi shule binafsi, Zina fundisha vizuri Kwa kiwango hicho kwamba Darasa Zima lipate A, ?? A mpaka ya Hisabati ?.

Hivi ni kweli, watoto wa Magari ya njano, wako na intelligence hiyo hata Darasa Zima wapate A ?.

Hivi kweli, Watoto wetu wa Kidumu Mfagio , ni wajinga sana mpaka waishie kupata B, C, D ?.

Au ndo kwamba, shule za Kidumu mfagio, Walimu hawajali na hawafundishi au malupulupu au nini??.

OMBI LANGU KWENU WAHUSIKA.

1-TAMISEMI, Wakati wa upangaji wa majina ya kwenda Sekondari, niwaombe sana, WALE WANAFUNZI WA KIDUMU NA UFAGIO, WALOBATIKA KUPATA UFAULU WA "B" , Tena akiwa amefaulu SOMO LA HESABU Kwa UFAULU WA " B ", wafikirieni Mara tatutatu kwenye Shule za Vipaji .

2-Wizara ya Elimu, hizi shule binafsi zinafanya Biashara, Hawa watoto sanasana wanachojua ni lugha tu ya kingereza, ila uwezo wao ni Mdogo , wanapata ufaulu mkubwa sababu ya WIZI WA MITIHANI ....NA KWA MAWAZO YANGU , WIZI WA MITIHANI UNAFANYIKA NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI , YAAN MSIMAMIZI/WASIMAMIZI WANAPIGWA MLUNGULA, KISHA MWALIMU AU MSAMIZI HUYOHUYO ATAANZA KUSOVU MTIHANI, KISHA MAJIBU WATAPEWA WANAFUNZI HAWA .

Sio haki, na haiwezekan Mwanafunzi alofaulu Kwa wizi WA MITIHANI wa SHULE BINAFSI, Apelekwe shule za Kipaji maalaumu ili hali amechukua Nafasi ya Mwanafunzi wa serikali alofaulu Kwa Daraja B lakini Kwa nguvu zake na Akili yake yaaan 'Kuvuna sawa na ulichopanda'.
Pole Sana Mkuu.
Kwa uchache ni kwamba:
1. Shule binafsi wanachuja mitihani ya kuanza Darasa la Kwanza vibaya mno. Hizo shule unazosema wanapata A ndiyo zile ambazo mtihani wa kuingia Darasa la Kwanza unakuwa na wanafunzi mpaka elfu 4 wanachaguliwa hapo 50 au 100 tu. Wataendelea kuchujwa hivyo mpaka shule binafsi zikijitosheleza waliobaki ndiyo wanaenda hizo za vidumu.
2. Shule binafsi mshahara na motisha kwa waalimu ni mkubwa Sana. Kule hakuna mwalimu anayeuza mihogo au karanga au mradi wa kupika uji na kuuza kikombe 100 au ,50. Wao KAZI Yao ni kufundisha tu. Tena wakifundisha wanafunzi wenye vichwa vyepesi maana vile vizito viko vidumuni.
3. Shule binafsi mtoto akiingia tu mzazi unapewa orodha ya vitabu ununue au ulipie shuleni ili mtoto awe na kitabu chake na hakuna Umoja (sharing). Huko vidumuni habari ya vitabu ni mtihani Sana.
4. Vidumuni Darasa Lina watoto 150-200. Hivi mwalimu wa husabati apambane na hivi vichwa vizito huku ana njaa anawaza biashara mdogomdogo na kuku wake wa nyama au mayai kawaacha Wana typhoid au cocidiosis halafu utegemee mtoto aelewe?
5. Miundombinu mibovu shule za vidumu ndiyo hatari kabisa. Yaani vile vyoo, madarasa n.k adha yake tu mtoto ataelewaje? Mvua zinanyesha zinapitia dirishani, vumbi Lao, dawati mtihani (hapa kumbuka wapo bado wanaokaa chini baada ya miaka 60 ya Uhuru). Sasa huyu kisaikolojia Kwanza ameshaathiriwa na miundombinu halafu unataka A ya hisabati na Kiingereza labda ya Uraia.
6. Shule binafsi kuna chakula cha saa 4 na mchana tena kizuri!!!! Hivyo wanasoma mpaka saa 10 jioni na madarasa ya mtihani (4 na 7) kuna remedial mpaka saa 12 jioni na Jumamosi pia. Hao wa vidumu wanatoka shuleni saa 8 au 9 jioni kama sikosei. Kisa hakuna chakula. Mtoto ametoka kwao saa 11 alfajiri wengine bila hata kufungua kinywa!! Wakifika shuleni wafanye usafi, waingie darasani mpaka saa 4 akaunge foleni ya kipande cha mhogo. Hivi huyu kwa njaa hiyo atafauluje? Ubongo unajengwa na chakula tunachokula. Yaani mtoto hata ubongoni oxygen ni ndogo maana njaa ni Kali. Huyu ataelewa Sawa na wa basi la njano kweli?
7. Usafiri asubuhi na jioni ni mtihani kwa watoto wavidumu. Yaani watoto wanateseka mno. Kipindi cha mvua ndiyo wako kama kumbukumbi. Apambane afike shuleni anatetemeka na vibration kama kanaswa na umeme. Huyo hesabu zitapita wapi?

Mkuu nikuambie kuwa ili shule za vidumu zifaulu unavyotaka wewe KAZI kubwa inatakiwa. Na kwa sasa mitihani usimamizi ni mzito mno. Kwanza wa basi za njano bila hata usimamizi watafaulu tu maana wakitoka kwenye mtihani wanatuambia kabisa mtihani rahisi kuliko wa shuleni kwao. By the way hata mitihani ya kupimwa kimkoa na kiwilaya (Mock) bado shule binafsi wanaongoza.
Niishie hapa Mkuu wangu maana nikiamua kuchambua Kwa undani nitaandika kitabu.
 
magari ya njano asubui wakiamka wanakutana na chai blueband na mayai ya kukaanga{hawapati kusinzia class},mchana wanakutana na wali nyama au maharage na juice au maji{hawapati stree} muda wa kutoka shule haooo wanakwea magari yao na kurudi home kwa furaha{ no stress}..walimu nao wanapata bonus watoto wakifaulu,achana na mshahra mkubwa wanaopata{hawana haja ya kuuza ubuyu---no stress mazee ni kufundisha kwa bidii ili wapate bonus},wanapewa nyumba au pesa za kupanga,wanatumia computer {hamna kukohoa kwa ajili ya vumbi la makaratasi''''''kuhusu shule za mama samia,watoto wakiamka wanakutana na kiporo au mihogo{inatia usingizi sana na wanasinzia class}..mchana wanachukua kamia mbili walikopewa na kununua ubuyu au viazi vya walimu{stress tupu},muda wa kutoka shule wanafikiria namna watakavodhalilishwa na makondakta wa daladala{maximum stress}..mwalimu ata afaulishe kiasi gani hamna cha bonus wala nini,sanasana walimu wenzake watamchukia na kumwita kiherehere au kazi kunoga na head master anaanza kumwekea bifu kwani anaogopa asije akatwaa kiti chake kwani anaogopa taarifa za mwalimu zikiwafikia wakubwa atapandishwa cheo{full stress}.....na mwalimu hajui alale wapi kwani hamna nyumba wala banda.......sasa ndugu yangu hapo ufaulu utatoka wapi?
Chukua 10 kabisa na shoulder touch. Yaani huko shule binafsi fikiria mwalimu unahidiwa kila A kwenye somo ni 10,000. Wakiwa wanafunzi 100 ni 1m. Kwa nini nisifundishe na kutoa assignment za kutosha? Huko vidumuni hii kitu hakuna. Homework hakuna. Yaani hata ukaguzi wa madaftari kama zamani hakuna. Acha niishie tu hapa.
 
Hii Olympio ya tajiri gani?
Soma matokeo yao kwanini yamefutwa?
Mkuu hii ni shule ya Serikali wanaita ya kishua. English medium. Kuipata lazima uhonge hata kama kichwani ni kweupe mradi pesa. Ndiyo ikifika NECTA wanafanya Yao. Ninachoshangaa shule za serikali zilizoiba mtihani mbona haziko hadharani? Hii Olimpio iko kwenye ile orodha ya wezi 24? Kama haipo basi jua ziko nyingi zimefichwa.
 
Back
Top Bottom