figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,494
- 54,906
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imevitaka vyama vya siasa vilivyoshindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kukubali kushindwa katika uchaguzi huo.
Imesema walikua wakisoma matokeo katika fomu namba 24 A ambayo imesainiwa na mawakala wote na hakuna chama kilicholeta fomu au kumpa fomu wakala wake yenye ushahidi kwamba haya matokeo karekebisheni hapa au Pale mumekosea kusoma.