Uchaguzi 2020 NEC yafanya uamuzi wa rufaa 616 zilizowasilishwa na wagombea Ubunge na Udiwani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
20200918_190551.jpg

20200918_190953.jpg
 
Hongera NEC kwa kazi nzuri
Inawapongeza kwa kutoa ushuzi hadharani?

Kukosa sifa ya kugombea ni mambo yaliyo wazi,wala haihitaji hata wiki moja kujua kwamba, mkwepa kodi,asiye raia,aliyefunga kwa jinai hao tu ndiyo wanakosa sifa ya kugombea.

Kukosea kujaza fomu bado hakumnyimi mtu haki yake ya msingi ya kugombea uongozi
 
Kazi ya kubinya haki na kuipendelea CCM? Hata waliorejeshwa hawapewi barua za kuwaruhusu kufanya kampeni. Haki iko wapi? Karibu mwezi umepita tangu kampeni zianze, wao hawajaanza kampeni. Mnajifanya kuwa dhuluma hii hamuioni!
Sio kwamba hawana pesa mkuu!!
 
Ambacho sielewi kivipi mtu amegombea ubunge toka 2010 siku zote hizo fomu zipo sawa alafu 2020 ndio anakosea kujaza?

Well kakosea, huwa wanahakiki fomu je kwanini tume isikuonyeshe kosa ili uka edit au ulete kiambatanisho ila wanasubiri ukisharudisha ndio aitolee kasoro kwa kivuli cha pingamizi?

Demokrasia ni haki ya wananchi wote sio habari za kupita bila kupingwa. Walau kungekuwepo kura ya hapana na ndio sio kupitishwa tu ndio nini hiko? Tuna safari ndefu sana kufikia uhuru wa kweli
 
Back
Top Bottom