NEC waficha taarifa za ‘voting’ na ‘counting’ kwenye mtandao wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC waficha taarifa za ‘voting’ na ‘counting’ kwenye mtandao wao

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Sep 30, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Tume ya uchaguzi imeondoa taarifa kuhusu namna ya kupiga kura na kuhesabu kura kwenye mtandao wao www.nec.go.tz .

  Hii ni makusudi kuwanyima wanachi taarifa hizo kwani taarifa nyingine zipo. Taarifa hizi zitakuwa zimechakachuliwa kwenye ‘mwongozo wa kupiga kura' mfano, baada ya kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kukaa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura lakini kwenye mwongozo uliosambazwa NEC inawataka wapiga kura waende nyumbani baada ya kupiga kura.

  Hivi ni makusudi au ni kosa la kiufundi?
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari sana wanataka kuchakachua matokeo nadhani vyama husika wataikemea TUME haraka iwezekanavyo
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu vyama vya upinzani viibane NEC irudishe haki ya wapigakura kusimamia haki mita 200 kutoka kwenye kituo ili kuzuia mashushu ambao ndiyo wachakachuaji wakuu kuvuruga haki isitendeke.

  Uchaguzi si huru wala wa haki kama hatupewi nafasi ya kujithibitishia wenyewe kama waliopo ndani ya chumba cha kuhesabia kura wanakubalika kisheria. Mashushushu siyo sehemu ya NEC ila mazingira yanajengwa ya kuiba kura.
   
 4. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo pa kupigia kelele, na tusipowahi kuandika na kupiga ukunga basi watatukamata wakati tunalinda kura tukiwa mita 200. Mimi lazima nikalinde kura nitakayoipiga na mke wangu na wafanyakazi saba nyumbani kwangu.
   
Loading...