NEC Kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC Kwanini?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Ilulu, Oct 5, 2010.

 1. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
   
 2. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wanasema ati walitoa muda mrefu kubadili kitu cha kupigia kura?

  Kama kweli NEC walitaka kuwepo na free and fair election wasingelikuwa kimya mpaka wa leo wangelikuwa wameisha jibu hiyo hoja muda mrefu sana na walikuwa wakitizama upepo wa upinzani au uelewa wa watanzania esp wanafunzi wa vyou mbali mbali ndani ya nchi.

  Hapa ndipo narudi kuliuriza JWTZ wao walisikia kuwa kunatetesi za damu kumwagika na hawakuangali courses ya tetesi hizo kuleta umwagikaji wa damu???
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wanafunzi waitisha serikali
  Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 4th October 2010 @ 07:27

  WANAFUNZI wa elimu ya juu ambao ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameitaka serikali kufungua vyuo hivyo kabla ya siku ya kupiga kura la sivyo watahamasisha wananchi kupiga kura ya mabadiliko.

  Wakati wanafunzi hao wakitoa kauli hiyo, chama hicho pia kimesema kitawatumia wanafunzi hao kulinda kura za wagombea wake.

  Mwenyekiti wa Kamati ya wahitimu na wanafunzi wa elimu ya juu ya Chadema, Richard Manyanga alisema hayo jana Dar es Salaam katika kongamano lililohusisha wanafunzi hao.

  Manyanga alisema kauli hiyo inatokana na hofu yao kwamba wanafunzi wa elimu ya juu takriban 60,000 watakosa haki ya kupiga kura ikiwa vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu.

  “Wanafunzi wengi walijiandikisha kupiga kura ndani ya vyuo vyao wakati wa uboreshaji wa daftari la kupiga kura… na fedha nyingi ilitumika kwa ajili ya kazi hiyo, sasa vyuo vikifunguliwa baada ya uchaguzi, haki ya wanafunzi kupiga kura haitoonekana, tunaiomba serikali isikie mwito wa kufungua vyuo kabla ya uchaguzi,” alisema Manyanga.

  Alisema, anaamini kuwa vyuo havijakosa fedha za uendeshaji hadi wasogeze muda wa kufungua mpaka baada ya uchaguzi na kuwataka wanafunzi wa vyuo hivyo popote walipo kutafuta kura zaidi ya moja na iwe kura ya mabadiliko.

  Manyanga alisema, katika kura hiyo ya mabadiliko, kila mwanafunzi anatakiwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi na kuwahamasisha kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa na vya upinzani ni kwa ajili yao ili wapige kura katika vyama vinavyolenga kuwakomboa wao.

  Mjumbe wa kamati hiyo, Joshua Massaba aliwataka wasomi wakumbuke wajibu wao wa kutengeneza viongozi wazuri kwa manufaa ya taifa na kuongeza kwamba wana imani na mgombea ubunge wa Chadema katika Jimbo la Ubungo, John Mnyika na wako tayari kwa hali na mali kuhakikisha anapata ushindi.

  Akizungumza katika kongamano hilo, pamoja na mambo mengine Mnyika alisema baada ya kufanya makosa mawili ya kisiasa mwaka 2005, wameanza kuandaa mawakala wakati wakiomba kura.

  Alisema hadi sasa, vijana wa vyuo vikuu wameunda mawakala wa ulinzi kwa wa kura siku ya kupiga kura na kwamba katika jimbo hilo dalili zote zinaonesha wananchi wako tayari kwa mabadiliko.

  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), John Kiravu aliliambia gazeti hili kuwa, kuanzia Julai mosi hadi Julai 10, 2010 tume hiyo ilitoa muda kwa wale waliotaka kuhamisha taarifa zao katika daftari la wapiga kura, wafanye hivyo ili wapige kura katika eneo walilopo.

  “Suala la wanafunzi wa vyuo vikuu mimi silijui, Nec inahusika na wapiga kura kwa ujumla, hivyo kama watapiga kura ama la sijui,” alisema Kiravu.<!-- google_ad_section_end -->

  Source: Ujengelele wa Jf (naye emetoa wapi??)
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Kama kweli kipindi hicho wataka kuniambia J.Kiravu hukuo ona alama za nyakati na kujari kusisitizia hilo kwa wanavyuo wote nchi nzima
   
Loading...