Cardinal06
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 963
- 327
Tume ya Uchaguzi (Nec) imetangaza kuanzia kesho, Jumamosi, wagombea wa nafasi ya urais wataanza kuchukua fomu za kuwania kiti hicho katika zoezi litakalodumu hadi Agosti 21, mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba ya Nec, vyama vitatu vya United Peoples Democratic Party (UPDP), Tanzania Labour Party (TLP) na Democratic Party (DP) vitafungua pazia kesho.
Akitoa taarifa ya kuanza kwa uchukuaji wa fomu hizo leo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema kuwa [/b]UPDP kitachukua fomu hizo saa tatu asububuhi, kikifuatiwa na TLP saa sita mchana na DP kitafika katika ofisi hizo saa nane mchana.
Lubuva alisema kuwa Agosti 4, mwaka huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakwenda kuchukua fomu hizo saa sita mchana, saa tatu asubuhi, Agosti 5 itakuwa zamu ya Alliance for Democratic Change (ADC), Tanzania Democratic Alliance (TADEA) huku-Alliance for Change and Transparency (ACT- Wazalendo) wakitarajiwa kuchukua fomu hizo Agosti 17 mwaka huu.
Baadhi ya vyama vya siasa vimesema vinakuja na wanachama wao kuchukua fomu kwa shamrashamra. Shamra shamra ziwepo lakini zisivunje amani ya wananchi, haki hiyo isifanywe kukatiza uhuru wa watu wengine, alisema Lubuva.
Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema kutokana na idadi kubwa ya wanachama wanaoweza kujitokeza wakati wa kuchukua fomu hizo zinazotarajiwa kurejeshwa kabla ya Agosti 21, mwaka huu, wagombea na watu wachache pekee ndio watakao ruhusiwa kuingia ndani kuchukua fomu ili shughuli nyingine katika jengo hilo zisisimame.
Chanzo: Mwananchi