Uchaguzi 2020 NEC: Inawezekana wapiga kura hawajui wana haki ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura endapo itatokea kwa bahati mbaya amekosea

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi wa utaratibu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu na kusema mpiga kura aliyeharibu kwa bahati mbaya karatasi ya kupigia kura akiwa kwenye kituturi kwenye kituo cha kupigia kura, anaweza kuirudisha karatasi hiyo kwa msimamizi wa kituo na kuomba apewe nyingine ili apige kura yake vizuri.

Hayo yalisemwa na Ofisa wa NEC, Flora Mkama jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari watakaoripoti uchaguzi mkuu unaofanyika nchini kote wiki ijayo Oktoba 28.

Akitoa mada kuhusu utaratibu wa kupiga kura, Mkama alisema mpiga kura aliyefika kituo cha kupigia kura na kuhakikiwa kisha kupewa karatasi ya kupigia kura na kuelekea kwenye kituturi cha kupigia na baadae akabaini amekosea kupiga anaruhusiwa kumrudishia msimamizi wa kituo karatasi hiyo kabla ya kuitumbukiza kwenye boksi la kura na kuomba nyingine ili kukamilisha upigaji kura wake.

"Inawezekana wapiga kura hawajui kuwa wana haki ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura endapo itatokea kwa bahati mbaya amekosea au amebadili uamuzi wake wakati akiwa kwenye kituturi atarudisha karatasi hizo kama ni zote au moja kati ya hizo tatu, yaani rais, ubunge au udiwani na kuomba kupewa nyingine ili akachague mgombea amtakaye."

"Inawezekana mtu amekosea katika kuchagua akakuta ameweka alama kwa mgombea ambaye hakumtaka au ameamua kubadilisha uamuzi sasa kuliko aharibu ile karatasi kwa kukatakata anatakiwa airudishe kwa msimamizi alafu aombe nyingine akapige," alisema.

Mkama alisema mpiga kura akiirudisha karatasi hiyo kwa msimamizi wa kituo msimamizi huyo ataichukua na kuandika kwa nyuma ‘Imefutwa’ na kuiweka katika bahasha namba 3A iwapo ni ya Rais au kama ni ya wabunge itawekwa bahasha namba 3B na udiwani bahasha namba 3 C.

Alisema mpiga kura atakayepewa karatasi nyingine ya kupigia kura ni yle tu ambaye alikuwa kwenye kituturi cha kupigia kura na sio aliyekwishapiga kura na kutumbukiza kwenye sanduku la kura.

Akizungumzia wapiga kura wenye sifa, Mkama alisema wanaoruhusiwa kupiga kura kwenye kituo husika ni wale tu waliojiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kwenye kituo hicho.

Aidha, alisema waliopoteza kadi ya mpiga kura lakini wana vitambulisho vingine vilivyoruhusiwa na tume kutumika wanaweza kupiga kura baada ya kuhakikiwa.

Hata hivyo, aliwataka wapiga kura kufuata maelekezo ya msimamizi wa kituo na kuepuka kukiuka taratibu za uchaguzi ili kuepusha migogoro isiyo na sababu.

Chanzo: Habari Leo
 
Kila mtu akikosea na kuomba karatasi ingine tutakesha labda akikosea arudi nyuma akapange foleni upya kabisa ILI ASIPOTEZEE MUDA watu wengine
 
Hapa wangefafanua Mazingura ya kubadili mawazo sababu:

Haiwezekani mtu umepiga kura kabla hujatumbukiza na hujaiaribu kwa lolote ; kabla hujaitumbukiza ukabadili mawazo; halafu upewe karatasi nyingine !! Ina.maana alishirurushwa !
 
Hii vurugu sasa. Ikitoa hiyo nafasi na ikatoe kundi kubwa la watu wanafika kwenye kichumba cha kupigia kura na baadaye kurudi kwa namna hiyo, upigaji kura utakwenda vizuri kweli. Hata monitoring yake inaweza kuwa ngumu na pengine vyama vingine kutumia nafasi hiyo kupiga kura mara mbili kama hizo zinazoitwa zimekosewa hazita kuwa na uangalizi mzuri.

Ni bora mtu apewe tahadhari ya kuwa makini na ndiyo maana kuna kura zilizoharibika wakati wa kuhesabu.
 
Hapa wangefafanua Mazingura ya kubadili mawazo sababu:

Haiwezekani mtu umepiga kura kabla hujatumbukiza na hujaiaribu kwa lolote ; kabla hujaitumbukiza ukabadili mawazo; halafu upewe karatasi nyingine !! Ina.maana alishirurushwa !
Pia ile ambayo hajaiharibu na amebadili maamuzi, ataipeleka wapi? au atazidumbukiza zote kwa pamoja, kuna harufu chafu inanukia humu...
 
Sasa watajuaje kama haki za mpiga kura haziko wazi tangu siku ya kwanza ya kutangaza uchaguzi?
na iweje kwamba mtu anaweza kuomba karatasi nyingine? ni vema waakanza utaratibu wa electro voting kwa kweli
 
KILA mtu akikosea na kuomba karatasi ingine tutakesha labda akikosea arudi nyuma akapange foleni upya kabisa ILI ASIPOTEZEE MUDA watu wengine
Hapa inawezekana ccm ikaibiwa kura. Nani anayehakiki kuwa imekosewa? Na utaratibu wa kuichana au kuidespose upoje?
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi wa utaratibu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu na kusema mpiga kura aliyeharibu kwa bahati mbaya karatasi ya kupigia kura akiwa kwenye kituturi kwenye kituo cha kupigia kura, anaweza kuirudisha karatasi hiyo kwa msimamizi wa kituo na kuomba apewe nyingine ili apige kura yake vizuri.

Hayo yalisemwa na Ofisa wa NEC, Flora Mkama jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari watakaoripoti uchaguzi mkuu unaofanyika nchini kote wiki ijayo Oktoba 28.

Akitoa mada kuhusu utaratibu wa kupiga kura, Mkama alisema mpiga kura aliyefika kituo cha kupigia kura na kuhakikiwa kisha kupewa karatasi ya kupigia kura na kuelekea kwenye kituturi cha kupigia na baadae akabaini amekosea kupiga anaruhusiwa kumrudishia msimamizi wa kituo karatasi hiyo kabla ya kuitumbukiza kwenye boksi la kura na kuomba nyingine ili kukamilisha upigaji kura wake.

"Inawezekana wapiga kura hawajui kuwa wana haki ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura endapo itatokea kwa bahati mbaya amekosea au amebadili uamuzi wake wakati akiwa kwenye kituturi atarudisha karatasi hizo kama ni zote au moja kati ya hizo tatu, yaani rais, ubunge au udiwani na kuomba kupewa nyingine ili akachague mgombea amtakaye."

"Inawezekana mtu amekosea katika kuchagua akakuta ameweka alama kwa mgombea ambaye hakumtaka au ameamua kubadilisha uamuzi sasa kuliko aharibu ile karatasi kwa kukatakata anatakiwa airudishe kwa msimamizi alafu aombe nyingine akapige," alisema.

Mkama alisema mpiga kura akiirudisha karatasi hiyo kwa msimamizi wa kituo msimamizi huyo ataichukua na kuandika kwa nyuma ‘Imefutwa’ na kuiweka katika bahasha namba 3A iwapo ni ya Rais au kama ni ya wabunge itawekwa bahasha namba 3B na udiwani bahasha namba 3 C.

Alisema mpiga kura atakayepewa karatasi nyingine ya kupigia kura ni yle tu ambaye alikuwa kwenye kituturi cha kupigia kura na sio aliyekwishapiga kura na kutumbukiza kwenye sanduku la kura.

Akizungumzia wapiga kura wenye sifa, Mkama alisema wanaoruhusiwa kupiga kura kwenye kituo husika ni wale tu waliojiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kwenye kituo hicho.

Aidha, alisema waliopoteza kadi ya mpiga kura lakini wana vitambulisho vingine vilivyoruhusiwa na tume kutumika wanaweza kupiga kura baada ya kuhakikiwa.

Hata hivyo, aliwataka wapiga kura kufuata maelekezo ya msimamizi wa kituo na kuepuka kukiuka taratibu za uchaguzi ili kuepusha migogoro isiyo na sababu.

Chanzo: Habari Leo
Ajabu: form za matokeo wanasema mawakala watapewa "kama zitakuwepo" lakini karatasi za kupigia kura wameweka za ziada!

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom