NEC hoi, itaharibu mambo

NEC hoi, itaharibu mambo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwa sababu ya NEC. NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa, katika kuandikisha wapiga kura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.

Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.

NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.

NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
haya aliwah kuyasema Nguruvi3 kwamba NEC iache kuhadaa watu kwamba watamaliza kufanya kazi ya kuandikisha kwa mudaa huu mfupi ili kura ya maoni ipigwe
haya sasa hata njombe hapajaisha kura ya maoni ni mwezi wa 4 inakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Umenena mkuu, mambo ya kutumia mabavu hayatafanikiwa. Maridhiano ya hatua kwa hatua na wadau wote ni muhimu katika jambo hili. Kuweka kura ya maoni Aprili 30 ni moja ya mfano hai wa kutaka kutumia mabavu, mambo mengine hayaendi hivyo.

Ila huenda pia ni mgomo baridi maana ya kura ya maoni ilipaswa kutangazwa na tume, lakini mkuu wa kaya akajichukulia majukumu ya kutangaza.
 
chanzo cha vulugu kwenye uchaguzi ni pamoja na kuwahi kumaliza kazi!!! kama muda wote wako njombe! kanda ya ziwa je???
 
kwa UMRI alionao Jaji Lubuva hastahili
kuendelea na utumishi wa Umma tena.

JK ndio wa kulaumiwa..angalia wenzetu Kenya wanaongozwa na vijana kwenye tume ya uchaguzi..sisi tunachukui hii mizee iko kwenye menopause ndo tunaipa mamlaka ..haya sasa bvr vurigu tupu mpaka tunaenda kuazima Kenya ! Aibu
 
kwa UMRI alionao Jaji Lubuva hastahili
kuendelea na utumishi wa Umma tena.
Sijui kwa nini tunang'ang'ania lazima kiongozi wa NEC awe jaji mstaafu. Nafasi hii siyo ya kutoa hukumu au kuitafasiri sheria ni nafasi ya kuongoza taasisi. Tuiache iwe huru kuongozwa na mtu mwenye uwezo, hali na nguvu za kuwajibika.
 
Anayelazima huu mchakato kum'make sana! Anayedanganya watu kuwa mchakato unaendelea vizuri na kura ya maoni itafanyika April 30 kum'make sana na ma.ta.ko yake!! Kwa ufupi UKAWA hapa wamepiga 3-0 maana walisema tangu mwanzo kuwa muda ni mfupi mno!! Lubuva ona aibu Mzee hili zoezi limebuma, hivi mtu huoni aibu mpaka unautangazia umma eti ulienda kuazima mashine za BVR Kenya na Nigeria, shenji kabisa yaani wenzio watumie kodi zao Wewe uende kuazima? AIBUUUUUUUU! NEC mmejivua nguo!!
 
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwasababu ya NEC.NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa,katika kuandikisha wapigakura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.

Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.

NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.

NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kweli kabisa mkuu, kuna siku niliwahi kuweka uzi hapa kuhusu Mzee Lubuva kuwa amechoka kimwili na kiakili hawezi hii kazi, na haoni hatari ya mbeleni kwa taifa hili endapo mambo yatavurugika kwa watu kukosa haki yao ya msingi. Ifike mahali mwenyekiti wa tume ya uchaguzi si lazima awe jaji anaweza kuwa mtu yeyote mwenye uwezo. Kenya walikuwa na kijana mdogo kabisa Bw. Isack kama sikosei alikuwa around 40yrs. Sasa leo tunakuwa na mtu hata kumbu kumbu zimeanza kumtoka bado tunampa majukumu mazito na yenye kugusa maslahi mapanda na mustakabali wa nchi yetu.
Taifa hili watu 45 milioni kweli tunakosa mtu makini atufanyie hii kazi??????
 
Calculation za Kikwete ni za hovyo sana anajidharilisha na kudharilisha nchi wote mpaka akina Lubuva tunaonekana hatuna akili kweli Kikwete na serikali yake na chama chake wamekamua hazina hadi kushindwa kununua vitendea kazi vya uandikishaji ujambazi wao sasa unaangaliwa kwa jicho la karibu sana tunajua hakuna kura ya maoni lakini uchaguzi utafanyika watake wasitake manake lengo la kikwete kuendelea kukaa madarakani ili yeye mkewe wanawe waendelee kuifirisi nchi
 
Ndio tatizo la nafasi hizo kupewa watu kama fadhila hivyo aliyetoa nafasi ya uteuzi huo hata angetamka kuwa kura hiyo itafanyika baada ya siku kumi mteuliwa hata akiona haiwezekani bado atamjibu mteuaji wa fadhila YES SIR! Watendaji huru huwa wanasema lipi linawezekana na lipi haliwezekani bila kigugumizi.
NEC wawe wakweli na kumwambia JK hatuwezi kwa muda huo na usiogope kubadili kauli yako badili tarehe kwa kushirikiana na wadau la sivyo utaumbuka. Basi.
 
Kweli kabisa mkuu, kuna siku niliwahi kuweka uzi hapa kuhusu Mzee Lubuva kuwa amechoka kimwili na kiakili hawezi hii kazi, na haoni hatari ya mbeleni kwa taifa hili endapo mambo yatavurugika kwa watu kukosa haki yao ya msingi. Ifike mahali mwenyekiti wa tume ya uchaguzi si lazima awe jaji anaweza kuwa mtu yeyote mwenye uwezo. Kenya walikuwa na kijana mdogo kabisa Bw. Isack kama sikosei alikuwa around 40yrs. Sasa leo tunakuwa na mtu hata kumbu kumbu zimeanza kumtoka bado tunampa majukumu mazito na yenye kugusa maslahi mapanda na mustakabali wa nchi yetu.
Taifa hili watu 45 milioni kweli tunakosa mtu makini atufanyie hii kazi??????

CCM mambo ni kuigana igana tu .................... kwa kuwa Nyerere alifanya hivi basi lazima Mwinyi, Mkapa na Kwikwete afanye vile vile!! Nyerere alikuwa anazungumza na wazee wa Dar lazima kila Rais ajae afanye vivyo hivyo!!

Kwa vile Mwinyi aliteua Jaji mstaafu kuongoza tume then Mkapa na Kikwete lazima wafanye vivyo hivyo!!

Tanzania tunafanya mambo kwa mazoea kama kuku ndiyo maana hatuendi popote!!
 
JK ndio wa kulaumiwa..angalia wenzetu Kenya wanaongozwa na vijana kwenye tume ya uchaguzi..sisi tunachukui hii mizee iko kwenye menopause ndo tunaipa mamlaka ..haya sasa bvr vurigu tupu mpaka tunaenda kuazima Kenya ! Aibu
Kigogo chama chetu mahiri kimechoka, kimezeeka, kimeishiwa kila aina ya mipango mkakati. Sasa hakijielewi, nimesikitishwa na mpango mkakati wa Kinana na Nape Nnauye kutembea na fisi, ili kuvuta watu mikutanoni, wanataka kujustify nini... Najua wana uhakina na maddudu toka katika vyombo vya kiserikali kusaidiwa ikiwezekana mabavu.

So, haya ya NEC ya Lubuva wala si ajabu ni muendelezo hu huuu.....
 
Last edited by a moderator:
Hicho mnakifanya makusudi, kuteua wazee waliochoka kuendesha taasisi nyeti kama NEC
 
Nilishasema mara nyingi na nitaendelea kusema tu.Mwaka huu hakuna uchaguzi na si kwa bahati mbaya,bali huu ni mpango na mkakati wa makusudi kuhujumu uchaguzi.

Time will tell.
 
Umenena mkuu, mambo ya kutumia mabavu hayatafanikiwa. Maridhiano ya hatua kwa hatua na wadau wote ni muhimu katika jambo hili. Kuweka kura ya maoni Aprili 30 ni moja ya mfano hai wa kutaka kutumia mabavu, mambo mengine hayaendi hivyo.

Ila huenda pia ni mgomo baridi maana ya kura ya maoni ilipaswa kutangazwa na tume, lakini mkuu wa kaya akajichukulia majukumu ya kutangaza.

Watumishi wa NEC ni watanzania ambao hawapendi pia jinsi mambo yanavyoendeshwa kihuni. Mchakato ulikuwa haramu, na hivyo hakuna anayependa kuupigia chapuo. Si busara kulazimishia watanzania katiba ambayo hawakuipendekeza wao. Hii ni katiba ya baadhi ya viongozi sio ya wananchi.

Kwa hapa tulipofikia, UONGOZI unahitajika, bahati mbaya sina uhakika kama tunao uongozi wa kututoa hapa, democrass inahujumumiwa peupee bila kujali, LAKINI mwisho watashindwa na kuona aibu
 
Back
Top Bottom