Nec: Hatuboreshi Daftari la Wapiga kura

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Ukisikia kuna uchaguzi mdogo hatukosi kuisikia Tume ya Uchaguzi nayo ikisema;"hatutaboresha daftari la wapiga kura, vituo vya kupigia kura vitakuwa vile vilivyotumika katika uchaguzi ulipita..." Ninapenda kujua kuwa gharama ya kuwaingiza wapiga kura wapya na kuwatoa waliohama ua kufa ili kuboresha daftari ni kiasi gani? Je, huko kutoboresha daftari la wapiga kura lina maslahi kwa nani?

Nina imani kubwa kabisa idadi ya wapiga kura wa Jimbo la Arumeru Mashariki katika uchaguzi mkuu wa 2010 na leo wanapofanya uchaguzi mdogo ni tafauti kabisa. Hii ikiwa na maana kuwa wapo waliokuwa na umri wa watoto na leo ni watu wazima. Wapo waliokufa na wapo waliohama vile vile.

Hivi umuhimu wa kuboresha daftari haupo kweli? wapo watu wengi wanapoona umati wa watu katika mikutano wakivishabikia vyama fulani, wanakuja na kauli kuwa, "usifikiri wote wana vitambulisho vya kura". Hiyo ina maana kuwa kushiriki kwao katika ushabiki wa chama fulani hakutaleta athari katika uchaguzi kwa sababu ushabiki wao hautakuwa na nafasi katika kupiga kura. Jambo la kuchekesha ni kuwa hata hao washabiki wakitaka kujiandikisha hawana nafasi sasa bali ile iliyopita, yaani uandikishaji katika uchaguzi mkuu uliopita.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom