NEC: Hakuna kura ya maoni bila daftari jipya

NEC: Hakuna kura ya maoni bila daftari jipya

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haitaendesha uchaguzi wa aina yoyote, wala kuitisha kura ya maoni hadi kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura itakapokamilika.

Kauli ya NEC imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na kulitaja suala la uboreshaji wa daftari la hilo kama mambo matatu yanayoiweka kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo njiapanda.

Mambo mengine ni Sheria inayotaka kura hiyo ipigwe ndani ya siku 84 baada ya Katiba inayopendekezwa kuchapishwa na kufanyiwa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema jana kwamba kuendesha uchaguzi bila kuboresha daftari hilo ni kuongeza malalamiko kwa wananchi na wadau, hususan vyama vya siasa.

"Msimamo wetu (NEC) ni kuwa bila daftari kuboreshwa hatuko tayari kuendesha uchaguzi wowote na hata huo wa kura ya maoni," alisema na kuongeza:

"Sasa tuna takriban vijana milioni 2.3 ambao wamefikisha umri wa kupiga kura ... lakini kuna watu waliokufa, vyote hivi vinatakiwa kuboreshwa kwanza na sisi Tume hatuko tayari, naomba muwaambie wananchi."

Kuhusu hoja kwamba NEC itumie daftari lililopo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika uchaguzi mdogo mara kwa mara pale mbunge anapofariki dunia, Jaji Lubuva alisema tume yake haitaki yajirudie malalamiko ambayo imeyapata kupitia uchaguzi wa aina hiyo.

"Katika Uchaguzi wa Kalenga, Arumeru Mashariki na Chalinze, tulilalamikiwa sana kuhusu matumizi ya daftari hili, hivyo kutokana na malalamiko hayo yaliyotoka kwa vyama vya siasa, hatutaki tena kupata mengine kama hayo, ndiyo maana nasema muwaambie wananchi kwamba hatutaendesha chaguzi zozote hadi pale tutakapoboresha daftari," alisema Jaji Lubuva.

Kuhusu lini kazi ya kuboresha daftari hilo itaanza, Jaji Lubuva alisema: "Tunasubiri vifaa vifike na vitakapofika tu tutaanza mara moja."

Kauli ya Rais Kikwete

Akizungumza juzi katika sherehe ya makabidhiano ya Katiba inayopendekezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alielezea maeneo matatu yenye utata ambayo yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili kufanikisha hatua hiyo.

Alisema suala la kwanza ni ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao ambayo inaonyesha mchakato wa kuandika upya Daftari la Wapiga Kura utakamilika Mei 2015.

Alisema suala hilo litaingiliana na mchakato wa Kura ya Maoni ambayo inatakiwa ifanyike ndani ya siku 84 tangu siku ambayo Katiba inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa Rais.

Alisema ili suala hilo lifanikiwe, ni lazima Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho, jambo ambalo linaweza kushughulikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atatakiwa kupeleka muswada bungeni.

"Ikifika Mei inabaki miezi miwili au mitatu kabla ya Bunge kuvunjwa na hapo ndipo watu huanza kampeni za uchaguzi mkuu.

"Lakini wapo pia wanaopingana na NEC. Wao wanasema mbona akifariki mbunge uchaguzi hufanyika. Jambo hili ninawaachieni na pale ambapo litapatiwa ufumbuzi mtaelezwa."

Alisema kutokana na kuwapo kwa utata huo, ni jambo gumu kwa Katiba Mpya kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa sababu ya utata wa masuala hayo matatu, huku akisisitiza jambo hilo kutazamwa ili kuona kama linaweza kupatiwa ufumbuzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna ukweli Hapo lakini naomba kuuliza,kama wakiboresha mwaka huu kwa ajili ya kura ya maoni mwakani kabla ya uchaguzi 2015 kuna watu wengine watafikisha hiyo miaka 18 na wengine watakua wameshafariki.je wataboresha tena?
 
Hawaboreshi mwaka huu. Walishasema wataboresha mwaka kesho na wamesema hilo zoezi linatarajiwa kukamilika May 2015 na ndio maana kura ya maoni inategemewa kupigwa baada ya uchaguzi mkuu !

Kuna ukweli Hapo lakini naomba kuuliza,kama wakiboresha mwaka huu kwa ajili ya kura ya maoni mwakani kabla ya uchaguzi 2015 kuna watu wengine watafikisha hiyo miaka 18 na wengine watakua wameshafariki.je wataboresha tena?
 
Hapo sawa ila isije ikawa porojo tu,manake na nyie hamkawii kuruhusu akili zenu wazishikilie manyani ya Chama Cha Majambazi/Mafisadi/Majizi/Matesaji/Maharamia/Marogaji/Maongo/Makabaji. n.k
 
.....yes jaji Lubuva uko sahihi kabisa.Tunadai haki yetu ya kuchagua na kuchaguliwa,kura ya maoni isije kabla hatujaandikishwa
 
Jamani hii tume sio ya kusimamia kura za maoni, inatakiwa tume huru. Tume hii ni ya rais kaichagua yeye sasa unategemea nini katika katiba hii. Hawawezi kusema kweli watapindua matokeo ya kura ya maoni tu. nani wa kuwauliza na sheria inasema hakuna kupinga matokeo yakishatangazwa.
 
Boresha daftari kwanza. Hakuna sababu ya kuwahisha kura ya maoni na kuwanyima haki wapiga kura ambao kwa sasa hawajaandikishwa
 
Jaji Lubuva una busara kama za babu Warioba Mungu akuweke hapo hado unayokusudia kuyasimamia uyakamilishe. Daftari liboreshwe kura ya maoni na uchaguzi mkuu ndio vifanyike.
 
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haitaendesha uchaguzi wa aina yoyote, wala kuitisha kura ya maoni hadi kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura itakapokamilika.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema jana kwamba kuendesha uchaguzi bila kuboresha daftari hilo ni kuongeza malalamiko kwa wananchi na wadau, hususan vyama vya siasa.

Kwa hili naona Jaji Damian anauelewa wa kutosha.
“Msimamo wetu (NEC) ni kuwa bila daftari kuboreshwa hatuko tayari kuendesha uchaguzi wowote na hata huo wa kura ya maoni,” alisema na kuongeza:

“Sasa tuna takriban vijana milioni 2.3 ambao wamefikisha umri wa kupiga kura ... lakini kuna watu waliokufa, vyote hivi vinatakiwa kuboreshwa kwanza na sisi Tume hatuko tayari, naomba muwaambie wananchi.”

Haraka hii ya nini?
Yaani uwaache hao 2.3milioni kana kwamba si watanzania,kweli CCM hawana nia njema na Nchi.Ila kilicho wazi CCM wanawaogopa hao vijana 2.3milioni maana elimu ya Uraia imeingia na wanajitambua.

Alisema ili suala hilo lifanikiwe, ni lazima Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho,
jambo ambalo linaweza kushughulikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atatakiwa kupeleka muswada bungeni.

“Ikifika Mei inabaki miezi miwili au mitatu kabla ya Bunge kuvunjwa na hapo ndipo watu huanza kampeni za uchaguzi mkuu.

Si wapeleke mswada Bungeni hapo November -2014 kama wanataka hiyo kura ya maoni kabla ya Uchaguzi.
 
IMG_4357.jpg
Z
9k=

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haitaendesha uchaguzi wa aina yoyote, wala kuitisha kura ya maoni hadi kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura itakapokamilika.

Kauli ya NEC imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na kulitaja suala la uboreshaji wa daftari la hilo kama mambo matatu yanayoiweka kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo njiapanda.

Mambo mengine ni Sheria inayotaka kura hiyo ipigwe ndani ya siku 84 baada ya Katiba inayopendekezwa kuchapishwa na kufanyiwa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema jana kwamba kuendesha uchaguzi bila kuboresha daftari hilo ni kuongeza malalamiko kwa wananchi na wadau, hususan vyama vya siasa.

“Msimamo wetu (NEC) ni kuwa bila daftari kuboreshwa hatuko tayari kuendesha uchaguzi wowote na hata huo wa kura ya maoni,” alisema na kuongeza:

“Sasa tuna takriban vijana milioni 2.3 ambao wamefikisha umri wa kupiga kura ... lakini kuna watu waliokufa, vyote hivi vinatakiwa kuboreshwa kwanza na sisi Tume hatuko tayari, naomba muwaambie wananchi.”

Kuhusu hoja kwamba NEC itumie daftari lililopo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika uchaguzi mdogo mara kwa mara pale mbunge anapofariki dunia, Jaji Lubuva alisema tume yake haitaki yajirudie malalamiko ambayo imeyapata kupitia uchaguzi wa aina hiyo.

“Katika Uchaguzi wa Kalenga, Arumeru Mashariki na Chalinze, tulilalamikiwa sana kuhusu matumizi ya daftari hili, hivyo kutokana na malalamiko hayo yaliyotoka kwa vyama vya siasa, hatutaki tena kupata mengine kama hayo, ndiyo maana nasema muwaambie wananchi kwamba hatutaendesha chaguzi zozote hadi pale tutakapoboresha daftari,” alisema Jaji Lubuva.

Kuhusu lini kazi ya kuboresha daftari hilo itaanza, Jaji Lubuva alisema: “Tunasubiri vifaa vifike na vitakapofika tu tutaanza mara moja.”

Kauli ya Rais Kikwete
Akizungumza juzi katika sherehe ya makabidhiano ya Katiba inayopendekezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alielezea maeneo matatu yenye utata ambayo yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili kufanikisha hatua hiyo.

Alisema suala la kwanza ni ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao ambayo inaonyesha mchakato wa kuandika upya Daftari la Wapiga Kura utakamilika Mei 2015.

Alisema suala hilo litaingiliana na mchakato wa Kura ya Maoni ambayo inatakiwa ifanyike ndani ya siku 84 tangu siku ambayo Katiba inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa Rais.

Alisema ili suala hilo lifanikiwe, ni lazima Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho, jambo ambalo linaweza kushughulikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atatakiwa kupeleka muswada bungeni.

“Ikifika Mei inabaki miezi miwili au mitatu kabla ya Bunge kuvunjwa na hapo ndipo watu huanza kampeni za uchaguzi mkuu.

“Lakini wapo pia wanaopingana na NEC. Wao wanasema mbona akifariki mbunge uchaguzi hufanyika. Jambo hili ninawaachieni na pale ambapo litapatiwa ufumbuzi mtaelezwa.”

Alisema kutokana na kuwapo kwa utata huo, ni jambo gumu kwa Katiba Mpya kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa sababu ya utata wa masuala hayo matatu, huku akisisitiza jambo hilo kutazamwa ili kuona kama linaweza kupatiwa ufumbuzi.

Chanzo: Mwananchi

Sijui kwanini MwanaDiwani anaogopa sana kuboreshwa kwa daftari la wapiga kura .
 
Yatatokea mazingaombwe , hamtaamini.

Sitashangaa kwasababu tumeona mengi ktk kile kilikuwa kinaitwa BMK ambako hata waliodhaniwa bado wana heshima kidogo wamefanya mambo ya aibu kwa Taifa!

Hii ilikuwa moja ya hoja ya msingi kati ya Rais Kikwete na Viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye Wabunge iliyo pelekea kuja na agizo kwamba Mchakato Usitishwe kutokana na ufinyu wa muda wa Kuboresha Daftari la Wapiga Kura.

Hata hivyo wenye Katiba yao wakaona wote huo ni Ujinga mtupu! Mimi sijawahi sikia popote Bunge la Kutunga Katiba la kijuha kama letu! Wakenya walitaka kufanya kosa letu lkn wananchi wakawa wakali wakawatimua wanasiasa na takataka zao ktk mchakato wao wa kuandika Katiba ya Kenya.

Jaji amewawahi kwa kujitokeza mapema na kukataa kutumika. Wanaelewa kama Katiba yao itachelewa kupitishwa basi Watanzania watatambua wameuziwa Mbuzi ktk Gunia... Hawataki mjadala huu uendelee kwa hiyo unaweza ukasikia pesa zimetolewa haraka haraka zoezi la kuandikisha limeanza hata kama litakatwa fungu la miradi ya maendeleo!!
 
tuombe mungu wasimmalizie kabla siku zake hazijatimia.maana haikawii kuambiwa ati majambazi ......
 
Back
Top Bottom