Ndullu akataa kutaja adhabu'waliochemsha' BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndullu akataa kutaja adhabu'waliochemsha' BoT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 28, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Ndullu akataa kutaja adhabu'waliochemsha' BoT


  Na Reuben Kagaruki

  GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, amesema hatarajii kutangaza leo wala kesho hatua watakazochukuliwa watumishi wa benki hiyo wanaodaiwa kuhusika kufanikisha kampuni 22 kuchota kiasi cha sh. bilioni 133 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya kumalizika mjadala kuhusu aliyekuwa Gavana wa benki hiyo, marehemu Gilman Tutihinda, uliofanyika Dar es Salaam , Prof. Ndulu, alisisitiza kuwa atatangaza hatua za kuwachukulia baada ya mchakato wa kuwahoji na kuwasikiliza kumalizika.

  "Kamati inayoshughulikia suala hili inafanya hivyo ili kutafuta haki, sitarajii kutangaza matokeo leo wala kesho," alisisitiza Prof. Ndullu.

  Huku akikaata kueleza hatua za uchunguzi na kuwahoji zilipofikia, Prof. Ndullu hakuwa tayari kutaja idadi yao. Alipobanwa na gazeti hili ataje ni wafanyakazi wangapi wa benki hiyo wanadaiwa kuhusika, alisema 'sijui.'

  Alipobanwa zaidi kuhusu suala hilo , Prof. Ndullu alisema tayari suala hilo alishawaeleza waandishi wa habari na kumtaka mwandishi wa habari hizi kurejea kumbukumbu zake.

  Awali akifungua mjadala huo, Prof. Ndullu, aliwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kuchangia mfuko wa Elimu wa Gilman Rutihinda ambao umeweza kusomesha watu wengi.

  Alisema baadhi ya watu wamesomeshwa shahada ya pili na mfuko huo. Alisema wanafunzi 17 wanaofanya vizuri katika maeneo yaliyoainishwa wamekuwa wakisomeshwa na mfuko huo.

  "Mfuko utaendelea kutoa udhamini, tunatoa mwito kwa wadau wote waendelee kuuchangia," amesema.

  Kwa upande wake mtoto wake hayati Rutuhinda, Renatha Rutihinda aliwashukuru wote ambao wamekuwa wakijitolea kuendeleza mfuko huo na kuwataka waendeleze moyo huo.
   
Loading...