Ndugu Zetu Wazanzibari.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu Zetu Wazanzibari....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoboasiri, Apr 27, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nimesikiliza kipindi cha BBC kilichomalizika hivi punde juu ya maoni ya Watanzania kuhusu Muungano. Nilichosikia leo kutoka kwa waliojitambulisha kuwa ni Wazanzibari hakina tofauti na kile ninachokisoma kutoka kwa watu wanaojitambulisha humu ukumbini kuwa ni Wazanzibari kila siku.

  Kwa ufupi, madai yaliyopo ni haya:

  • Muungano si halali na mwanasheria mkuu wa Zanzibar alishakiri kutokuwepo (au at least hakuwahi kuziona) hati za Muungano. Kilichopo ni hati iliyotiwa sahihi na Pius Msekwa (akiwa katibu wa bunge) na Adam Sapi Mkwawa (msemaji alisema akiwa mbunge lakini naamini - nipo tayari kusahihishwa katika hilo -akitaka kusema "spika wa bunge") na Mzee Karume.
  • Muungano huu ni wa ghilba, ujanja ujanja na wa vitisho kutoka Tanzania Bara (soma Tanganyika). Wazanzibari hawajawahi kuuridhia na Baraza la Mapinduzi halikuwa na uhalali wa kuidhinisha Muungano kwa kuwa halikuwahi kuchaguliwa na Wazanzibari.
  • Muungano uliopo ni mpango wa Nyerere kutaka kuifuta Zanzibar kitu ambacho hakikubaliki.
  • Kuwepo na kura ya maoni kuamua kama Muungano uwepo ama la, na kama uwepo uwe wa aina gani.
  Mimi binafsi (na ni Mtanganyika) sioni ninachofaidika na kuwepo au hasara nitakayopata kwa kutokuwepo kwa Muungano huu - japo ninaamini (kwa kusoma historia na kuunganisha matukio ya hapa nchini, Afrika na duniani kwa ujumla kipindi Muungano huu unaanzishwa) kwa nini kilichofanyika kuhusu Muungano huu kilipaswa kufanyika. Naamini pia kuwa mazingira yaliyopo yamebadilisha kwa kiasi kikubwa namna mataifa yanavyoshirikiana.

  Ushauri wangu: Tuache malumbano yasiyokwisha wakati uwezo wa kukipata kile tunachokihitaji upo mikononi mwetu wenyewe. Wazanzibari mna bunge lenu na serikali yenu na mna uwezo wa kuamua (bila hata kutushirikisha Watanganyika) kujiondoa kwenye hiyo ghilba na kulazimishwa kufanya msichokitaka.

  Malalamiko yenu yasiyokwisha (wakati hamchukui hatua huku uwezo mnao) yanatupotezea malengo yetu huku. Mnawapa nafasi watu kutufanya tuache kujadili mambo ya maana zaidi kwa nchi yetu kwa kisingizio cha kutatua kero zilizopo kwenye Muungano ambao wala hamuoni manufaa yake. AMUENI LEO. Chukueni hatua, kulalamika kila siku hakutawafikisha popote.

  Wenzenu tunahitaji kumuua nyoka anaejitoa magamba ili tuweze kuwa na mfumo utakaotuletea maendeleo yanayokwamishwa na watawala wasiojua wanafanya nini.
   
 2. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kiakili wazanzibari si wazima, msiniamini, lakini chunguzeni, iko siku mtanikumbuka.
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Pharaoh,
  wewe ni katika wao? Kwa hiyo ni first hand info?.. au unafanya kazi Mirembe na wao ni wagonjwa wako unaowasaidia huko kwa hiyo una data za kuthibitisha unayosema au?

  Uchunguzi wako ndio ulikupa hitimisho hilo? Ulichunguza nini na uliona nini?

  Hata hivyo,unaweza kujadili mada bila ya lugha kama hizi za kuchokoza nyuki!
  kwa bahati lugha zinazotawala mijadala ya siasa za muungano zinachakachuliwa ili kupoteza ,kupindisha mjadala.

  Kwa nini hatujadili faida na hasara za muungano kwa kila upande, na hata kwa wananchi wa kawaida?..ikiwezekana backed with data badala ya kejeli na matusi!!

  Muanzisha mada huelewi kuwa kuna kambi nyingi za jeshi kule Zanzibar ili wakileta fujo tuwadhibiti?..huelewi kuwa CCM wanajitangaza kuwa washindi kule kwa kuviweka stand by vyombo vya ulinzi kama hawatotangazwa..jeshi linaidhibiti Zanzibar? Tuache "unafiki"...tatizo tunalijua lilipo wala halihitaji mtoto kumwambia "mfalme anatembea uchi...kila mtu anajua mfalme hana nguo.

  sasa vipi tufanye tumvalishe nguo, au tumshawishi avae nguo... ndio pa kuanzia..
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilikwambia mwanzoni kuwa kauli zako zinaendana na jina lako.

  Kama huwezi kujadiliana, kwanini usijinyamazie?

  Kwanini unapenda kutumia matusi ya reja reja dhidi ya Wazanzibari?

  Au umekosa hoja Pharaoh?
   
 5. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Na hii ndio kazi yao kila uchaguzi:

  haya tena basi jamani 2.jpg

  haya tena basi jamani.jpg


  Muungano huu unadumu kwa ukandamizaji na udhalimu namna hii. Lakini yana mwisho wake haya.

  Halafu vipi tuukubali "muungano" wa namna hii?
   
 6. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hata Sudan ya Kusini kulikuwa na kambi za jeshi (na kumbuka wao hawakuwa na bunge wala serikali yao). Hali kadhalika, Pakistani walipojitoa India, Bangladesh walipojitoa Pakistan, Eritrea, Somaliland, n.k, n.k. Kama wao waliweza (bila kuwa na serikali na bunge linalotambuliwa kisheria) nyie iweje mshindwe?

  Nina uhakika serikali ya Muungano (nyie mnaita ya Tanganyika) haiwezi kuwazuia mkitoa tamko rasmi (kupitia serikali yenu au kwa namna yeyote mtakayo ona inafaa) la kujitoa kwenye Muungano. Pinda si alishawaambia wazi wazi bungeni? Huo uoga wa kambi za jeshi mbona haukuonekana mlipokuwa mnajadili habari ya mafuta (ambayo wala hayajagunduliwa) na kutoa tamko kwenye baraza la wawakilishi kuwa Zanzibar ni nchi (na wala si sehemu ya Tanzania)?

  Wala msihofu, mkitoa tamko kupitia vyombo halali jumuiya ya kimataifa itawaunga mkono nina uhakika (ukichukulia kuwa nchi yetu wala haijafikia hata kuwa "Banana Republic"), mbona Kosovo wamejitenga wakati Serbia haitaki? Chukueni hatua, la hamuwezi kaeni kimya. Tumechoshwa kusikia malalamiko yasiyoisha (na kwa mtazamo wangu hayana mantiki yeyote). Kwa nini ulalamike kunyeshewa mvua wakati uko kwako, si uingie ndani tu yaishe?
   
 7. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wazanzibar wazuri katika kupiga domo.. lakini si kwa vitendo...! mfano mzuri kama alosema mdao hapo juu.. sudani kusini ...
   
 8. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kafanye tena huo utafiti wako.... Ila utafiti wangu mimi ,sijawahi kuona Mzanzibar anafanya kazi nyumbani kwa Mtanganyika....hio kwangu mimi ni akili tosho...
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280

  Sisi vs wao?
  wewe vs mimi?

  Au unazungumzia hoja?
  Yule prof aliyeuwawa, alikuwa mrwanda kwa sababu alikuwa anamwakilisha,anamtetea mrwanda mahakama ya kimataifa ya Arusha?

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/124295-majibu-ya-membe-mchango-wa-tanzania-kutatua-mgogoro-wa-libya-ni-kupitia-african-union-a-u.html#post1825261
   
 10. A

  Albimany JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mdomo ni pigo ukijua kuutumia hata kushinda risasi na kama huamini utaona matokeo yake.

  Munatakiwa kwanza mufahamu nini matakwa yetu na nini hoja zetu na imani yangu ni kua munaanza kuelewa.

  Wazanzibari hawana nia mbaya wanataka kujikomboa na pia kuwakombolea nchi yenu(Tanganyika) ambayo kwa sasa hamujajua kua munaibiwa Kwa kutumia neno MUUNGANO.

  Mutawaelewa Wazanzibari siku za mbele.
   
 11. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtoboasiri.
  Sudan ya kusini ni matokeo ya vita vya muda mrefu....baadae,Interest ya West,US in sudan Oil na UN kupitia mazungumzo ya serikali ya AL bashir na "waasi" au wanaharakati wa kusini ndio yalipelekea Waasi kuingia serikali ya Al Bashir na referendum ikafuatia....je unataka TZ pia ipitie mkondo huu? Vita na uasi na sio mjadala na majadiliano?

  India na Pakistan... ni Muingereza ndio aligawa hizo sehemu kulingana na wakaazi wa sehemu moja kuwa kundi la aina moja, wahindu,waislamu....devide and rule!...Pitia historia hiyo mkuu.

  Mifano mengine pia ni ile iliyopelekea vita, mapambano ya silaha....hapa TZ..maradhi na njaa na peke yake inatumaliza..sifikirii tunahitaji vita kumaliza matatizo ya Muungano. Unahitajika mjadala wa wazi wa kitaifa wa Muungano na mfumo wake na pia referendum kuamua hatima ya sehemu zilizoungana kama ziendelee kuungana katika baadhi ya mambo au kila nchi iende kivyake kama Senegambia.
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Umenifanya nicheke, asante kwa hili.....unafaa kuwa mshauri wa rais wa serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili umsaidie katika kutatua hili jinamizi la Muungano.
  Na umshauri vipi atekeleze kwa ustadi sera ya serikali mbili kuelekea moja.
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mimi nadhani nyinyi WATANGANYIKA msiojitambuwa, baada ya kupiga makelele na kujadili mambo ya wazanzibari, mungejipanga kutafuta Tanganyika yenu na kulitupa, siyo kulivua,hilo gamba (CCM) lilokugandeni tokea uhuru, zanzibar wameshalivua nusu huku halina nguvu tena ya peke yake, ni suala la muda tu kulizikilia mbali, na nyie mungefanya hivyo msingekuwa hamjitambuwi hadi leo
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..Tanzania with or without Zanzibar ina athari gani kwa Mtanganyika?

  ..wa-Zenj kama hamuutaki muungano ni bora mkajitoa wenyewe, msisubiri wa-Tanganyika wazinduke.

  ..wa-Tanganyika tuna matatizo yetu mengi ya kujadili na kukabiliana nayo, muungano is not a priority at this time.

  ..kauli kwamba tusipojadili matatizo ya muungano yanaweza kutokea ya Sudan ni vitisho visivyo na msingi.

  ..kwanini tuelekee kwenye machafuko wakati Zanzibar wana vyombo[serikali,baraza la wawakilishi,baraza la mapinduzi,mahakama] vyenye mamlaka ya kuwaondoa kwenye muungano bila machafuko?

  ..nani amewazuia viongozi wa Zanzibar walioko kwenye serikali ya muungano, wawakilishi wa Zanzibar ktk bunge la muungano,pamoja na wa-Zanzibar wenye makazi yao huku Tanganyika, kurudi kwao Zanzibar na kutangaza ukomo wa muungano wetu?

  ..
   
 16. m

  mubi JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Tatizo siyo Muungano, Tatizo kubwa ni Katiba mbovu, inafavour Watawala hata wakiiba wanapewa muda wakujipima wakati wananchi wako hoi kwelikweli. Rasilimali zote zinaliwa na wachache tu, angalia madini, utalii, samaki wa ziwani, misitu yetu wanfaidi watawala tu. Zanzibar wanahofu ya maliasili zao hasa mafuta. Wasipochangamka itakuwa kama mikoa ya ziwani madini wanafaidi watawala, wenye nchi hoi na njaa kali.Katiba iliyopo imepitwa na wakati. Naamini kabisa kama katiba ingekuwa bomba hakuna hat Mzanzibari mmoja angelalamika. Mimi ni Mtanzania lakini nikiangalia policy ya uwekezaji ya madini na ya energy ni mbovu sana tu.Kwanza sioni haja ya wawekezaji. Mwisho Watanzania tuache uvivu na ubinafsi, uroho, uchoyo na technical know who. Nyerere alisema kazi ndiyo msing wa maendeleo, lakini Watanzania wengi tunapenda dezo, hatutaki kufanyakazi kwa ufasaha tunapenda kazi za kulipua na malipo juu. Government expenditure ni kubwa sana kazi iliyofanywa na government inakuwa hailingani kabisa na kiwango cha pesa iliyotolewa. Kwa maana nyingine hakuna standards za kupima malipo ya kazi hiyo. Kuna mapungufu mengi sana ndani ya Katiba yetu ndiyo maana Viongozi wetu wanacheza na sheria kama vile mtu yeyote anayekwenda holidays kuogelea kwenye the most beautiful beaches in the world. Katiba yetu ni maji yakuogelea, imefika sasa tuifanye iwe moto mkali wa kuogopewa hapo maendeleo yatakuja.
   
 17. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nadhani mtoa maada amesahau siasa za kitanganyika.Zanzibar tuna serekali yetu ? Au umekusudia ile inayochaguliwa na Tanganyika huko Dodoma ?

  Ukishaweza pata jibu juu ya serekali ya Zanzibar inachaguliwa wapi na akina nani huwafanyia maamuzi wazanzibari juu ya rais wao (kwa sasa anaitwa Dr.Shein alichaguliwa na Kikwete pamoja na mafisadi wenzake....maana waonekana kutofahamu kabisa kinachoendelea)....
   
 18. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  By the way, hilo la siasa kuwa sehemu ya muungano pia ni moja ya kero za muungano....ooops I forgot muungano wenyewe ndio kero!
   
 19. kalamata

  kalamata Senior Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pharao
  Tuombe radhi wa-zanzibari
   
Loading...