Ndugu zangu wananitenga

Heci

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
3,866
Reaction score
6,884
Tumezaliwa watatu wa kwanza ni wa kiume, wa pili mimi na watatu ni wa kike hawa wawili wananitenga na kunibagua hawanithamini wala kunijali kananiita hopeless huyu kaka yetu hana kazi na mimi sina kazi.

Huyu kaka yetu anasomeshewa watoto wake wote watatu, mimi ninaye mmoja, kwa sasa yuko nyumbani kisa sina ada niliona msaada kwa mdogo wangu ananijibu kirahisi kuwa ana madeni mengi ya kuyalipia najisikia vibaya kutengwa na ndugu zangu ila naamini Mungu hajanitenga.
 
Huna tofauti na nchi nyingi za kiafrika unaonekana bila msaada bajeti haikidhi mahitaji yako.
Amka pambana na hali yako
 
wewe mwenyewe inaelekea unajinyanyapaa umeweka kichwani kuwa hujiwezi mpaka usaidiwe kweli WEWE NI HOPELESS Kwani wewe ni mlemavu mpaka usaidiwe kulea mwanao?
Asante kwa maoni yako
 
hamisha mtoto mpele serikalini mkuu kupunguza gharama...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…