Ndugu zangu nisaidieni ujanja ili nitambue dhahabu halisi na feki

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,033
173,724
Morning Fam,

Kimsingi licha ya exposure katika mambo mengi tu yakiwamo mahusiano, magari, fashions na teknolojia nikiri tu kuna maswala mengine niko katika ujima.

Hivi karibuni nimekumbwa na kipengele, nataka nikanunue Gold jewelleries zikiwemo hereni, chain na pete ila sasa kimsingi sijui whats the difference between a real Gold and fake chain. Japo najua composition yake inapimwa kwa Karats kuanzia 12 mpaka 24.

Msaada kwa ambaye ni mzoefu wa haya mambo hasa warembo na washua wa humu JF! Maybe store ambayo ni genuine kwa kuuza hayo mavitu maana nimeenda City Mall pale nikakagua mali kwenye jewellery stores 2 ila still nna maseke.

Pia bei ya gold imesimamaje per gram sababu kuna ambao wanauza 175K per gram kwa 18 karats na wengine ni 190k kwa 21 karats. Katika story niliwahi kusikiaga gold ni 150k per gram.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom