Ndugu zangu arumeru ilikuwa vita! 2015 tunaingi ikulu ila lazima tufanye kazi

Bolivar

JF-Expert Member
Oct 23, 2010
229
103
Uchaguzi ni vita! Kupata ridhaa ya kuwaongoza/kuwawakilisha watu ni mchakoto mrefu. Hatoshi pekee kuuza sera na kukubalika, haitoshi pekee kupigiwa kura la hasha! Siku mbili nilizokesha na makamanda wengine katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki na kipindi chote cha kampeni nimejifunza mengi.


Ili kushinda uchaguzi unahitaji
1. Kuwashawishi watu wakubaliane na Sera zako
2. Kuwahamasisha watoke kukupigia kura
3. Uwezo wa kuwa na mawakala makini kulinda kura zako vituoni.

MUHIMU ZAIDI: Kusoma mbinu chafu za adui yako na kuchukua hatua stahiki mapema.

Mengi yamejiri kuelekea uchaguzi wa jana A. mashariki, siwezi kueleza mengi kwani ntaweka hadharani mambo yasiyostahili kuwekwa hadharani lakini somo kubwa nililopata ni kuwa kuishida CCM usisinzie hata kidogo, usipepese macho. CCM ni bingwa wa mbinu zote chafu za kuiba uchaguzi, sifikiri kama kuna chama duniani kilichojikusanyia uzoefu wa kuiba chaguzi kama CCM, hakuna. Kuanzia vituo feki, kununua shahada, kuhonga mawakala wa vyama pinzani wasitokee vituoni, na hata wakala mwaminifu, akisinzia kwa sekunde 10 tu wanafanya madhara makubwa kabisa. Hizo kura alfu ishirini na sita plus sio kura halisi, CCM isingefika kura alfu ishirini.

CCM ilifanya mengi na kuna baadhi ya sehemu ilifanikiwa lakini niwapongeze viongozi wa CDM kwa kubani mbinu chafu za CCM na kuchukua hatua za haraka kurekebisha hali kila mara.

Ni rahisi kubweteka na kushangilia ushindi, there is a bigger prize ahead! IKULU 2015 lakini sharti tufanye kazi kufa na kupona, haitakuja hivi hivi tu. Nilichojifunza wakati wa kampeni ni kuwa CDM ina washabiki na wapenzi wengi lakini ina wanachama wachache. Ili kuingia ikulu sharti CDM iwageuze washabi na wapenzi hawa kuwa wanachama! CDM ikifanikiwa kugeuza nusu tu ya wapenzi wake kuwa wanachama haitakosa walau wanachama milioni saba. Wanachama hawa wasichukuliwe kwa staili ya kugawa kadi kwenye mikutano, la hasha! Wanachama hawa sharti watokane na matawi yaliyopo mahala wanapoishi, wanachama hawa sharti wapewe mafunzo ya awali kuelewa chama kinasimamia nini na majukumu yao kama wana CDM. Viongozi wa matawi sharti wajue wana wanachama wangapi na idadi gani ya wanachama hao wana vitambulisho vya kupigia kura. Viongozi wapewe jukumu la kuhakikisha utakapofika muda wa kujiandikisha kupiga kura wanachama wasio na vitambulisho wanajiandikisha na wale waliojiandikisha sehemu nyingine wanabadili vituo ili waweze kupiga kura kwenye uchaguzi wa 2015. Utaratibu uandaliwe wa kuhakikisha siku ya kupiga kura wanachama wanafuatiliana kuhakikisha WOTE WANAPIGA KURA!

Hili likifanyika 2015 tunaingia Ikulu not for the sake ya kwenda Ikulu but kuleta mabadiliko watakayohakikisha rasilimali za nchi hii zinawanufaisha Watanzania wote, kuanza upya safari ya maendeleo ya kweli kwa Taifa hili, kujenga misingi itakayohakikisha tunatoka dunia ya tatu kuelekea ya pili, na vizazi vinne au vitano vijavyo viishi kwenye Tanzania iliyo dunia ya kwanza.

Nitaendelea Makomredi wenzangu
 
Shukrani mkuu kwa taarifa, lakini poleni nyote kwa kazi kubwa na ngumu mliyofanya. Endelea kutujuza mbinu mbali*2 na uzoefu wako kwa manufaa ya wazalendo wa kweli wa nchi hii.
 
amini usiamini kuna msemo kwenye jeshi unasema. MAZOZI NI MAANDALIZI YA MAPAMABNO NA MAPAMBANO NI MWENDELEZO WA MAZOEZI. tuendelee kupambana wajameni.
 
Nimeipenda sana hii analysis na ulichokisema ndicho kinachotakiwa kifanyike kuanzia sasa. Viongozi wa CHADEMA waweke watu maalum katka kila miji, manispaa, halmashauri, vitongoji na vijiji kukusanya taarifa za wanachama wa CDM. Wateule watakaoteuliwa kuendesha zoezi hili la ukusanyaji wa taarifa za wanachama wa CDM pamoja na kukaribisa wanachama wapya wapewe mafunzo na kisha kujitolea kufanya zoezi hilo. Naamini kwa kupitia utaratibu wa sasa wa kukichangia chama, wananchi wako tayari kukichangia chama kwa ajili ya kuendeshea zoezi hili. Watumishi wengi wa serikali naamin wako tayari kukichangia chama ili mradi kuwe na usiri wa hali ya juu kwamba kusijulikane nani kachangia nini.
 
Ccm ni mabingwa kweli kwa kuchakachua, hilo halina ubishi. Maana pia wanahusisha vyombo vya dola na tume yenyewe ya uchaguzi. So far tume ya uchsguzi si huru bado. Mabadiliko makubwa ni lazima pia yafanyike kwenye katiba mpya.
 
Nimevutiwa na jinsi wabunge wa CDM wanavyopiga kazi kama timu. Kikubwa zaidi ni jinsi watu walivyojitoa kusaidi toka majimbo jirani ya Moshi na Arusha. Watu waliamshwa saa nane usiku bila shida wakaingia kazini tena kwa gharama zao!

A strong point mkuu, tufanye kazi ikulu yetu 2015
 
Siku CCM itakapotoka madarakani ndio siku safari ya maendeleo kwa Taifa la Tanzania itakapoanza...
Angalia maendeleo ya Taifa hili kabla ya uhuru,miaka michache baada ya uhuru na sasa miaka 50 baada ya uhuru,je tulipokuwepo ni hapa tulipo?
Hivi uanafahamu nafasi ya Taifa hili kimaendeleo ilikua ya ngapi Afrika na duniani kwa ujumla?
Taifa hili limeharibiwa na Serikali ya TANU/CCM(viongozi wake wanategemea nguvu za giza,matambiko na makafara ili kuingia madaakani) pamoja na sisi Watanzania kwa kuwapa dhamana watu wasiostahili na huku tunatambua hawastahili...
Kama ni uzoefu wa kupiga kura tayari tunao,nchi imeshaingia kwenye chaguzi kubwa mara nne lakini bado matokeo yamekuwa ni ya kufedhehesha maana bado dhamana ya Taifa tunawapa walewale wenye kutunyonya,kutuibia na wazandiki.

"CCM waachieni Watanzania wamue hatma ya Taifa na Nchi yao, hamna jipya."
 
Back
Top Bottom