Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,101
- 34,916
MUUGUZI wa Kituo cha Afya cha Buguruni wilayani Ilala, Dar es Salaam amefariki katika ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwake ambayo hata hivyo, imesababisha mfarakano baina ya familia yake na ya mumewe kutokana na kile wanachodai kuwa limegubikwa na utata.
Rosemary Munseri (38) alifariki jana saa 11 alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuungua na moto nyumbani kwake, Yombo Limboa. Ndugu zake wanadai tukio hilo la moto la juzi, limezingirwa na utata huku wakidai kwamba mumewe anahusika.
Kutokana na tukio hilo, ndugu hao wamesusa msiba kwa mume na badala yake, wameweka msiba nyumbani kwa baba mdogo wake, Fred Munseri, eneo la Ubungo Maziwa, Dar es Salaam.
Taarifa kutoka msibani hapo zilidai kwamba mume huyo, Denis Mlazi, ambaye ni Mchungaji wa Kanisa moja Dar es Salaam anashikiliwa na polisi. Hata hivyo, gazeti hili liliwasiliana na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuthibitisha hilo, akaelekeza atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Polisi Temeke.
Simu ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabas, haikupatikana. Lakini katika kufuatilia zaidi, mmoja wa maofisa wa polisi ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa siyo msemaji, alisema taarifa zilizopo ni kwamba tukio hilo la moto ni la kawaida.
Hiyo taarifa sina, akimaanisha la mume kumuua mkewe kwa kumchoma moto. Ila tunachojua ni kwamba kuna tukio la moto lilitokea Yombo. Nyumba imeungua. Na ni ajali ya kawaida, na kwamba mtu huyo alikufa wakati akiokoa mali kwenye nyumba, alisema ofisa huyo na kusisitiza kuwa mume huyo hakumuua mkewe.
Kwa mujibu wa ofisa huyo ambaye alisisitiza gazeti hili limtafute Kamanda wa Temeke athibitishe, alisema ingawa hana taarifa za kushikiliwa mume huyo, lakini ikitokea hivyo, atakuwa anashikiliwa kwa sababu za kiusalama kwa kuzingatia hisia za ndugu wa mke zilizojengeka.
Hadi tunakwenda mtamboni, Kamanda Sabas hakupatikana ingawa taarifa zilidai polisi walishafungua jalada la jinai na kwamba ndugu wa marehemu, wameambiwa waendelee na taratibu za maziko.
Kwa upande wa mwanamume, dada yake aliyetambuliwa kwa jina moja la Herieth, alipopigiwa simu na gazeti hili kutaka kupata usahihi wa madai kwamba kaka yake ameshikiliwa na polisi, alijibu kwa mkato kuwa, mimi siyo msemaji wa familia.
Kulingana na madai ya ndugu wa marehemu, wanadai kwamba ndugu yao kabla ya kufariki, alielezea moto ulivyotokea na kubaini kwamba mazingira yanaonesha kuwa mume amehusika.
Alisema moto ulikuwa mkubwa sana. Na kwa kauli yake, alisema kabla ya kulala, alihisi harufu ya petroli. Lakini zaidi, majirani ndiyo walimpeleka hospitali, mumewe alibaki nyumbani akidai anazima moto, alidai Geraz Marcel ambaye ni mdogo wa marehemu. Walidai kuwa aliwaambia kwamba alishtuka muda mfupi baada ya kulala kukuta moto mkubwa ukiwaka kutoka kwenye godoro.
Alisema hakuwa na uwezo wa kujiokoa na akasema mume wake alikuwa sebuleni akifanya kazi kwenye kompyuta, alidai mdogo wa marehemu ambaye hakutaka jina litajwe huku akisisitiza kwamba mazingira na historia ya uhusiano wao ndivyo vinawashawishi waone anahusika.
Mfanyakazi mwenzake na muuguzi huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema katika mazungumzo kazini, Rosemary alikuwa akibainisha matatizo ya kifamilia aliyo nayo nao wakawa wanampa moyo.
Ndugu wengine waliozungumza msibani hapo, walidai wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu ambao chanzo chake, ni kutokana na mke huyo kukaa muda mrefu bila kuzaa. Lakini baadaye, alipata mtoto ambaye ana umri wa miaka mitano sasa.
Kwa upande wa baba yake mdogo, Gratian Mutashobya, alisema, ugomvi wa Rose na mumewe nimesuluhisha mpaka nimechoka. Mama wa marehemu, Ameria Kazimili (57) alisema mwanawe alikuwa akilalamika kuhusu uhusiano mbaya aliona nao na mumewe.
Tukawa tunasema tumuombee mimi kama mama, mtoto wangu wa kwanza nataka nimzike mwenyewe, alisema mama huyo. Hata hivyo, baadhi ya wanafamilia, waliliambia gazeti hili kwamba katika kikao walichokifanya, waliamua iwapo mume wake ataamua kuomba mwili wa mkewe auzike, watampatia kwa kuwa alikuwa mke halali.
Chanzo: HabariLeo