Ndugu wa mume wanataman kuniua nmuache mtoto wao

mmoja wenu akimua kufata dini ya mwenzake ili kufunga watu midomo kuna tatzo?
 
tafuta mganga mzuri wa kienyeji uwaloge wasikanyage kwako tena. Nenda bagamoyo.

Uwiii usiende kwa mganga wala msoma ramli mwaya tena ukiwa hivyo utapandikiza maroho hadi kwa kiumbe chako loo wasikitoe kafara tuuu.... mi namjua mmoja tu wala hupandi gari ni Yesu ...jamani amini usiaminii kuna maombi ukiyafanya hakuna mtu ataingilia ndoa yenu .dini zenu sio tatizo Mungu alikuwa na makusudi kuwakutanisha mayb siku 1 utamkiri kristo na atakuokoa na shida zote.Mimi mbona niliwahamisha wakwe zangu kwa maombi lol..Yesu anafanya ukiomba hapohapo ulipo ila inakubidi umkiri kwanza,,,najua wengi mtaona nyotanyota tuuu
 
ondoka au subiri ufe ndo hiyo akili itakaa sawa huko mbele kwa mbele!

Na wewe! Aondoke ende wapi? Angekuwa dada yako anakujia na kichuguu we ungemwelewa? Acha hizo mkuu!
Mimi nafikiri waliopendana ni wawili tu hapa. Hakuna cha wifi wala mjomba! Hakuna cha mama wala babu! Wawili tu hawa wakiamua kuishi watadumu katika ndoa yao! Wakiamua kuachana ni wao hao wawili. Hata kama hao wakwe na mawifi wangekupenda namna gani mume akikukataa huna chako. So shukuru kuwa naye mume anakupenda na wewe unampenda! Achaneni nao jengeni maisha yenu kwa mstakabali wa huyo mtarajiwa ndani ya hii miezi 3 iliyobakia. Katika mapendi sikilizeni miyoyo yenu na wala msitegemee nguvu za kutoka nje yenu. Ni nyie wawili tu. Hii huitwa milima na mabonde. Mtakutana navyo vingi tu ila tu ni kukabiliana navyo na zaidi mumwombe Mungu awape moyo na ujasiri wa kuvuka hivi vikwazo.
 
niondoke ntaenda wap na hali hii..napia nkiondoka nadhan ntakua nmepoteza nguv zangu bure mana nmejtahd kujijenga kmaisha na mume wangu...>magnificient

basi vumilia ndugu,we umesema wanataka kukuua ndo maana nikakwambia uondoke dadangu,kwa hyo kwako ni bora kufa kuliko kuondoka?
 
kama wanaona ndoa ni dini si angefunga na kanisa?achana nao,as long as your husb loves,wat then?wapotezee tu na lea mimba yako,waongee mwisho watachoka
 
pole dear
usiwajali hao nyie endeleeni kupendana mawifi/mamkwe hawaishagi maneno hata mngekuwa dini moja wangetafuta jambo
lea mimba yako bila wasi, usiwe na mazoe sana nao wakifika kwako salam ya kawaida endelea na shughuli zako
 
Huenda wanadhani au kusikia kuwa wewe unatokea m...............e! Na hivi huenda hiyo mimba yako ni ya mtoto wa kiume hivyo wanchelea kutupia mchnga kunako kaburi la mwanawe/kaka yao miaka kama kumi ijayo from now!
 
mambo haya rd ndodi anayapigia kelele sana. fahamu kuwa ndoa inahusisha ndugu pia
 
Huyo mume ajifunze kuweka 'mipaka yake'
ili ndugu zake waheshimu na kutomuingilia....
Ajifunze kuwa 'mwanaume'
 
wewe ndo mwenye ndoa. Vumilia. Kwa nini uwape nafasi ya kukuharibia? Meanwhile mwambie mumeo adili nd ndg zake
 
Nlijarbu kuondoka kwangu na walfurah sana ndugu zake na mama ake lakn ilikua adhabu kwa mume wangu...alikonda kwa mawazo na alnsihi nirud nlee mimba yake...ckua na jns nlirud kwa mume na walpockia nmerud ndo kama nlipalilia moto kwao...>magnificient

jaribu kubadili dini kama ndo tatizo,honestly hata mimi siwez kumuoa muislam hata siku moja,nitatengwa na ukoo mzima,nitakimbilia wapi nikija kupata matatizo kwenye hyo ndoa?

Akili yako+tathmini yakinifu-hisia na msisimko wa mapenzi=suluhisho la tatizo lako.
 
hata nkbadil itakua yaleyale mana nlijarbu kumwambia mume wangu bas nbadil dn labda ntapumua ila alnsihi nibak na dn nlozaliwa nayo...najuta kuwajua hawa watu jaman
 
KWa nilivyoelewa ni kuwa huyu ni mumeo halali, yaani mumefunga ndoa inayotambulika. Swali langu je ina maana wazazi wa mume hawakuiafiki ndoa yenu? Au mmechukuana tu mnaishi pamoja??

yaelekea wanaishi tu bila ndoa maana sidhani kama wazazi waliowahi kuafiki ndoa hapo awali wanaweza ghafla wakabadilika kwa hatua ya kutaka kumuua!! kwa kuwa ndoa kafungu na mume 1 basi aangalie uhusiano wake na huyo mume 1. ingekuwa amefunga na ukoo mzima hapo ndio ingekuwa mtafaruku, otherwise sion i tatizo kubwa hapo
 
Back
Top Bottom