Ndugu wa mume wanataman kuniua nmuache mtoto wao

moyo wangu

Member
Nov 18, 2011
59
13
Hope wazima nyote....Mm ni msichana mwenye 24yrz...nina miaka mitano toka Mungu aliponkutanisha na mume wangu kipenzi, mpaka sasa naishi na mume wangu lakini mimi nae dini tofauti.

Mimi muislam na yeye mkrsto....hapo ndo tatzo lilipo mana famlia nzima ya mume wangu wananichukia kupita kiasi sina aman na mume wangu hata kdogo. Nimevumilia mpaka nimechoka na kumwacha mume wangu siwez maana ananipenda na kunijali kwa kila kitu.

Ni yeye anaenipa moyo kuhusu kero na maneno na visa vya ndugu zake...sijui ni mimi peke yangu ndo niliye na matatzo na ndugu wa mume wangu au ni ndoa zote...

Kwetu wananishauri ndoa niiache na kila niktaka kumwambia mume wangu anipe talaka nashndwa maana nampenda naye ananipenda na kibaya zaidi kwa sasa nina mimba ya miez 6 na inanitesa sana,..

iIa wifi na mama mkwe ndo wanazidi kuniandama wanataka mimba itoke...wanasema hawanitambui.....nimevumilia sana na kumwacha mume wangu siwez na ndugu wa mume wanatamani kuniua...

Sijui nifanye nini.
 
Duh, umri wako unaelezea yote afu mimba huwa zinaleta mawenge kichwani, waweza lia kwa kunyimwa hata Big G.
Inawezekana hormone fluctuations inachangia wewe kukuza tatizo. HOLD ON, hadi ujifungue ndio uanze kutathmini hili jambo.

Mwisho wa siku hujaolewa na familia, umeolewa na mumeo.

Kwa kuwa ni mjamzito nimekuelewa otherwise!
 
Well kama mume ye hasikilizi maneno ya nduguze na wewe hutaki muachane hamieni mbali na hao ndugu muishi maisha yenu kwa amani!!
 
Najarbu sana kujkontroo.....>kongosho


naish nao mbali lakn haina msaada kwangu..mana wananfata mpaka kwangu...>lizy
 
ww tu unawaendekeza mawif zako..kwn ukiwaambia hata ww huwapend watimue kwako na ww usiende kwao na mmeo kama hawez kuwakataza nduguze wa kike kuingilia ndoa yake mwambie awaoe dadazake wawe wake wenzako ujue moja
 
Bibi weeeeeeeee Mama mkwe+Mawifi hawa watu ni mapacha dawa yao ni kuwapotezea kikubwa umesha gundua mumeo anakupenda tulia tuli, wakija wakilianzisha wachambe tu hao hawana wema
 
Ndoa ni yakwako na mmeo na si hao wavimba macho,
Chakufanya wala usiwaendekeze,wapotezee na endelea na maisha yako,
Kwao usiende,wakija kwako tafuta safari ondoka,
Hao wanakusumbua coz wanaona wanayokufanyia ulalamika na kulia lia,
Wakiona huwajali na maneno yao na huoneshi kukerwa nao wananyamaza wenyewe!
Huwezi acha ndoa yako kwa maneno na vituko vya ndugu wa mume ile hali mmeo anakupenda mnapendana,ni ujinga!
 
wewe angalia afya yako,
kwa mawazo haya hiyo mimba itatoka
na watasema umeamua kutoa mimba
achana nao, wewe si ndo umeolewa kama walimtamani mwanawao/kaka yao
si wangeolewa wao, ala achana nao.
 
Endelea kujaribu hadi ujifungue, tulia ivo ivo kama unanyolewa hadi miezi tisa. Tulia tu usijitingishe hata kidogo, sasa mdogo wangu?!

Najarbu sana kujkontroo.....>kongosho


naish nao mbali lakn haina msaada kwangu..mana wananfata mpaka kwangu...>lizy
 
Kwa hiyo inaonekana ndoa mlifunga bomani sio?Usijali.Ni wanawake wachache sana ambao hukubalika na ndugu wa mume.Jione kwamba hauko peke yako katika tatizo hilo maana ni la kawaida sana,then potezea.
 
niondoke ntaenda wap na hali hii..napia nkiondoka nadhan ntakua nmepoteza nguv zangu bure mana nmejtahd kujijenga kmaisha na mume wangu...>magnificient
 
kama ningekua wewe wala singeumia hata tone!
ati mume ananipenda mume hanipendi!!??
hiyo ni juu yao
naziba maskio......wasemeeeeeeeeeeeeeeee
mie kimya!!!!!!!!!!!!
salam nitawapa kama watapokea sawa wakigoma pia sawa tu
 
KWa nilivyoelewa ni kuwa huyu ni mumeo halali, yaani mumefunga ndoa inayotambulika. Swali langu je ina maana wazazi wa mume hawakuiafiki ndoa yenu? Au mmechukuana tu mnaishi pamoja??
 
Back
Top Bottom