Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Saaly

Senior Member
Feb 17, 2022
102
129
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.

Pia soma: Mrejesho: Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo
 
Mfanyie suprise Kama yule jamaa wa Kenya alivyofanyiwa na mke wake pamoja na michepuko yake!,jitahidini azimie asipozimia imekula kwenu na hakikisheni anazimia kwelikweli sio kuzimia kwa furaha kwa fumanizi mliyomfanyia..😁
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

a mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Mrudishie vitu vyake muombe muachane.

Akianza kuwa mkorofi na hapo atakuwa anayatafuta.
 
Ujengewe nyumba
Gari ununuliwe..
Kazi nzuri utafutiwe ..


Halafu unasema anaku suffocate?

Tukusaidie umuache vipi?

Huyo Kijana umemwambia kuhusu kodi?


Why usirudishe nyumba na gari kwanza uone huyo Kijana mpya atakupenda vipi?

Ukiuliwa wala usimlaumu mtu
Huna akili
 
Hapo tunasema you are between a rock and a hard place. Kuna mawili.

Either uamue kuendelea kuishi kama mtumwa wa mapenzi na mume wa mtu and waste your life.

Au uhame mji ubadili namba za simu, kurasa za mitandao ya kijamii na uanze maisha mapya na huyo mpenzi wako.

Using'ang'anie mali aliyokupa. Freedom is more expensive.
 
Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua.
Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana.
Gunia 4 za mkaa zinakuhusu wewe

PS. Kaa nae umueleze ukweli juu ya maamuzi yako na sio uamue tu kumuacha. Najua unahofia anaweza kukunyanganya materials alizokupa! Bora umwambie kuhusu future yako ili yeye aamue kukuacha na achukue mali au akuachie AU akufanye mke wa pili....Wengi tu wameolewa na watu wasiowapenda

Hayo ndio madhara ya kumpenda mtu kutokana na Status/materials aliyonayo na sio kutoka ndani ya Roho yako🚶🚶🚶
 
Lete Maneno Tuone Kama Ingekuwa Mleta Mada Ndiyo Dume Ungekubali
Gari Ina Thamani Ya Millions Ngapi?
Nyumba Thamani Yake
Umetafutiwa Kazi
Unawekewa Gari Mafuta

MAGAZIJUTO,


JK Alisema!! Oops Mlisema Sichomoi Kwani Nilichomeka Wapi?
 
Back
Top Bottom