Ndugu wa marehemu, Muhimbili walumbana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu wa marehemu, Muhimbili walumbana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 31, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeingia katika mgogoro mkubwa na ndugu wa marehemu, Scolastika Rwambo, baada ya ndugu hao, kudai kuwa marehemu alikufa kutoka na kusahaulika tumboni mwake mkasi uliotumika kumfanyia upasuaji.


  Madai ya ndugu hao wa marehemu, yanafuatia maelezo ya uongozi wa hospitali hiyo kuwa kifo cha marehemu kimetokana na matatizo mengine ya tumbo na si kusahaulika kwa mkasi kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa Hospitalini ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema kuwa uchunguzi wa kina ulibainia kuwa hakukua na mkasi tumboni mwa marehemu.

  Alisema marehemu alikuwa na ugonjwa mwingine unaowakumba wanawake ambao hata hivyo, hakutaka kuutaja.

  “Marehemu Scolastika aliletwa hapa Desemba 27 mwaka huu na kulazwa katika wodi ya Kibasila namba tisa akilalamikia maumivu ya tumbo. Uchunguzi ulifanyika na hatimaye kubaini kuwa alikuwa na tatizo lingine la tumbo lililojitokeza na hivyo kumfanyia upasuaji tena,”alisema Aligaesha

  Alidai kuwa tatizo ambalo madaktari waliligundua kwa marehemu kabla ya upasuaji, haliwezi kutajwa kwa sababu ni siri baina ya daktari na mgonjwa.

  “Kutaja ugonjwa ni sawa na kumdhalilisha mgonjwa ila jueni kuwa alikuwa na tatizo la tumbo ambalo ni magonjwa ya wanawake hivyo ikalazimika kufanyiwa tena upasuaji,”alisema Aligaesha

  Hata hivyo kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Peter Rwambo, alikuja juu na kudai kuwa alikuwa na marehemu tangu anaumwa na alipofanyiwa uchunguzi kwa mara ya pili alionekana kuwa na mkasi tumboni.

  “Alipopigwa picha ya x-ray kwa macho yangu niliuona mkasi na daktari akaniuliza nina mpango gani na huo mkasi, nikamwambia maisha ya mdogo wangu namuachia Mungu iweje leo niambiwe hakuwa na mkasi,”alisema Rwambo
  Kaka huyo wa marehemu alisema tangu ndugu yao alipopigwa picha hiyo ya x-ray madaktari wamekuwa wakimzungusha kumpatia picha hiyo wakati ni mali ya mgonjwa wake.

  “Baada ya kuonyeshwa majibu katika chumba cha x-ray na kuona mkasi madaktari wananizungusha kunipa picha hiyo nikae nayo kwanini wakati ni mali ya mgonjwa wangu na mimi ndio muuguzi wake wa karibu”alilalamika Rwambo.

  Kaka huyo wa marehemu aliendelea kudai kuwa tangu ndugu yao alipofanyiwa upasuaji hawakuruhusiwa kumuona na muda wote alikuwa amezungukwa na wauguzi hadi walipopewa taarifa kuwa amefariki dunia.
  Marehemu Scolastika alifariki Desemba 29, saa 1:05 jioni katika Hospitali yaTaifa Muhimbili, alikokuwa amelazwa kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwa mara ya pili.
   
 2. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kesha pigwa changa la macho hiyo X ray haipati tena, ushahidi kwishney.
  Ndo madaktari wetu hao, wanafanya operation wanafikiria kuwahi mechi ya chelsea na arsenal
   
Loading...