Ndugu upande wa baba walinikataa baada ya baba kufariki

Ndugu upande wa baba walinikataa baada ya baba kufariki

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,460
Habari wana Jamii Forums.

Nitalieleza hili tukio kwa nafsi ya kwanza ili kulijengea hisia zaidi.Ila ni ishu serious na huyu binti anahitaji msaada haswa tena ushauri wa busara.

"Naitwa Izza, mama yangu na baba yangu waliachana mimi nikiwa mdogo sana (kabla sijatimiza mwaka)!! Mama akaniacha kwa baba na kuondoka zake kusaka maisha kivingine. Kwa udogo niliokuwa nao baba alilazimika kuoa haraka haraka ili apate mtu wa kuweza kusaidiana nae kunitunza na vile alikuwa mfanyakazi.

Baada ya kuoa nashukuru Mungu mama huyu wa kambo si kama wanaohadithiwa na wengi, kwani alinilea vizuri sana. Na nasikitika baada ya miaka kadhaa nikiwa darasa la tano baba yangu alifariki ghafla. Nililazimika kubaki na mama wa kambo pamoja na wadogo zangu kadhaa aliozaa na baba.

Ajabu, mama wa kambo baada ya kuona baba amefariki alinipeleka kwa ndugu zangu aliwajua wa upande wa baba tu lakini hawakuwa tayari kuishi nami, kifupi walinikataa. Wakati huo huo wakijua mimi nitaendelea kuishi na mama huyu bado wakampora mali zote.

Na mama yangu mzazi alipewa taarifa za yaliyonikuta lakini hata hakujisumbua kuja kuniona au kunichukua. Nashukuru Mungu, huyu mama wa kambo kakomaa nami mpaka nimemaliza chuo, nimepata kazi. Ndugu zake ndiyo ndugu zangu hawajawahi kunibagua hata siku moja, ndugu wa upande wa baba baada ya kumpora mama mali walikata mguu na kuvunja undugu kabisa so, nimeishi na ndugu wa mama wa kambo tuu

Mungu hamtupi mja wake, nimefanikiwa kwa kweli nisiseme sana hasa kikipato na kimaisha kiasi cha kuyabadilisha maisha yetu kabisa! Mama yangu mzazi kumbuka sijawahi kumuona kabisa mimi, leo hii ananitafuta kwa simu kila leo na kuniita "mwanangu mpenzi".

Ndugu wa upande wa baba walionibagua leo wananitafuta na kuniambia mimi ni mtoto wao, niende nikawajue ndugu zangu wengine.Nikikumbuka nilivyoishi kwa upweke mkuu, roho inapata kutu hata kujuana nao hasa huyu mama mzazi!! Je kama ni wewe ungewatafuta kuonana nao au ungewapotezea.

Please, kama huna cha kuandika just leave it,nahitaji maoni ya walio serious thus why nimeandika kirefu kujitahidi kuelewesha."

Nawasilisha wana Jamii Forums
 
Mbona elimu yake ni kubwa sana! ameshindwaje kusolve tatizo kama hili kabla ya kulileta hapa?

Lete kwanza primary data kabla sijaenda mbali. Haya mambo yanayohusu familia unaweza kuonekana mchawi baadae kwa sababu ya ushauri tu!!!

Ajishauri kwanza kabla hajashauriwa!

Sibling matters are always complicated.
 
Kwanza pole kwa yaliyokufika,huyo mama yako wa kambo ndiye mama yako hasa,alikujali ulipokuwa huna kitu,mlihangaika naye,muheshimu mtunze watunze ndugu zako. Mama yako mzazi kaa naye mbali,ukitaka upate matatizo mkaribishe nina hakika ataharibu mfumo mzima wa maisha yako.Kwa nini aanze kujipendekeza wakati una mali na uwezo,wakati ulipokuwa unamhitaji hakuwa na habari na wewe? Kwa upande wa ndugu zake ndiyo kabisaa,waishie mali waliyokunyang"anya ya baba yako. Waulize hawakutosheka nayo na sasa wanataka ya kwako? Hao ni wauaji wapotezee
 
Kuna watu wana roho za paka, kama kweli alisikia kifo cha baba yako na matatizo uliyopata huyo hafai hata kwa ndimu.

Kukuacha kwa baba ukiwa na mwaka mmoja huwezi kulaumu kwa sababu labda alilazimishwa akuache na wewe ukaaminishwa vinginevyo. Kosa ni kuendelea kukuacha uhangaike wakati baba yako amefariki na ndugu wa baba wamekukataa, ukabaki kwa mama wa kambo.

Huyo mama wa kambo ndio mfanye mama yako mzazi na ni muda wake wa kula matunda yako. Mfanye asijutie kukulea kwa tabu, na kujibana na kuhangaika kukusomesha hadi kufanikiwa kama unavyosema, nae huu ndio muda wake wa kufurahi.

Huyo mama yako mzazi na hao ndugu wa baba yako waache kama walivyo.
 
ningekua mimi ni huyo dada dah!!!!!! sjui ingekuaje
 
mbona hayo yajibika kifamilia kabisa, baina yake na mama zake...
 
Mi naona kwnye ishu ya mama yako mzazi usimtumpe na wala usimuwekeee kinyongo uyo ni mama yako aliyekuzaa, asingekutaka angekupoteza ingali bado upo mdogo, ila alikuacha japo akuweza kukulea, ujue ni hali gani iliyompelekea mpaka kutoweza kuwa karibu nawe kipindi ulichomuhitaji kwa iyo haina haja kumlipizia, kwa upande wa ndugu wa baba zako uo ni uamuuzi wako kwa kuona mahitaji yao kwako ila husiwatupe jua malipo yako yapo kwa mola alokuwezesha, kwa mama yako alokulea apo akuna pa kusema ndo mtu wako wa karibu uyo..... ILA OMBI; MAMA YAKO MZAZI USIMTUPE NDO WAKO UYO HATA IWEJE, MAMA NI MAMA NA NDO MUNGU WA DUNIANI UYO.......
 
Pole kwa yaliyokukuta,
Huyo mama aliyekulea toka ukiwa chini ya mwaka mmoja hadi chuo na uko na kazi, usijesema si mama yako hata siku moja maana huyo ndiye mama yako. How is she different from our mother( kwa tuliolelewa na mama zetu )?

Usimkatae mama mzazi wala ndugu za baba yako. Just help them ila usikubali wakijaribu kukutenganisha na huyo mama na wadogo zako.
 
Akili kichwani mwako ndg! Kwangu mm ndg zangu wa kweli ni wale niliowajua tangu utotoni na nikakua nikiwaona na kuwajua! Ndg wa ukubwani tena kwasababu nimepata hela ya mboga wanisamehe tu kwa kweli.
 
Nosense ...MUNGU WA DUNIA!Acha kumtukuna MUNGU!Kama alimwacha bila kujali ustawi wake leo wa nini ! Kuna tofauti gani na nyoka amabaye halei watoto wake ! Dada endelea na Dunia yako na hao ndugu walio kujali ! Akija msalimie tu na usisiste kumwambia ukweli wa hisia zako ! Hao ndugu wengine ndio kabisa achana nao
Mi naona kwnye ishu ya mama yako mzazi usimtumpe na wala usimuwekeee kinyongo uyo ni mama yako aliyekuzaa, asingekutaka angekupoteza ingali bado upo mdogo, ila alikuacha japo akuweza kukulea, ujue ni hali gani iliyompelekea mpaka kutoweza kuwa karibu nawe kipindi ulichomuhitaji kwa iyo haina haja kumlipizia, kwa upande wa ndugu wa baba zako uo ni uamuuzi wako kwa kuona mahitaji yao kwako ila husiwatupe jua malipo yako yapo kwa mola alokuwezesha, kwa mama yako alokulea apo akuna pa kusema ndo mtu wako wa karibu uyo..... ILA OMBI; MAMA YAKO MZAZI USIMTUPE NDO WAKO UYO HATA IWEJE, MAMA NI MAMA NA NDO MUNGU WA DUNIANI UYO.......
 
Bahati mbaya sana mama yako mzazi atakuja kukuvuruga. Atataka ukosane na mama yako wa Kambo, It is unfortunate unatakiwa kufanya maamuzi magumu. Mifano ipo mimi namfahamu binti mmoja aliachwa akiwa mchanga kwa baba yake , nadhani ilikuwa hasira kwani huyo baba aliamua kumuoa mwanamke mwingine. Yule mototo ( binti) alinyonya na kaka yake, yaani walikuwa kama mapacha. Mama wa kambo alimlea kwa mapenzi yote km mutoto wake. Sumu iliinga punde mtoto alipomtambua mama yake mzazi amba akamtengasha totally na mama yake aliyemlea. Hivyo kuwa makini sana.
 
Huyo Mama wa kambo ndio kila kitu kwako kwani bila huyo usingekuwa hapo ulipo sasa, ila hao wanaojitokeza leo huku walikukana kabla wanataka kukuvurugia maisha yako tu kwani hawakuwa na msaada wowote kwako toka ulipokuwa mdogo ila sasa hivi wanataka kuvuruga mahusiano yako na mama yako mlezi.
KAA NAO MBALI ILA WASAMEHE KWA WALIYOKUTENDEA.
 
Ndugu yangu,huyo mama aliyekulea ndo mama yako,yeye alijua kuamka na kulala kwako toka ukiwa mdogo hadi umekuwa mkubwa,yeye ndiye amekuhangaikia toka ukiwa mdogo,kakusomesha na pia kukufundisha dunia hadi ulipofikia,hao ndugu zako wanaokutafuta sasa hivi pamoja na mama mzazi wala usijihangaishe nao,sana sana watataka kukuachanisha na huyo mama aliyekulea toka ukiwa mdogo maana wataona anafaidi matunda yako na labda unamjali yeye zaidi kuliko wao.Jiulize kama ungekuwa kapuku wangejihangaisha kukutafuta?la hasha,hivyo kaa nao mbali maana ni sumu katika maisha yako,jiepushe kumliza huyo Mama aliyekulea maana ndiye mama yako mzazi.
 
ushauri wangu mfupi sana.nenda kakae chini na mama wa kambo aliyekulea nacumuombe ushauri juu.kumbuka she was there from the beginning na anaelewa tote kwa undani kuliko kuuliza huku ambapo most of the people hawajapitia maisha uliyoishi
 
Huu ndo ushauri sasa,safi sana mkuu
 
mbona hayo yajibika kifamilia kabisa, baina yake na mama zake...

Simply yanajibika ila hebu vaa hivyo viatu wewe....!!! Kuna conflict kubwa sana ndani yake inafanya mtu anakonda
 
Bahati mbaya sana mama yako mzazi atakuja kukuvuruga. Atataka ukosane na mama yako wa Kambo, It is unfortunate unatakiwa kufanya maamuzi magumu. Mifano ipo mimi namfahamu binti mmoja aliachwa akiwa mchanga kwa baba yake , nadhani ilikuwa hasira kwani huyo baba aliamua kumuoa mwanamke mwingine. Yule mototo ( binti) alinyonya na kaka yake, yaani walikuwa kama mapacha. Mama wa kambo alimlea kwa mapenzi yote km mutoto wake. Sumu iliinga punde mtoto alipomtambua mama yake mzazi amba akamtengasha totally na mama yake aliyemlea. Hivyo kuwa makini sana.

Thank you sana, mambo ya family bana ni very complicated!
 
Wamama kama huyu aliyekulea mi huwaweka kwenye kundi la watakatifu. Shikamana naye Ligogoma na utayaona mema ya nchi kuliko unavyofikiria.
 
Last edited by a moderator:
Kisasi ni juu ya Mungu, Huwezi jua mipango ya Mungu kumtumia mama wa kambo kukulea na kukusomesha, inawezekana mama mzazi angekulea asingekusomesha, na usingekua hivyo ulivyo, mshukuru Mungu kwa yote, na uwasamehe waliokukosea ila uishi nao kwa akili.
 
Back
Top Bottom