Uchaguzi 2020 Ndugu Polepole, Sera zetu za CCM kuna sehemu hazikidhi. Ukimshambulia Lissu utaharibu na kuvuruga mambo

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Mgombea Tundu Lisu ni Mtanzania kwa kuzaliwa na kuishi. Wewe Mh. Polepole nawe ni vivyo hivyo.

Tutamheshimu yeyote kwa kumwona Mzalendo pale tuu atakapokidhi matarajio yetu kwa vitendo na hata kwa ahadi katika kampeni zinazoendelea.

Sera za CCM zinalenga haki, uhuru na maendeleo ya Wanyonge.

Lakini, Lissu kasema:

1. Haki za wanyonge zinanyongwa kwa kuporwa ardhi na kutozwa vitambulisho na mifano mingi katoa.

2. Hawana uhuru wa kudai haki kwa vile nguvu kubwa inatumika kuwazima mfano Wakulima wa Korosho , wafanyakazi nk.
Hizo hoja zinaimpress jamii na wanaona ni kweli.

Badala ya kujibu hoja hizi kwenye vyombo vya habari, tuzijibu kwenye kampeni zetu.

Ninamshukuru M/kiti wetu alijibu baadhi akiwa kule Itigi akijinadi. Hii ni sawa,lakini je,majibu hayo yapo kwenye sera zetu? Je, watekelezaji wa sera zetu hawapindishi mambo? Mfano MaDcs, RCs, nk.

Kushinda tutashinda ila kuna mambo yanatakiwa yarekebishwe kisera na siyo majibizano kwenye vyombo ambavyo ni biased .
 
Yupo Dodoma kujieleza kwanini mipamgo waliyoipanga kwa gharama kubwa inaonekana kutokuzaa matunda.
 
Polepole na Bashiru sio comredi wa siasa

Kwa sera hizo hizo wanaume wa siasa wanatoboa
Sasa hoja ya kupandisha mishahara ya watumishi ya watumishi haihitaji maneno
Wewe tia hela kwenye account tu za watumishi

Swala la ajira sasa hapo we si unaajiri tu umemaliza

Sasa sijui wanakwama wapi
 
Umeona mbali na umetoa ushauri mzuri sana kwa chama chako, ila hio fikra ya kwamba kushinda mtashida you are wrong brother.
 
Ccm wamebaki kubebwa na dola tu, tume, polis na vyombo vya habari kila kukicha Live Massa yote, wenzao hawapewi.
 
Mgombea Tundu Lisu ni Mtanzania kwa kuzaliwa na kuishi. Wewe Mh. Polepole nawe ni vivyo hivyo.

Tutamheshimu yeyote kwa kumwona Mzalendo pale tuu atakapokidhi matarajio yetu kwa vitendo na hata kwa ahadi katika kampeni zinazoendelea.

Sera za CCM zinalenga haki, uhuru na maendeleo ya Wanyonge.

Lakini, Lissu kasema:

1. Haki za wanyonge zinanyongwa kwa kuporwa ardhi na kutozwa vitambulisho na mifano mingi katoa.

2. Hawana uhuru wa kudai haki kwa vile nguvu kubwa inatumika kuwazima mfano Wakulima wa Korosho , wafanyakazi nk.
Hizo hoja zinaimpress jamii na wanaona ni kweli.

Badala ya kujibu hoja hizi kwenye vyombo vya habari, tuzijibu kwenye kampeni zetu.

Ninamshukuru M/kiti wetu alijibu baadhi akiwa kule Itigi akijinadi. Hii ni sawa,lakini je,majibu hayo yapo kwenye sera zetu? Je, watekelezaji wa sera zetu hawapindishi mambo? Mfano MaDcs, RCs, nk.

Kushinda tutashinda ila kuna mambo yanatakiwa yarekebishwe kisera na siyo majibizano kwenye vyombo ambavyo ni biased .

CCM walijichelewesha wenyewe walipotoa katazo ya siasa za majukwani kwa vyama vya upinzani.kwani hoja zinzoibuliwa sasa na upinzani ni za msingi ,ila ccm kama chama dola imechelewa kuzisikia sababu ingekwisha kuzisikia mapema let say miaka mitano iliyo pita.wangekwisha kujua kiasi cha kiu ya kweli walionayo wanchi.

Ndiyo maana nasemaga vyama vya upinzani vingeachwa huru kwa sababu ni kama kipaza sauti chenye sauti za kweli kutoka kwa wanchi.Ndani ya ccm kuna hofu kubwa kiasi ukweli hausemwi ,wale wanaomshauri Raisi wanapima upepo wa Raisi kabla ya kumshauri.so mara nyingi wanamuaminisha uongo mtupu

Usije ukasahau hoja ya Elimu bure ilitolewa na chadema kwa kupitia Lowasa.

Sijui kama kuna mtu ambaye amewahi kujua ikiwa ni kweli moja ya mahitaji ya kimkakati ya Watanzania ni pamoja na Miundombinu ghari kiasi hicho.pengine kulikuwa na haja ya kuwekeza ku usawa katika mahitaji ya nchi.

Tunazungumzia Tanzania ni nchi yenye asilimia kubwa ya watu wanao tegemea kilimo,je tumewekeza kiasi gani huko?
 
Pole pole na bashiru eti ndo watunga sera wa kampeni angalau Ile ya kina kinana na nape
 
Back
Top Bottom