Ndugai kumfananisha CAG na 'Mbwa' ni tusi zaidi ya mtu kusema 'Bunge lina udhaifu' katika kuiwajibisha Serikali

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
6,062
10,461
Ndugai , spika wa Bunge la JMT, wakati wa press conference yake na waandishi habari jumapili tarehe 14/4/2019 amesikika akimuita Prof. Assad, CAG kuwa ni mbwa anayemng'ata mtu anayemlisha.

Hili ni tusi kubwa kuliko kutokuelewa kwake juu ya neno DHAIFU. Prof. Assad ni muislamu, kumuita mbwa kunaongeza uzito wa tusi.

Hivi, huyu spika Ndugai ana nini kichwani? Huku kutojua uzito wa maneno si pia kunadhihirisha hadharani UDHAIFU wake?

Hivi Prof. Assad akiamua kwenda mahakamani kufungua kesi ya kuchafuliwa jina/kutukanwa (defamation) dhidi ya spika atakuwa amekosea?
 
Ni muda sasa CAG aache kujibizana nae. Wananchi tushaelewa nani anasimamia maslahi ya taifa na nani mchumia tumbo.
Lengo lao akina Ndugai na huyo Jiwe anayemtuma, tushalielewa watanzania

Lengo lao ni kum-frustrate huyo CAG, ili aachie ngazi mwenyewe

Kwa kuwa wanajua hawana namna ya kumtoa kwa jinsi Katiba yà nchi inavyomuwekea kinga.

Na kwa kuwa tayari Jiwe ana "mkolomije" mwenzie aliyemuaandaa awe CAG mpya, ambaye atakuwa anamfichia wizi wake wa pesa ya walipa kodi wa nchi hii kwa matrillion ya shilingi........

Kwa hili amenoa, kwa kuwa CAG kagoma kabisa kung'oka, pengine wampyupyu!
 
Mambo ya kawaida tu kwenye siasa Hayo

Mbona kuna watu huitwa nyumbu na hamlalamiki?
Au nyumbu ni bora kuliko mbwa,tatizo profesa ameamua kuwa mwanasiasa anajibu kila neno hiyo haitakiwi hata kidogo kwa mtaalamu

God first
 
kwa Taifa CAG...M J.Assad ni ASSETS na kwa nchi Nduga boy ni Liabilities

na kama kamwita hivyo atambue kategua kitendawili cha UDHAIFU maana kwa desturi 'mdhaifu' hawezi kumpenda mbwa..

Kuna mbwa wanaonusa mabomu,madawa ya kulevya,kukamata wahalifu,kuzuia wezi majumbani,kufichua ubadhirifu.

MBWA wa sifa hizo hawezi kupendwa na mwenye nia ovu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya kawaida tu kwenye siasa Hayo

Mbona kuna watu huitwa nyumbu na hamlalamiki?
Au nyumbu ni bora kuliko mbwa,tatizo profesa ameamua kuwa mwanasiasa anajibu kila neno hiyo haitakiwi hata kidogo kwa mtaalamu

God first

Kwa nini Prof anajibu kila neno...????
Hiyo ni another technic ya kuifanya public kutowa judgement.
Fanya analysis kidogo tu,so far kwenye hili sakata ni nani aliyekwenda nje ya MENU....??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ndugai analifanya bunge kama ni mali yake....bunge ni wabunge..wabunge hajapiga kura kutofanya kaz na assad
 
Mambo ya kawaida tu kwenye siasa Hayo

Mbona kuna watu huitwa nyumbu na hamlalamiki?
Au nyumbu ni bora kuliko mbwa,tatizo profesa ameamua kuwa mwanasiasa anajibu kila neno hiyo haitakiwi hata kidogo kwa mtaalamu

God first
Kwa hivyo nikikwambia mama yako ni bitch (mbwa jike) na wewe ni son of a bitch itakuwa sijakosea?
 
Back
Top Bottom