Ndugai kama bunge vs Assad CAG na maoni ya wengi

Ndugai kama bunge vs Assad CAG na maoni ya wengi

Kayemba

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2013
Posts
221
Reaction score
175
Nimejaribu kufuatilia hotuba ya jana ya Spika wa Bunge nimetafakari kwa upeo wangu nikajiuliza maswali kadhaa na kujipa majibu mimi mwenyewe yakaishia kwangu kama mtazamo wa kile nilichokisikia.

Sikuishia hapo, nimejaribu kusikiliza na kusoma mitazamo ya wananchi ambao ndio waliowachagua akina Mh. Ndugai (nikimaanish Bunge), wengi wao naona wanatoa maoni ambayo yanakinzana sana na maamuzi ya bunge huku wengine wakidiriki kurudia kuliita Bunge lile neno ambalo Spika na wengine walioadhimia kutofanya kazi na CAG hawalipendi.

Sasa maswali ninayojiuliza ni haya:
1. Je Spika pamoja na watu wake hapitii mitandao ya kijamii ili kuona public views kwenye hili jambo?

2. Kama wanapitia, je hawatambui kwamba hao watoa maoni ni sample ya waliowachagua?

Ikumbukwe kuwa wabunge ni sisi wananchi ila tunawakilishwa na baadhi yetu.

Maendeleo hayana chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nime maoni ya mwananchi japo mmoja kutoka KONGWA
 
CAG apewe tuzo ya uadilifu katika kazi zake. hako kaneno kasitutoe kwenye mada kuu maana huwa tunalalamika tanzania tunaupungufu wa watu waadilifu kwenye kazi zao.
Kwangu mimi huyu ni mmoja wao. Maneno au sintofahamu ya neno'' dhaifu'' haibatilishi sifa njema alizo nazo.
Ikiwa anamabaya yawekwe wazi tuyachambue, ili uzuri wake usifyonzwe kwenye msamiati ''dhaifu''.
 
Kuna watu wanajua kusimamia kile wanachoamini hawayumbishwi.
 
Statistical evidence please

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimepiga kura miaka mingi nameneo tofauti tofauti niliyoishi, kiufupi asilimia kubwa ya wale wanaoongeaga sana au wanaojionaga wajanja hua hawapigi kura!!

Isipokua wale wanaoonekanaga siyo wajanja ndo wanaopiga sana kura, yaani kiufupi aslimia kubwa ya wapiga kura ni wale watu wa hali ya chini, hata ukiangalia kipindi cha kuandikisha vitambulisho vya wapiga kura utakuta wanaotii hayo maelekezo ni watu wa hali ya chini, na wakina mama wa hali ya chini, tena wakina mama wenye uwezo wana majivuno sana.
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako watu wa chini ambao wana "Udhaifu" fulani ndo wanaotuchagulia wabunge? Kama ni hivyo vipi kuhusu wanaochaguliwa na hilo kundi?

Tutumie mda kutafakari mantiki za yanayojiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wa Tz ni mabingwa kuandika mitandaoni but no reactions. Tuige hapa kidogo
IMG-20190411-WA0000.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom