East African
JF-Expert Member
- Nov 27, 2013
- 704
- 990
Habari za siku wadau wa jf
Bunge ni chombo huru na linapaswa kulindwa ili kiwe na nguvu ya kutetea maslahi ya wananchi na taifa bila kujali vyama vyao. Kiongozi Mkuu wa chombo hiki ni Spika akisaidiwa na Naibu Spika, ambapo kazi ya kiongozi wa Bunge ni kuwaongoza wabunge bila kujali vyama vyao.
Vyama ni kama njia tu ya kuwafikisha pale Bungeni hivyo ni vyema kuongoza chombo hiki kwa maslahi ya taifa lote. Kutokana na sintofahamu na mgongano unaoendelea kujitikeza ningemshauri ndugu Spika Ngugai akae chini na uongozi wa Bunge na kutafuta suluhu ili chombo hiki kiendelee kuaminiwa kama ilivyokuwa enzi ya Sita na Makinda ambao angalau wabunge walikuwa wanaongea na kutoa maelekezo kwa serikali kwa pamoja.
Kama Kiongozi wa Bunge unatakiwa uhakikishe unarekebisha tofauti hizo la sivyo hata wewe hutapenda kuona unaongoza chombo ambacho hakina maelewano. Najua kuna watu wengine wangependa kushabikia kuadhibiwa kwa wapinzani. Lakini wewe kama kiongozi hakikisha Bunge linakuwa moja wakati wote ili liweze kusimamia serikali.
Nimeona nilete ushauri huu moja kwa moja kwako kwa kuwa huyu msaidizi wako hataki na wala hatakubali kutafuta suluhu kwa kuwa yeye ndio katibua hali ya hewa.
Inawezekana CCM wakapenda hali hii iendelee ili kuwakomoa wapinzani ila mimi nakushauri itisha kikao cha uongozi wa Bunge au uunde kamati ya maridhiano kama ilivyokuwepo kwenye Bunge la katiba.
Mwisho, natambua kuwa sheria za Bunge zipo ila sio kila jambo utatumia sheria. Mambo mengine ni busara inaweza kuamua na maisha yakaenda. Nakumbuka enzi za kina Sita na Makinda sio kweli kuwa hawakuwa wanafuata sheria bali busara ilitumika na ndio maana masuala mazito yaliweza kujadiliwa kwa mapana.
Lakini kwa kufuata sheria bila busara sifikirii kama masuala mazito yanaweza kupewa nafasi na kujadiliwa Bungeni hasa yale machungu kwa serikali. Maana ili mbunge alete hoja atatakiwa alete ushahidi kamili kitu ambacho hata huo ushahidi utaambiwa umeiba nyaraka za serikali.