Ndugai: Chenge,Ngeleja kuenguliwa mwezi ujao

Ndugai: Chenge,Ngeleja kuenguliwa mwezi ujao

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Job-Ndugai-December11-2014.jpg

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai

Wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge, watavuliwa rasmi nyadhifa zao Januari, mwakani, ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 321 katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wenyeviti hao ni Andrew Chenge wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Bajeti, Victor Mwambalaswa wa Kamati ya Nishati na Madini na William Ngeleja wa kamati ya Katiba, Sheria na Utawala.

Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema ni lazima Bunge litekeleze maazimio ya Bunge kwa viongozi husika kuondolewa kwenye nafasi hizo.

"Wakati wa vikao vya Kamati za Bunge vitakavyofanyika Januari, mwakani, ndipo hatua zitachukuliwa kwa kila kamati husika kuchagua mwenyekiti wa kujaza nafasi ya viongozi hao…maamuzi ya Bunge lazima yatekelezwe na yatatekelezwa kabla ya Bunge la Januari 27, mwaka 2015," alifafanua Ndugai.

Katika Azimio namba tatu lilisema kuwa, kwa kuwa katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco);

Na kwa kuwa, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao.

Katika mialama ya Benki ya Mkombozi, ilionesha Chenge alipewa kiasi cha Sh. bilioni 1.6, Ngeleja Sh. milioni 40. Mwambalasu ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tanesco ambayo inatuhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP'), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP').

CHANZO: NIPASHE
 
Wakishavuliwa bunge liwakabidhi kwenye vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua za kisheria kama wezi wengine wa kuku!
 
Chenge yumo kwenye kila wizi, yote hii ni kwa sababu hakuna hatua anazochukuliwa. Afadhali China ukiiba unanyongwa tu, hakuna muda wa ujanja ujanja wa kujisafisha.
Ova
 
Chenge atatafuta chimbo jingine humo humo serikalini na ataiba tena, kuvuliwa nyazifa tu haitoshi
 
Wakishavuliwa bunge liwakabidhi kwenye vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua za kisheria kama wezi wengine wa kuku!

Kwa taarifa yako ukiwa mwanasheria mkuu wa serikali ukishatoka kwenye hiyo nafasi huwezi kushtakiwa kwa maamuzi uliofanya wakati wa utumishi wako! hata kwa werema pia..
 
kuwavua vyeo vidogo kama ivyo haisaidii...tunataka kuona wanarudisha pesa na wanaenda jela kama mramba na wengine... mambo ya ushikaji kwa mali ya uma hatuitaji kwa sasa,kama unamvua cheo ambacho akikaa hata kwa miaka 2 haez pata pesa aliyoichota escrow haina maana...
 
Chenge atatafuta chimbo jingine humo humo serikalini na ataiba tena, kuvuliwa nyazifa tu haitoshi

Jamaa ni Lichawiii!!! Si mnakumbuka walinzi wa bunge walimwona anamwaga unga unga mweupe kwenye ukumbi wa bunge? Kuling'oa kunahitajika nguvu ya ziada.
 
chenge ni zaidi ya mpigaji madili. da! yaani kila sehemu yupo. kule kwenye radar alidaka sio chini ya bil 5, majuzi kadaka bil1.6. kwenye meremeta alidaka sio chini ya bil 3. bado kwenye mambo mengine mengi. chenge ni zaidi ya mpigaji.
 
Job-Ndugai-December11-2014.jpg

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai

Wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge, watavuliwa rasmi nyadhifa zao Januari, mwakani, ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 321 katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wenyeviti hao ni Andrew Chenge wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Bajeti, Victor Mwambalaswa wa Kamati ya Nishati na Madini na William Ngeleja wa kamati ya Katiba, Sheria na Utawala.

Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema ni lazima Bunge litekeleze maazimio ya Bunge kwa viongozi husika kuondolewa kwenye nafasi hizo.

“Wakati wa vikao vya Kamati za Bunge vitakavyofanyika Januari, mwakani, ndipo hatua zitachukuliwa kwa kila kamati husika kuchagua mwenyekiti wa kujaza nafasi ya viongozi hao…maamuzi ya Bunge lazima yatekelezwe na yatatekelezwa kabla ya Bunge la Januari 27, mwaka 2015,” alifafanua Ndugai.

Katika Azimio namba tatu lilisema kuwa, kwa kuwa katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco);

Na kwa kuwa, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao.

Katika mialama ya Benki ya Mkombozi, ilionesha Chenge alipewa kiasi cha Sh. bilioni 1.6, Ngeleja Sh. milioni 40. Mwambalasu ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tanesco ambayo inatuhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP’), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP’).

CHANZO: NIPASHE

Ndungai na mkubali, kauli zake kuhusu sakata la Escrow zinamshiko kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom