Ndugai angalia wenzako walivyopigwa kumbo

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,478
3,363
Nianze kwakusema sifungamani na chama chochote cha siasa bali ninawakubali wanasiasa wasioteteatu maslahi ya vyama vyao kwanza bali wananchi kwanza
Nimeamua kumkumbusha Ndugai kwani binadamu huwa na hulka ya kujisahau.Namna anavyoendesha bunge kwa jazba anayosifa moja anaikosa nayo ni uvumilivu kutokana na nafasi.Pia amekua mchama zidi kuliko wadhifa alionao.Ninajua amepata wadhifa kwa ukada wake lakini......its not to that extent

Nakukumbusha juu ya walioipigania CCM kuliko we we.Ukiwekwa nao kwenye mizani utaelea juu.Mfano nakuuliza je unayohadhi kama Nape wewe kwakukipigania chama?haijalishi kama ilikua ajira.Ndugai nakuuliza je Nape nichochote ndani ya chama kwa sasa?

Je ww ndugai unaweza kuvaa viatu vya mzee Warioba?Yaliyojitokeza kwenye bunge maalum la katiba sikuambii unayajua kuliko mimi,amedhihakiwa hadi kuitwa msukule na Komba lakini hakuna hatua yoyote chama wala serikali na hata bunge lilichukua dhidi ya mtukanaji huyo sababu nikwamba aliwafurahisha makada.Wote tumashahidi mzee alinaswa makofi pale chuo kikuu cha Dares salaam na aliyemuadhibu hadi leo anadunda akihubiri UZALENDO,AMANI na UADILIFU ila aliye mpiga mzee Mwinyi alishughulikiwa nikwanini?,Ndugai mimi nakukumbushatu

Simtaji kwa ubaya mzee Samweli Sita(Mungu amuweke anapostahili).Alifanya kazikubwa ya kulinda maslahi ya chama hususan kwenye bunge maalum la katiba,kilichotokea baadae aliomba nafasi kibao hakupata hadi alitishia kwenda mahakamani,je Ndugai unayo historia ya mema ndani ya chama ukilinganishwa na Sitta?
Ndugai nakuuliza kwann Wassira hapiganiwi na chama?Kwanini asingepewa hata ukuu wa mkoa kule Kilimanjaro?Umeona kumbo lingine lililowaudhi baadhi yawanachama wenzako?Hujifunzitu?
Walitupwa mbali akina Lowassa,Pinda,Sumaye,Ahmed Salum nk,naendelea kukuuliza je unayonguvu ya kisiasa kama hao?
Unawajua Sophia Simba,Msambatavangu kilichowakuta juzi na ulinganishe na waliyoifanyia CCM hata ndani ya bunge la katiba lakini WAMEPIGWA KUMBO na mfumo.
Wapo wengi unaowajua kuliko mimi nijuavyo na walishabikiwa isivyoelezeka lakini historia imewatupa mkono na ukada umewavuka
Ndugai nakuambia amini usiamini inaweza kutokea siku ukawa mpinzani ndani ya nchi hii,Sumaye na Lowasa wawe rejea nzuri kwako maana hata wao wangeulizwa kabla wangeapa kutokua wapinzani

Nimalizie kwa kusema tendeni haki wala msitoe hukumu,amueni kesho yake wala sio leo mkiwa mmeudhiwa,waombeni wengine wawashauri wala hisia zenu zisitoe msukumo kwenye kuwaelekeza waliokosa.MaDc na maRC tendeni haki kwani mtasifiwa siotu mkiaga dunia pale historia zenu zikisomwa,lakini hata mkiwa mnaishi humu kwenye huu uwanja wa fujo(dunia)
 
Ndugai nikwambie kitu!!!!

"Mimi ni bwana mungu wako, usiwe na miungu mingine ila mimi" Asema Bwana.

Magufuli sio Mungu!!!! ****** make no mistake
 
Back
Top Bottom