Ndugai anapokuwa msemaji wa serikali bungeni

Sir M.D.Andrew

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
201
Reaction score
37
Ndugu wana jf,nimefuatilia kwa makini vyombo vya habari siku ya leo ambapo masikio ya wengi yameelekea dodoma kikao cha bunge kuanza! Lakini kabla sijafika mbali naomba nieleweke kuwa katika nchi kuna mihimili mitatu yaani bunge,mahakama na serikali,lengo lake ni kila mhimili usimamie mhimili mwingine kwa maana ya checks and balance.Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali,lakini tofauti na dhana hii leo naibu spika bwana ndugai kasema kuwa: Bajeti ya mwaka huu ni nzuri,imelenga kuwaletea maendeleo wananchi wote na kwamba wananchi waendelee kuiamini serikali yao ili itimize malengo yake,bajeti hii ni nzuri na haina sababu ya kutiliwa mashaka,na amekwenda mbali zaidi kwa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa vurugu bungeni hazitakuwepo sababu serikali imekuja na bajeti nzuri yenye kukidhi haja ya mtu mmoja mmoja,hakuishia hapo,pia akawaasa wabunge kufuata kanuni za bunge ili kuepusha mgongano bungeni utakaosababisha wananchi kudharau bunge lao: Hoja yangu ya msingi hapa ni kwanini ndugai kaisemea serikali? Maneno haya yangepaswa kusemwa na waziri mkuu ili bunge li prove,je spika na naibu spika ni sehemu ya serikali? Au bunge linaweza kukaa kama serikali hivyo kujijadili lenyewe na kujisahihisha lenyewe? Jamani kwa akili zangu nahisi bunge limeanza vikao vyake kukiwa na kasoro,ndugai si msemaji wa serikali,hakupaswa kusema hivyo! Nawasilisha.
 
Hilo liko wazi kuwa uongozi wa bunge upo kutetea serikali... sio wananchi.
 
Ndugai ni miongoni mwa watu wasiojielewa kabisa. Bahati mbaya sana mhimili huu wa Bunge ulihitaji kiongozi ukapata Makinda na huyu afisa wanyama pori.
 
Tangu lini Spika wa Bunge wa Nchi hii ni independent?
Wote ni rubber stamp ya serikali!

Ndugai & Makinda are the worst offenders tangu uhuru.
 
Kwa mfumo tulionao wengi wanashindwa kutofautisha chama cha siasa(na hasa wana CCM- chama tawala), serikali na bunge kwa kuwa viongozi wengi wako sehemu zote tatu! Kwa hiyo kiongozi huyo anashindwa kujitofautisha lini na wapi ni mwanasiasa, lini na wapi ni mbunge na lini na wapi ni mtendaji wa serikali!
 
Tulimsikia asubuhi TBC1 aibu ya karne lakini nchi ya watu waliokuzimu tumemuacha aendelee kucheza na akili zatu
 
Huwezi jua labda ametumwa aseme hayo na bikiroboto
Ndugu wana jf,nimefuatilia kwa makini vyombo vya habari siku ya leo ambapo masikio ya wengi yameelekea dodoma kikao cha bunge kuanza! Lakini kabla sijafika mbali naomba nieleweke kuwa katika nchi kuna mihimili mitatu yaani bunge,mahakama na serikali,lengo lake ni kila mhimili usimamie mhimili mwingine kwa maana ya checks and balance.Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali,lakini tofauti na dhana hii leo naibu spika bwana ndugai kasema kuwa: Bajeti ya mwaka huu ni nzuri,imelenga kuwaletea maendeleo wananchi wote na kwamba wananchi waendelee kuiamini serikali yao ili itimize malengo yake,bajeti hii ni nzuri na haina sababu ya kutiliwa mashaka,na amekwenda mbali zaidi kwa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa vurugu bungeni hazitakuwepo sababu serikali imekuja na bajeti nzuri yenye kukidhi haja ya mtu mmoja mmoja,hakuishia hapo,pia akawaasa wabunge kufuata kanuni za bunge ili kuepusha mgongano bungeni utakaosababisha wananchi kudharau bunge lao: Hoja yangu ya msingi hapa ni kwanini ndugai kaisemea serikali? Maneno haya yangepaswa kusemwa na waziri mkuu ili bunge li prove,je spika na naibu spika ni sehemu ya serikali? Au bunge linaweza kukaa kama serikali hivyo kujijadili lenyewe na kujisahihisha lenyewe? Jamani kwa akili zangu nahisi bunge limeanza vikao vyake kukiwa na kasoro,ndugai si msemaji wa serikali,hakupaswa kusema hivyo! Nawasilisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom