Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Kaka kama vile sijakupata hapaNilikuwa nafuatilia Bunge na nikakuta sehemu ambayo walikuwa wanazungumzia suala la Bima za Wabunge - wakijadili kauli ya Kafulila kuwa Wabunge ni "privileged class" kuwa wanapata huduma ya afya wao na watoto wao. Ndugai alipokuwa akijaribu kutoa ufafanuzi alidokeza kitu kuwa wabunge hawana bima ya afya na Bungeni linawafanyia utaratibu. Akatumia muda pia kurusha vidonge vya mwisho na kama utakavyosikia Halima Mdee akataka kupata "taarifa"... well listen
View attachment 33772
sikiliza hiyo audio hapo kwenye postKaka kama vile sijakupata hapa
Nimesikiliza hii Audio, nadhani Mh. Halima Mdee ana haki kabisa kuandika lalamiko rasmi kwa kamati ya uongozi wa bunge kutokana na maneno makali aliyotumia Naibu Spika dhidi yake pale aliposema 'kwa leo nakupuuza'. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa Naibu Speaker huyu hakuwa amesikia ni taarifa gani Mh Halima Mdee alitaka kutoa Bungeni.
Kadri siku zinavyosonga mbele wabunge wa ccm wanazidi kujiamini kuwa wamewashinda wabunge wa CHADEMA. Laiti wangejuwa huku mtaani hukumu wanayolimbikizia wangejirudi. Wao waendelee kutetea posho lakini come 2015 every man and woman will have to fend for him/herself. Na hakuna pa kutokea maana DVD zitapigwa kila kona.
Sure!tena ni tangu mchana.maana hii issue ya kafulila na bima ya afya imeanza asubuhi!mi nimekerwa sana!bunge limekuwa km vikao au mikutano ya kijiji!sauti zinatoka mpaka maneno makali,km kavuta huyo! Siyo mwongozo! Achia kiti! N k!ni aibu sana.Na hasira na hiyo mijitu kusema kweli imechafua hali ya hewa
Mkuu nahisi wabunge wetu wa cdm kama wameishiwa mbinu za kupambana na mbinu za ccm kuzima hoja nyingi mle ndani.hoja nyingi kuzimwa ni ushindi kwa ccm hasa tukiangalia namna wananchi wengi wakiwa bado hawajakomaa na elimu ya democrasia na uwajibikaji wa viongozi.siku zinakwenda na hoja zinazimwa kwa mbinu zile zile huku wabunge wetu wakionekana kama walalamikaji tu bila hatua zozote.cdm tunapaswa kuwa wamoja mle ndani kiitikadi na ki mbinu.inabidi utumike mtindo wa kijeshi wa collective responsibility kulazimisha kusikilizwa na kufanyiwa kazi hoja zao.wabunge wanadhalilishwa mno kama kuambiwa kaa chini! Nakupuuza na kukamatwa kama vibaka tena kwa kejeli!binafsi sitaki kumlaumu spika wala wabunge wa ccm maana wanafanya kazi waliyotumwa! Lakini wabunge wa cdm wanakabiliana vp na uhuni huu? Uhuni umezidi bungeni hakuna hatua na matamko yametuchosha inabidi kutumia sheria zilizopo na za kimataifa kulazimisha demokrasia kuchukua nafasi.tusiwalaumu ccm wanafanya waliyotumwa,cdm wanafanya nini mle kabla hawajarudi kwetu mitaani?Nimesikiliza hii Audio, nadhani Mh. Halima Mdee ana haki kabisa kuandika lalamiko rasmi kwa kamati ya uongozi wa bunge kutokana na maneno makali aliyotumia Naibu Spika dhidi yake pale aliposema 'kwa leo nakupuuza'. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa Naibu Speaker huyu hakuwa amesikia ni taarifa gani Mh Halima Mdee alitaka kutoa Bungeni. Kadri siku zinavyosonga mbele wabunge wa ccm wanazidi kujiamini kuwa wamewashinda wabunge wa CHADEMA. Laiti wangejuwa huku mtaani hukumu wanayolimbikizia wangejirudi. Wao waendelee kutetea posho lakini come 2015 every man and woman will have to fend for him/herself. Na hakuna pa kutokea maana DVD zitapigwa kila kona.