Ndug banda aenziwe kwa haya na wote.

mwakajilae

Member
Mar 11, 2011
58
46
Sitaki kumpongeza Ndg Sata zaidi ntawapongeza watu wawili kwa uchaguzi mkuu wa zambia, ambapo hata wanastahili kupewa tuuzo ya amani,ambapo ni ndugu Lupia Banda na wananchi wa Zambia.kuna sababu ninazotaka nieleze kutokana na msimamo huu kwa kilichotokea Zambia.
Suala ninaloliona ni historia ni kutokana na hulka za viongozi wengi wa Afrika kujenga utamaduni wa kwamba ukisha simikwa na wananchi basi ni lazima umalize awamu zako zote zilizopo kikatiba na zilizonje ya katiba.Kwa mfano viongozi wengi wa Afrika walitarajia vitu vikuu viwili zambia,ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya watu wawili,Banda ambaye ni Rais aliye madarakani na anatetea kipindi chake cha pili kikatiba na Ndugu Sata kutoka chama cha upinzani anaye omba ridhaa ili awaongoze wananchi wa Zambia kwa mara ya kwanza,matarajio ya viongozi wa Afrika ilikuwa ni Banda kushinda ama kushindwa na kugoma kuondoka madarakani ili serikali ya wanachokiita muafaka wa kitaifa itengenezwe ambapo SADC na AU Walikuwa wanaisubiri kwa hamu kuunda tume huku wananchi wakiwa wameshamchagua Sata kwa kura nyingi na wanachinjwa kama kuku kwa maamuzi yao hayo.Lakini kitu hicho hakijatokea zaidi ya Ndugu Comrade Banda kukili wito wa sauti ya wananchi ya Mabadiliko,Sauti ya Zambia waitakayo na siyo Banda aitakayo.Banda alimuunga mkono Sata kwa moyo mkunjufu.,sote tunajua nini kimetokea Kenya,Zimbabwe,Ivory coast na pengine pengi.Kwa hili Ndug Banda historia nchini Zambia na barani Afrika ameiandika na atakumbukwa na ametoa somo,kwasababu historia haioneshi ni kiongozi gani alikubari kushindwa kwa kura kabla ya ukomo wa kimipaka wa katiba yake zaidi ya Banda,alifaa kupewa heshima ya kuwa Katibu mkuu wa umoja wa Afrika iliaongoze njia ya kukubali maamuzi ya wananchi.
Wengine wa kuwapongeza ni wananchi wa Zambia ambao kwao hawalewi na historia ya miongo ya chama,kuanzia miaka ya 1990's ambapo hawakulewa na ushujaa wa Baba wao wa Taifa Mzee Kaunda na chama chake kwenye uchaguzi,walikitupa chama tawala na Kaunda wake na Kuchagua mabadiliko yaani upinzani chini ya Chiluba,Hawakumtuma Chiluba kuiba mali zao bali mabadiliko ya kimfumo yanayohusiana na maisha yao yani kiuchumi,kisiasa na kijamii wakamfungulia mashtaka wakati wa Rais Mwanawasa.Lakini mara baada ya Banda kushika hatamu chini ya miongo miwili ya utawala wa chama chao cha upinzani kilichoshika dola kwa miaka hiyo mingi,wananchi bado hawakuridhishwa na utendaji wa serikali ya chama chao kilichochukua dola kama chama pinzani na kutawala tofauti na matarajio yao hasa hususani maisha yao,usalama wao na Taifa lao.Wameamua kukipa chama kingine ndani ya kapu la upinzani kinchoongozwa na Sata ambaye sasa ndo Rais,.Wazambia hawaangaliii sura wala Historia ya chama bali utendaji,serikali itakayojibu masuala ya msingi ya maisha yao;kiuchumi,kisiasa na kijamnii.Hivyo Ndug Sata alikuwa shuhuda wa maamuzi ya wazambia na anajua kwamba wananchi wake hawlewi na chama bali mabadiliko juu ya uchumi wao,siasa yao na jamii yao,akikoroga watamwondoa na kumfanya awe Rais wa Awamu moja kama mwenzie Banda na Sijui kama atakubali sauti ya wananchi??huku akiwa na Jeshi hatalitamani kulitumia na kutangaza hali ya hatari iliwagawane madaraka??hatutarajii kwani Banda kaonesha kivitendo tafsiri ya Demokrasia.
Sasa Rudi kwa wananchi wa Tanzania na Taifa la miaka50 ya uhuru;Tumethubutu,tumeweza,tusonge mbele.Nadiriki kusema ni miaka ya mwl Nyerere tuu na TANU yake ndipo japo uhuru uliweza kutafsirika na maendeleo yaliendana na miaka ya uhuru kwa miaka ile lakini pia na Raslimali za kipindi kile,lakini siyo sasa;ambapo tunashuhudia msiba wa ujinga ukizidi kulinyemelea Taifa kwa wanaojua kusoma na kuandika kushuka kutoka 80% mpaka 35%, vifo vya watoto chini ya miaka mitano inaongezeka,Elimu inazidi kuwa mzigo hata ile ya kusema Cost Sharing inaondoka mfano serikali imejiondoa kwenye elimu ya chuo kikuu kwa mwanafunzi kukopa na kurudisha zote huku serikali imebaki kama mudhamana mkuu,pia wenzetu waliopewa dhamana wanaju amani ni baraka ya mwenyezi Mungu wakati ni Miundombinu inayojengwa,mwl Nyerere alijenga miundombinu ya amani ambapo mpaka leo tunamshikamano wa kitaifa japo hawa CCM wa leo wanazidi kuivunja
na kuichoma moto.Ni kazi ya watanzania kuamua sasa na siyo wakati ambapo watu watakapoingia msituni na Afrika kusin kuwa mpatanishi!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom