Ndovu arudi Somalia baada ya miaka 20

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
160310110554_morgan_one_640x360_bbc_nocredit.jpg


Morgan alifungiwa kifaa ya kufuatilia mienendo yake mwezi Disemba katika eneo la Tana River pwani mwa Kenya.

Ndovu mmoja kwa jina Morgan amefanikiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Somalia mwezi huu, na kuwa mara ya kwanza ndovu huyo kuonekana nchini humo tangu miaka 20 iliyopita.

Ndovu huyo kwa jina Morgan aliye na umri wa takriban miaka 30, alifungiwa kifaa ya kufuatilia mienendo yake mwezi Disemba katika eneo la Tana River pwani mwa kenya, kati kati ya mwezi Februari kabla ya kuanza safari isiyotarajiwa kuelekea nchini Somalia na kufanikiwa kuwasili mpakani wiki tatu baadaye.

160310110747_morgan_two_640x360_bbc_nocredit.jpg


Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuwa lenye usalama.

Safari yake imewashangaza watunza mazingira ambao wanasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa ndovu huyo alikumbuka njia za zamani baada ya miongo kadha ya kuondoka Somalia kutokana na mapigano.

Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuboreka kiusalama na ikiwa hali itakuwa shwari kusini mwa Somalia, basi ndovu waishio uhamishoni watarudi nyumbani.

Kutoka ene la Tana River Morgan alitembea umbali wa kilomita ishirini usiku wa kwanza kabla ya kujificha ndani ya msitu mkubwa na kuendelea na safari siku iliyofuata. Alirudia mtindo huo kwa siku 18


Chanzo: BBC Swahili
 
Miongoni mwa wanyama wenye hisia Kali ni hawa viumbe aina ya Ndovu ata kipindi cha Tsunami kule Indonesia wengi waliondoka kwa makundi siku kadhaa kabla ya lile tukio kutokea.
 
Duu hongera morgan kwa kupona vihunzi katika safari yako. Ila usithubutu kurudi kenya usije kosea ukaingia Tanganyika msomali mwenzio(kinena) atakufanya kitu mbaya!









Duu hongera morgan kwa kupona vihunzi katika safari yako. Ila usithubutu kurudi kenya usije kosea ukaingia Tanganyika msomali mwenzio(kinena) atakufanya kitu mbaya!




Angalia hii usitamke mbele ya mama yako ataon unatak upajue kwake ulipotokea
 
Back
Top Bottom