Ndoto za mke wa mtu zinanitesa

Ndoto za mke wa mtu zinanitesa

mgaya chacha

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
497
Reaction score
658
Habari wana JF!

Niliwahi kuwa na mahusiano ya mapenzi na dada mmoja toka tukiwa shule ya msingi na baadae sekondari na hata baada ya shule tuliendeleza mahusiano yetu.

Baadae yeye akapata ajira kapelekwa mkoani mimi nikabaki bado nasota. Na mimi baada ya miaka 2 nikapata ajira ila sikudumu nayo baada ya mwaka 1 nilipoteza ajira nikaamua kurudi nyumbani ila kabla ya kufika nyumbani nikaamua nishuke mkoa fulani kujaribu maisha bahati nzuri ndiyo mkoa aliokuwa anafanya kazi.

Nikampigia simu nikampata tukafurahi sana kuonana ila aliishabadilika kutokana na kazi aliyonayo akawa si yule tena. Nikaamua kwenda kuishi guest house ili kujipanga upya nikitafuta pa kuanzia.

Baadae alipohamishwa kikazi akaniomba nije nimuangalizie chumba chake, sikukataa maana bado sikuwa vizuri. Baadae alirudi kuchukua kilicho chake tena kwa kushitukiza na kuniacha nalala chini.

Baada ya miaka kadhaa nikaambiwa kazalishwa na jamaa na akamuacha na kipindi hicho Mungu aliishanibariki nikapata kazi nzuri nikapanga nyumba nzima.

Siku anaenda kwao likizo akaniomba afikie kwangu huku akisema hata kama nitakuwa nalala chini atalala ili mradi apate pakufikia ili kesho yake aendelee na safari. Sikumkatalia maana yeye ndiyo aliyenipokea mjini.

Hakuamini baada ya mimi kwenda kumpokea na gari na kumpeleka nyumbani nilipokuwa nimepanga nyumba nzima. Alichosema ni "hapa ni kwako au kwa rafiki yako?" Sikuwa na jibu!

Basi alikaa siku mbili bila kumgusa/kusex akaondoka. Alivyorudi baada ya likizo pia akapitia kama kawaida ili baadae aendelee na safari na kesho yake akaondoka.

Baada ya miaka miwili nikasikia amepata mtoto mwingine na jamaa mwingine. Bahati mbaya akapewa uhamisho kuja huku mkoa niliopo huku akiwa na mtoto wa wiki mbili. Akaniomba afikie kwangu nikamkatalia aliendelea kuomba kama wiki mbili hivi baadae nikaona huruma nikamwambia njoo. Huko alimuaga mmewe kuwa anafikia kwa kaka yake.

Alikuja nikampa chumba yeye na housegirl wake na watoto wake wawili, tuliishi kama dada na kaka kwa miezi minne. Lakini baada ya hapo siku moja nilitoka job nikiwa nimechoka sana baada ya msosi nikaenda kulala chumbani kwangu. Usiku wa manane nilishtuka baada ya kukuta tupo wawili kitandani hata sikujua alikuja saa ngapi.

Nikamuuliza vipi uko huku? Akajibu amechoka kunivumilia ameamua anifuate hukuhuku. Nikamwambia ujue wewe ni mke wa mtu, akanijibu yule wamejuana juzi mimi tulijuana toka kitambo.

Hapo ndipo tulipoanza ukurasa mwingine wa mapenzi. Hakika tuliishi kwa Amani na furaha kupita kiasi mpaka watoto walijua mimi ndiyo baba yao wakanifurahia sana. Baada ya miezi kadhaa jamaa yake alimpagishia chumba ikamlazmu kuhama japo kwa shingo upande. Akawa havumilii kwa wiki lazima aje mara 2 kupewa shughuli.

Baadae jamaa akaenda kwao akalipa mahali hapo ndipo nilipoanza kuogopa kushare nae tena ikawa vita mimi na yeye. Yeye anataka mimi sitaki.

Miezi miwili iliyopita wameoana na mawasiliano yamekatika kabisa. Sasa najikuta namkumbuka sana tena sana ila najizuia nisimpigie nikikumbuka tulivyokuwa tunacheza ndani kama watoto huku tukikumbushana tilivyokutana primary miaka ya 96 mpaka sekondari basi ilikuwa ni furaha hasa nikiwa nadrive pekee yangu huwa najikuta natabasamu mwenyewe kwa kumkumbuka.

KIBAYA KULIKO VYOTE NAPATA NDOTO ZAKE MARA KWA MARA TUKIWA NA FURAHA SANA YÀANI NAOTA TUNACHEZA TUNAFURAHI SANA TUPO WOTE. NIKISHTUKA NAJIKUTA PEKE YANGU NAUMIA SANA ILA NAJIKAZA SANA NIMESHINDWA HATA KUWA NA MTU MWINGINE MAANA KILA NIKITAZAMA SIONI WA KULINGANA NAE. HAKIKA NILIMPENDA SANA YEYE NA WATOTO WAKE WOTE WALINIPENDA SANA MAANA NILIWAJALI PASI KUJALI KUWA SI WANGU.

Je nifanye nini niache kumuota?
 
niamini mimi, na yeye anakuwaza hivyo hivyo.

Sasa usimtafute jifanye kama haupo, piga mishe zako utashangaa atakapotokea.

Wanaume wa Dar tunaendesha training za mapenzi mshtue mwenzio
 
niamini mimi, na yeye anakuwaza hivyo hivyo.

Sasa usimtafute jifanye kama haupo, piga mishe zako utashangaa atakapotokea.

Wanaume wa Dar tunaendesha training za mapenzi mshtue mwenzio
Toka niliposikia kalipiwa mahali niliacha kumtafuta yeye ndiye alikuwa kero kwenywe kunisaka ila nilimkatalia katakata mpaka siku ya kufunga ndoa alinipigia na kulaumu kwanini? Sikuhudhuria harusi yake na kuniuliza eti! Ina maana nimeamua kumuacha baada ya kuolewa nilimjibu ndiyo kuolewa ndiyo mwisho wa mahusiano yetu akasema hakubali aliendelea kupiga simu kutuma sms ila sikujibu wala kupokea wiki moja baadae akaacha na sasa ni miezi mitatu tupo kimya japo tunakaa mji mmoja.
 
Toka niliposikia kalipiwa mahali niliacha kumtafuta yeye ndiye alikuwa kero kwenywe kunisaka ila nilimkatalia katakata mpaka siku ya kufunga ndoa alinipigia na kulaumu kwanini? Sikuhudhuria harusi yake na kuniuliza eti! Ina maana nimeamua kumuacha baada ya kuolewa nilimjibu ndiyo kuolewa ndiyo mwisho wa mahusiano yetu akasema hakubali aliendelea kupiga simu kutuma sms ila sikujibu wala kupokea wiki moja baadae akaacha na sasa ni miezi mitatu tupo kimya japo tunakaa mji mmoja.
Miezi mitatu huna mpenzi mwingine? Tafuta mpenzi halafu endelea na kukaa kimya, anarudi huyo.
 
Miezi mitatu huna mpenzi mwingine? Tafuta mpenzi halafu endelea na kukaa kimya, anarudi huyo.
Arudi wakati tayari ni mke wa mtu na walizaa kabla ya ndoa si janga hilo kibaya zaidi Jamaa lake ni Ri CID la polisi si ntapewa kesi ya Kibiti wala sikubali
 
Back
Top Bottom