Ndoto yangu ya urais

Ndoto yangu ya urais

zema21

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
619
Reaction score
257
Wana jamvi nimeota kuwa nimepata urais wa JMT, katika ndoto yangu nikawa nawaza nitawafanyia nin waTz, kama ndoto hii ingekuwa ya ukweli ningefanya yafuatayo.

1..Ningejenga umoja ushirikiano na usawa kwa watanzania pasipo kujali kabila wala dini ya mtu. Ningewaunganisha wananchi waishi kama ndugu badala ya kuwagawa kwa udini, ukanda na ukabila.

2. Wananchi wangu wangeishi kwa furaha na amani bila kuhofu chochote. Kwani pasingekuwepo na m2 wa kuwanyanyasa.

3. Ningehakikisha rasilimali za waTz zinawanufaisha waTz wote kwa usawa, badala ya wazungu na mafisadi wachache.. Ardhi ya wananchi isingeporwa wala wasingenyanyaswa kwenye ardhi yao. Ningehakikisha tembo faru n.k hawauliwi ovyo na mafisadi kwa ajili ya kujitajirisha.

4. Ningesafiri safari zisizozidi tano kwa mwaka kwenda nje ya nchi. Zile nyingine za muhmu wasaidizi wangu wangeniwakilisha Ningepunguza kwenda misibani na kwenye sherehe.

5. Ningepunguza kukopa ili kupunguza deni la Taifa. Ningepunguza kuomba omba ningetumia rasilimali za ndani ya nchi kama vile madini, sekta ya utalii, gesi kwa ajili kujenga uchumi wa nchi na kuwasaidia wananchi kuinuka kiuchumi kama nchi ya botswana wanavyofanya. Wawekezaji wa ndani wangepewa kipaumbele na kujengewa uwezo.
Gharama za chai, posho zisizo na tija ningezitoa.

6. Ningewatimua wezi na mafisadi serikalini hata kama ni rafiki zangu ningewapeleka mahakamani kwa hatua za kisheria. Nisingemchekea hata mmoja.

7. Ningehakikisha jeshi la polisi haligeuki kuwa shubiri kwa wananchi wake badala yake lingelinda raia na mali zao. Ningekomesha mauaji ya wasio na hatia kama marehemu Mwangosi (R.I.P), ningehakikisha manyanyaso na mateso kama ya dr ulimboka.. Kesi zote zingeshughulikiwa kama ile ya marehemu kamanda ballow (R.I.P). Maandamano yangekuwa haki ya msingi ningemwajibisha yeyote ambaye angewapiga mabomu au risasi.

8. Ningehakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa huru na vinafanya bila vitisho wala kufungiwa vile vinavyoendesha miadhara ya chokochoko za kidini zinadhitiwa.

9. Ningehakikisha kuwa vijana (nguvu kazi ya taifa) wanajengewa uwezo wa kuwa wazalishaji, kwa kuajiriwa au kujiajiri badala ya kuwalaumu.

10. Ningeteua watu kulingana na sifa stahiki na wala sitajali kigezo cha ushkaji wala undugu na udini

Je wewe mwanajamvi ungenipa kura yako?
 
du,kama rais anaweza kumfunga raia wake kwa utashi wake,muhimili wa mahakama ukiwa umeachwa huko,basi huyu rais ni dikteta.mie nisingekuchagua.
 
Mahakamani lazima ukamshtaki mwizi, ni lini umeona mahakamani kesi inaendelea afu hakuna mlalamikaji?
du,kama rais anaweza kumfunga raia wake kwa utashi wake,muhimili wa mahakama ukiwa umeachwa huko,basi huyu rais ni dikteta.mie nisingekuchagua.
 
Keep on dreaming!!!??

Tatizo CCM hawalali wanaiba masaa 24. Wao swala la kuota halipo ni kazi mbele kwa mbele kuifilisi nchi yetu. Period!!
 
Get a vision kaka. huwezi kujenga vision yako ya kua Rais
based on what Rais ambae yupo madarakani sasa hivi anakosea.
Mfano, huwezi kusema uta-limit safari zako to five. Based on what?
maana safari zingine huwezi kupanga, zinatokea tu, tokana na circumstances.
Kama umesha enda safari tano, halafu itokee mkutana wa head of states wa SADC
wewe huendi sababu umesha safiri mara tano?


Mfano mngine: Ungetumia rasilimali za nchi kuleta maendeleo,
but do you know Tanzania tayari inategemea ressources ya riches zake kuliko inavo takiwa
na hivo kua katika "frail countries" zinazo weza ku-develop resource
curse?
How do you increase the country dependency on riches rents
na kuhakikisha government inawanawajibika kwa wananchi wasio lipa kodi?

Mengine are easier said than done.
Wewe ungeteuwa watu kufatana na uwezo wao (competence)
but ungehakikishaje kua na wenyewe wanafanya hivo?
you can't control everything. So leadership inajengwa pia.
sio kuamka tu na kusema kuanzia leo hakuna udini wala ukabila.

You have to inspire, motivate and sanction people to get them around that positive vision.
 
Wewe umefanya kazi ya kumjibia Nape maswali aloulizwa leo hii humu ndani ya jf nakushindwa kujibu. Umeleta majibu yake na ningefikiria mala mbili kabla ya kukuopa kura kwani hujaonyesha baadhi ya majukumu muhimu jinsi ya kuyahandle. Like mahusiano ya nje, ujenzi wa uchumi hauwezi kutegemea madini, gasi na utalii tu; usalama wa nchi na afya za watu wako, n.k
 
Rasilimali nilizotaja hapo juu ni kwa uchache ila zipo lukuki za kuweza kuendesha nchi, kuna mianya mingi ya upotevu wa fedha za serikali kama posho zisizo za lazima, marupurupu yasio lazima, misamaha ya kodi isiyo na tija, kodi ndogo kwa baadhi ya sekta zenye mapato makubwa, ukwepaji kodi, mishahara hewa. Haya yote yakidhibitiwa fedha zake zingeenda katika huduma za kijamii, pia kumbuka uwekezaji unahitaji uwekeze katika rasimali watu kwani ndio ki2 muhmu kuliko vyote.. Ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kupata elimu bora, huduma bora za afya na huduma nyingine muhmu za kijamii, hapa utajenga taifa lenye nguvu kazi kubwa.
Wewe umefanya kazi ya kumjibia Nape maswali aloulizwa leo hii humu ndani ya jf nakushindwa kujibu. Umeleta majibu yake na ningefikiria mala mbili kabla ya kukuopa kura kwani hujaonyesha baadhi ya majukumu muhimu jinsi ya kuyahandle. Like mahusiano ya nje, ujenzi wa uchumi hauwezi kutegemea madini, gasi na utalii tu; usalama wa nchi na afya za watu wako, n.k
 
Get a vision kaka. huwezi kujenga vision yako ya kua Rais
based on what Rais ambae yupo madarakani sasa hivi anakosea.
Mfano, huwezi kusema uta-limit safari zako to five. Based on what?
maana safari zingine huwezi kupanga, zinatokea tu, tokana na circumstances.
Kama umesha enda safari tano, halafu itokee mkutana wa head of states wa SADC
wewe huendi sababu umesha safiri mara tano?


Mfano mngine: Ungetumia rasilimali za nchi kuleta maendeleo,
but do you know Tanzania tayari inategemea ressources ya riches zake kuliko inavo takiwa
na hivo kua katika "frail countries" zinazo weza ku-develop resource
curse?
How do you increase the country dependency on riches rents
na kuhakikisha government inawanawajibika kwa wananchi wasio lipa kodi?

Mengine are easier said than done.
Wewe ungeteuwa watu kufatana na uwezo wao (competence)
but ungehakikishaje kua na wenyewe wanafanya hivo?
you can't control everything. So leadership inajengwa pia.
sio kuamka tu na kusema kuanzia leo hakuna udini wala ukabila.

You have to inspire, motivate and sanction people to get them around that positive vision.
ningehakikisha nafanya delegation of power, safari zisizo na ulazima wanaenda wengine kama waziri au wakurugenzi kutegemea wizara, hvyo safari zangu zisingekuwa nyingi.

Ningeunda organ ambayo ingekuwa very strong ingehusika na ukusanyaji wa mapato, sheria ya mapato ingekuwa makini dhidi wakwepa kodi pasipo kujali jina wala sura! Ningeondoa misamaha ya kodi isi na tija.

Ningeongeza thaman ya resource zetu, pasipo kujilinganisha na hizo "frail countries" ningehakikisha tunapata mapato sawa.

Ningefanya evaluation ya mara kwa mara na kila wizara kuona kama vision yetu imefikiwa na kama imefiwa ningejua wafanyakazi wangu ni wachapakazi, na wanafiti, kama ni jaji akashindwa kuandika hukumu ningemtimua
 
nitahakikisha familia yangu haijihusishi na mambo ya siasa,na watoto wangu watakuwa sio mabilionea
 
wa jf niambieni juu ya haya mmenipa kura?
 
wa jf niambieni juu ya haya mmenipa kura?

Kwa ufafanuzi huu mkuu mie nakupa kura ila nami nafaa kuwa PM wako kama ukiniamini. Ila tunapitia chama gani kitakacho tufaa au twende binafsi?
 
Bora hata ikawa SAU kuliko magamba
Kwa ufafanuzi huu mkuu mie nakupa kura ila nami nafaa kuwa PM wako kama ukiniamini. Ila tunapitia chama gani kitakacho tufaa au twende binafsi?
 
Back
Top Bottom