Jogoli
Member
- Jun 20, 2016
- 36
- 45
Nimekuwa nikiota kitu kama ndoto ya ajabu, sikumbuki vizuri huwa inaanza vipi, lakini ninachokumbuka huishia na kulipukiwa na kitu kama Bomu usoni kwa nguvu "Puuuuuuuuuh!". Wakati mwingine nahisi kama kichwa kimesambaa.
Huo mlipuko ukishatokea tu hujihisi kama nimerushwa, na hapo nashtuka wakati huo huo namkuta mke wangu nae kashtuka kwa taharuki akiniuliza " kuna nini? Mbona umeshtuka hivyo?" Nami humjibu ni ndoto tu bila kumueleza ni ndoto ya aina gani. Kilichonifanya niandike usiku huu ni baada ya mke wangu kushtuka kwa nguvu usiku huu kama amerushwa na kitu.
Nilipomuliza kaniambia kaota kama analipukiwa na moto usoni kwa nguvu, nilivyomdadisi sana maelezo aliyonipa ni sawa sawa na ndoto au hali ambayo na Mimi imenikumba kama Mara NNE. Na Mara ya mwisho Mimi kutokewa na hali kama hiyo ni juzi.
Je hii itakuwa ni kitu gani? Kama ni ndoto itakuwa inamaanisha nini? Na kwann kitu hicho hicho kinitokee mimi na mke wangu? Najua humu kuna wataalam mbali mbali naamini nitapata ufafanuzi juu ya hili jambo. Na je labda kuna MTU mwingine alishawahi kutokewa na hali kama hiyo akiwa usingizini.
Sent using Jamii Forums mobile app