Wasalaamu,
Kwa muda wa takribani miaka 12 nimekuwa nikiota ndoto baada ya muda mfupi hutokea tukio halisi likiashiria ndoto niliyoota.
Mfano, mwaka 2006 nilikuwa najisomea usiku, tena nilikua na nguvu ya kusoma kweli siku hiyo usiku, malengo yangu ya usiku huo ilikuwa nisome hadi saa 8 usiku, kipindi hicho dada yangu alikuwa ana mimba, ilipofika saa 6 usiku ghafla nikajihisi kuchoka nikahisi usingizi. Ile kulala tu kama dakika 1 nikaota kama katoto kachanga keupe kamezaliwa nakaona kwenye mboni za macho yangu. Kesho asubuhi naamka dada yangu akanipigia simu, bwana flani umepata mjomba wa kiume anaitwa Given. Nikareflect na ndoto ya usiku nikakausha tu.
Mwaka 2008 niliota ndoto ya mazishi, kweli kesho yake mtoto wa mama angu mdogo alifariki, alikuwa mdogo wangu tuliokua tunaishi nae nyumbani.
Mwaka 2011, niliota ndoto tena ya kifo, siku si nyingi babu yangu mzaa mama alifariki,
nilikaa wiki moja, nikaota tena ndoto kama ile bibi mzaa mama akafariki.
Mwaka 2012 kope za chini zilicheza sana wakati nikiwa mdogo tuliambiwa ukiona kope za chini zinacheza ujue kuna tukio sio zuri litatokea, kweli siku si nyingi bibi yangu mzaa baba alifariki.
Kama wiki imepita, nilisumbuliwa sana na ndoto za mazishi, muda si muda nikapigiwa simu babu yangu mzaa mama pia amefariki.
Jana usiku niliota tena ndoto ya mazishi leo asubui napigiwa simu rafiki yangu kipenzi amefariki kwa ajali ya boda boda.
Imefika wakati nikiota ndoto kama hizi naanza kuwaza, sijui leo itakuwa zamu ya nani hii ndoto imemlenga. Najawa na mawazo, ndoto ikitimia, isipotimia namshukuru Mungu.
Kwa wazoefu, hizi ndoto chanzo chake nini?
cc mshana jr,
nawasilisha