bachelor sugu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 2,689
- 3,651
Amani iwe juu yenu.
Ndugu zangu nimekuwa na ndoto ambayo imekuwa ikinitesa sana katika maisha yangu,
Ni ndoto ya kutamani siku moja nimiliki kampuni ya UOKOAJI katika majanga mbalimbali isipokuwa majanga ya moto.Majanga ninayoyakusudia hapa zaidi ni ajali za Barabarani pamoja na zile za Majini bila kusahau ajali zingine km za treni,majengo n.k
Ndoto hii nakumbuka iliibuka ghafla kipindi kile ilipotokea ile ajali ya treni Dodoma katika vile vijiji vya Msagali sikumbuki na kijiji gani ila wote tunakumbuka iliua maelfu ya ndugu zetu.Iliendelea kunitesa pia zilipotokea zile ajali 2 za meli za kule Nungwi za MV Skagit na Spice Islander bila kusahau matukio ya ajali za barabarani ambazo zinachukua maisha yetu kila uchao.
Ni kweli tuna jeshi la zimamoto na uokoaji ila kiukweli nadhani limeelemewa na bado linafanya kazi kianalogia/Kizamani mno hali inayopelekea watu wengi katika ajali huwa kwa kukosa msaada wa oukozi wa haraka.
Ndoto hii inanitesa kwa kuwa inahitaji investment/Uwekezaji ambao nashindwa kuelewa kama nitakuja kuufikia mpaka naondoka ktk dunia hii maana ninahisi nitahitaji vifaa vya mabilioni km ifuatavyo
--Helicopter walau 2 always standby
--Heavy Crane motovehicles walau 4 ziwepo katika kanda 4 za nchi hii.
--Boti ziendazo kasi walau 5 zigawanywe katika maziwa na baharini.
--Vifaa vya Kisasa vya kukatia vyuma vigumu.
---Jeki zenye uwezo wa kunyanyua vitu vizito sana na za kisasa.
--Well tranned Resque squad.
Vingine vi naweza kuwa vya kawaida.
Kutokana na picha ya hiyo investment nalazimika kuendelea kuuumia na hakika naweza kufa nikiwa sijaitimiza ndoto yangu hii na kinachouma ni pale unapobahatika kupata nafasi ya kufika katika eneo la ajali na KUMSHUHUDIA MTU ALIYEBANWA NA VYUMA AKIKUOMBA MSAADA UMUOKOE HUKU AKIKUAHIDI KUKULIPA HATA KILE ASICHOKUWA NACHO ILI MRADI TU UWEZE KUMUOKOA ila kwa kuwa huna uwezo basi unashuhudia pia hadi mtu huyo anakata roho mbele yako,hakika niliwahi kuuumia kwa hili.
Tafadhalini ndugu zangu naombeni japo mawazo kidogo namna gani hata naweza kuliweka katika maandishi tu at least nijue niliwahi kujaribu kitu hili katika uhai wangu japo nilikwama kutokana na uwezo wangu licha ya kuwa naamini hakuna kisichowezekana chini ya jua.
Wenu BACHELOR SUGU.