kabon14
JF-Expert Member
- Jun 14, 2016
- 1,233
- 867
Wakuu naombeni msaada wa tafsiri ya ndoto hii, jana nimeota kuwa nipo maeneo fulani nimevaa gwanda za FFU ghafla nkakutana na askari kibao wametanda barabaran njiapanda hivi wakiwa kama wanasaka kitu fulani (kwa walioko Dodoma ni pale ilipo Airtel shop)
Kutokana na hofu nilishtukiwa na afande mmoja akaniuliza kitu ambacho sikumbuki ni nini, nikamuita pembeni nikamwambia bro naomba unisamehe na usiwaambie wenzako please, naomba unitoe eneo hili akakubali.
Tukiwa njiani kuelekea kusikojulikana tukakutana na askari wengine wengi sana wakiwa kwenye paredi, jamaa yaonekana alikuwa mkubwa alipokaribia akawaamulisha wakafungua mguu (mguu pande), nikiwa katika hofu sana nilitembea kwa kutetemeka hadi nikasikia minong'ono miongoni mwa askari waliokuwa pale.
Tulifika sehemu inayoonekana kuwa ni nje ya mji kwenye mashamba ya watu, niliwaona jamaa fulani wanalima tuliwasemesha (sikumbiki tuliwasemesha nini) tukakatiza katikati ya mashamba kutafta njia, mbele kulikuwa kama na korongo fulani lililotuzuia kupita, tukapinda kulia hivi, kulikuwa na nyumba fulani ndogo hivi inayoonekana ubavuni, kwa mbele kulionekana barabara ya lami na magari yalionekana kupita.
Yule Askali akaniambia sasa tafuta barabara inayoelekea Babati au Arusha urudi, nilishangaa sana kwanini jamaa kanifikisha mbali hvo na sijui narudi vipi Dodoma maana sikuwa hata na mia mfukoni.
Wakati na tafakari jamaa sikuona alipopotelea ghafla wakaja mabinti wawili ninaowafahamu, ambao sikuwa na wazo la kujiuliza wametokea wapi kwa sababu tulikuwa pembeni ya nyumba ile.
Basi wakanisemesha (sikumbiki tuliwasemeshana nini), dada mmoja akaniambia kuwa anapenda shati langu huku akilishikashika, ghafla nikagundua sijavaa gwanda za FFU tena bali ni nguo fulani kama rangi ya maziwa hivi.
Wakati akishika shati langu nikagundua kuna maandishi mengi sana kwenye suruali yangu mguu wa kulia yaliyoandikwa kwa kalamu ya wino.
Nilishangaa sana na kujiuliza yametoka wapi, baada ya kuchunguza vizuri nikagundua sio maandishi bali ni namba nyingi sana zimeandikwa na kutengeneza kama umbo la mraba hivi.
Niliangalia kwa umakini nikaona kuna namba tatu zimeandikwa kwa wino mwekundu ambazo ni 1, 3, na 7 halafu kuna moja ya mwsho iliandikwa kwa wino wa blue kama zingine ila naikumbuka kwa sababu ilikuwa ni ya mwsho upande wa chini kulia mwa umbo lile la mraba na ilikuwa haijaandikwa kikamilifu na ilikuwa kubwa kuliko zote, nayo ni namba 8 (iliandikwa as if mwandishi alikuwa na speed kubwa hivyo haikufungwa vizuri upande wa juu kulia).
Baada ya hapo nilishtuka toka usingizini.
Naombeni mchongo wa mawazo yenu.
Sent using Jamii Forums mobile app